Jinsi kipimo cha mimba kinavyo fanya kazi
Je, una shaka kuwa huenda ukawa na mimba?
Njia za kudhibiti uzazi huenda zikawa na nafasi ya kasoro. Hata kama umekuwa ukitumia mbinu fulani ya kudhibiti uzazi kwa muda mrefu na haijai enda mrama. Kuna nafasi ndogo ya mbinu hizi kuto zuia mimba wakati wote. Kondumu zimesemekana kupasuka mara nyingi na inapo pasuka. Inamtia dada anaye husika katika hatari ya kupata mimba. Kuna mbinu tofauti unaweza tumia kupima mimba. Kama vile kupima mimba kwa kutumia kitunguu maji ama kwa kutumia kipimo unacho nunua kwenye maabara ama zahanati.

Je, unapaswa kuchukua kipimo cha mimba baada ya muda upi?
Mara nyingi, unashauriwa kupima mimba baada ya kukosa kipindi chako cha hedhi. Wiki mbili baada ya kufanya ngono isiyo salama. HCG ambayo ni homoni inayo tolewa ukiwa na mimba huwa kwa viwango tofauti kwa watu tofauti. Ili kupata vipimo sawa, unapaswa kungoja hadi viwango vya HCG tosha vianze kutolewa mwilini. Huchukua muda wa siku saba hadi kumi na mbili. Kwa muda huu, yai huwa lime pandikiza kwenye kuta za uterasi. Kufanya kipimo mapema sana kunaweza sababisha matokeo yasiyo sawa.
Je, Ishara Za Kuwa Na Mimba Ni Zipi?
- Kukosa kipindi chako cha hedhi
Mojawapo ya ishara maarufu na inayo aminika zaidi ni kukosa kipindi chako cha hedhi.
Ikiwa hauko makini sana na hedhi yako, huenda ikawa vigumu kwako kugundua kuwa kipindi chako cha kila mwezi kimechelewa. Unashauriwa kufanya kipimo cha mimba ikiwa imekuwa zaidi ya mwezi mmoja tangu ulipo shuhudia kipindi chako cha hedhi.
Mbali na mimba, kuna sababu tofauti ambazo zinachangia kuchelewa kwa kipindi chako cha hedhi. Hizi ni kama vile, kukwazwa kimawazo, lishe, kubadili mazingira, mazoezi ama ugonjwa.
Kuwa makini kwa hedhi yako kwani huenda ukapata damu inayo toka baada ya yai kushikilia kuta za uterasi. Aina hii ya damu ni nyepesi na ya pinki. Pia unashauriwa kuwasiliana na daktari wako ikiwa kipimo cha mimba ni chanya na bado una shuhudia kipindi chako cha hedhi. Huenda ukawa na maradhi.

Hii huwa mojawapo ya ishara za mapema za kuwa na mimba. Chuchu zako zinakuwa laini na chungu.
Ishara hii hushuhudiwa na baadhi ya wanawake. Lakini wengi wao huhisi uchovu na kuumwa na mgongo wanapokuwa na mimba. Ukikosa kipindi chako cha hedhi kisha uanze kuumwa na mgongo. Hakikisha kuwa unafanya kipimo cha mimba kudhibitisha ikiwa una tarajia mtoto ama la.
Kupandikiza kwa yai kwenye kuta za uterasi husababisha kuumwa na tumbo. Sawa na ukishuhudia kipindi chako cha hedhi. Huenda ukahisi uchungu huu na kungoja kipindi chako cha hedhi lakini ukakikosa. Fanya kipimo cha mimba kwenye zahanati ama kupima mimba kwa kutumia kitunguu maji kudhihirisha ikiwa una mimba ama la.
Unapo shuku kuwa una mimba, ni vyema kufanya kipimo ili kujua ukweli wa mambo ulivyo. Watu tofauti huwa na mbinu tofauti wanazo penda kutumia kupima mimba. Ikiwa ungependa kufanyia kipimo chako nyumbani bila kuwajuza watu wengi shaka zako, unaweza fanya kipimo cha baking soda, ama kutumia chumvi kupima mimba, ama kupima mimba kwa kutumia kitunguu maji. Kwa sababu vipimo hivi bado havina ushuhuda wa kisayansi unao dhihirisha kuwa bila shaka ni vya kuaminika, unashauriwa kwenda kwenye hospitali iliyo karibu nawe kupata matokeo sahihi.
Soma pia: Mambo Yote Unayo Paswa Kujua Kuhusu Homa Ya Corona Na Ujauzito