Jinsi Ya Kupima Mimba Kwa Kutumia Mafuta Ya Kula

Jinsi Ya Kupima Mimba Kwa Kutumia Mafuta Ya Kula

Kipimo cha kupima mimba kwa kutumia mafuta ya kula ni mojawapo ya vipimo maarufu vya kinyumbani. Soma jinsi kinavyo fanyika!

Kuna sababu nyingi ambazo zina athiri kipindi cha hedhi kisicho cha kawaida ama mwanamke kukosa kipindi chake cha hedhi. Wanawake wanao tamani kupata mimba huenda wakawa na fikira nyingi na wasiwasi mwingi kuona kama watapata kipindi chao cha hedhi mwezi huo. Kwa wasio kuwa tayari kuwa mama, huenda bado wakawa na shaka na kutaka kujua kama wana mimba ili kupunguza uwoga wao. Ikiwa una shuku kuwa una mimba, unaweza tumia kipimo cha kupima mimba kwa kutumia mafuta ya kula kudhibitisha kama una tarajia ama la.

Aina ya vipimo

kupima mimba kwa kutumia mafuta ya kula

Kuna vipimo vingi ambavyo mwanamke anaweza tumia kudhibitisha kuwepo kwa mimba ama la.

  • Vipimo vya hospitalini/maabara

Kuna vipimo vinavyo fanyika hospitalini kama kipimo cha damu kwenye maabara. Ama kutumia kipima ujauzito. Vipimo hivi vina pima kichocheo cha HCG (human chorionic gonadotropin). Vipimo hivi vinaweza dhibiti hali ya mama kabla ya kipindi chake cha hedhi kufika ama kukosa. Homoni hii hutolewa mwilini yai linapo jipandikiza kwenye kuta za uterasi siku 11 ama 14 baada ya kutunga.

  • Vipimo vya nyumbani

Kuna vipimo tofauti ambavyo mama anaweza fanyia nyumbani kufahamu hali yake ya mimba. Kipimo cha mimba kutumia chumvi, kipimo cha mimba kutumia sukari, kupima mimba kwa kutumia mafuta ya kula na vipimo vingine. Ni muhimu kuenda hospitalini baada ya kufanya kipimo cha kinyumbani ili kupata matokeo sahihi.

Kipimo cha mimba kutumia mafuta ya kula

Vipimo vingi vya kinyumbani humsaidia mwanamke kufanya kipimo chake kwa usiri wa nyumbani mwake. Pia, hakuna gharama inayo tumika kwani vitu vyote vinavyo tumika vipo nyumbani. Vipimo hivi havichukui muda mrefu kuonyesha matokeo yake.

Mahitaji ya kipimo cha mimba kutumia mafuta ya kula

kupima mimba kwa kutumia mafuta ya kula

  1. Kontena safi na wazi
  2. Kiasi kidogo cha mafuta ya kupikia/ kula
  3. Mkojo wa kwanza wa siku

Maagizo

  1. Chukua kontena yako safi, kisha uongeze mkojo
  2. Ongeza kiasi kidogo cha mafuta ya kula kwenye kontena hiyo
  3. Ikiwa yana kusanya na kuwa tone moja kubwa, una mimba
  4. Ikiwa mafuta hayo yana geuka na kuwa matone mengi madogo, hauna mimba

Unapofanya vipimo vya mkojo, mama anashauriwa kutumia mkojo wa kwanza wa siku kabla ya kuchukua kiamsha kinywa. Kwani mkojo huu huwa na viwango vya juu vya kichocheo cha HCG.

Chanzo: Healthline

Soma Pia: Kwa Nini Kupima Mimba Mapema Sana Hakushauriwi?

Written by

Risper Nyakio