Hatua 3 Rahisi Za Kupima Mimba Kwa Kutumia Sukari

Hatua 3 Rahisi Za Kupima Mimba Kwa Kutumia Sukari

Mbinu ya kupima mimba kwa kutumia sukari ni mojawapo ya njiia rahisi na ya haraka zaidi ya kudhibitisha ikiwa una mimba ama la.

Mtindo wa kupima mimba kwa kutumia sukari ndio ulio shika kasi siku hizi. Huenda ukawa umeskia kuuhusu kutoka kwa marafiki zako wakipita mahali. Lakini bado hauna uhakika jinsi ya kufanya kipimo hiki bila usaidizi.

Kilicho saidia kipimo hiki kutambulika na kuvuma kwa sana ni kupatikana kwa urahisi kwa vitu vinavyo hitajika. Na pia ni rahisi kufanya, kufanyika kwa mbio na kwa mtindo wa kisasa.

Hata mimba inaweza kupata usipo kuwa tayari. Kazi nyingi za nyumbani na ofisini huenda zikakosa kukupa mwanya tosha wa kukimbia hospitalini kufanya kipimo. Pia unataka kufanya kipimo hiki kwa mbio na kwa usiri wako. Kipimo hiki kitakuwa bora kwako.

Jinsi Ya Kupima Mimba Kwa Kutumia Sukari

Mbinu ya kupima mimba kwa kutumia sukari ni mojawapo ya njiia rahisi na ya haraka zaidi ya kudhibitisha ikiwa una mimba ama la.

Kipimo cha mimba kutumia sukari ni rahisi. Lakini kabla tuzame kwa mada hii, kipimo cha mimba cha sukari ni nini hasa?

Kipimo hiki ni cha kujifanyia kudhibitisha ikiwa una mimba ama la kwa kutumia sukari na mkojo. Kipimo hiki kina gundua kuwepo kwa homoni ya mimba maarufu kama human chorionic gonadotripin (HCG).

Je, human chorionic gonadotropin (HCG) ni nini?

HCG pia ina julikana kama homoni ya ukuaji, na ina gundulika siku 10 baada ya fertilization kufanyika. Ina onyesha iwapo una mimba ama la. Pia, HCG ina ujulisha mwili wako kuwa na viwango vya juu vya progesterone ili usiwe na kipindi chako cha hedhi na kusababisha kutoa fetusi mwilini.

Unafahamu ishara za mapema za mimba? Kichefu chefu, chuchu laini na uchovu? Ongezeko la homoni ya HCG ina zisababisha. Pia, inamlisha mtoto maziwa ya mama baada ya kuzaliwa.

Mahitaji ya kufanya kipimo cha mimba ukitumia sukari

 • Sukari nyeupe
 • Bakuli safi
 • Mkojo wa kwanza kabla kunywa chochote

Utaratibu wa kufuata kufanya kipimo hiki

Hakikisha kuwa unafanya kipimo hiki na mkojo wa kwanza, punde tu baada ya kuamka kabla ya kufanya kitu chochote. Una jukumu kubwa katika kipimo hiki. Hii ni kwa sababu mkojo wa kwanza wa siku huwa na kiwango kikubwa cha HCG.

 • Ongeza vijiko viwili ama vitatu vya sukari kwenye bakuli safi
 • Ongeza mkojo wako wa kwanza wa siku kwenye bakuli hilo iliyo na sukari
 • Ngoja angalau dakika tano kabla ya kujaribu kuangalia matokeo yake

Jinsi ya kusoma matokeo ya kipimo chako cha mimba

Baada ya kukojolea bakuli iliyo na sukari huenda ikasababisha mkusanyiko. Hii ina ashiria kuwepo kwa HCG kwenye sampuli yako ya mkojo, na kumaanisha kuwa una mimba. Lakini sukari iki yeyuka, hiyo ni ishara ya kukosekana kwa HCG. Ina maana kuwa hauna mimba.

Mambo yanayo weza kuathiri matokeo yako

 • Hatua zinafuatwa kwa umakini kwa sababu. Kukosa hatua moja kunaweza athiri matokeo yako
 • Hakikisha kuwa unakojoa kwenye bakuli safi. Kuepuka mkojo huo kuchafuka ukiweka kwa chombo tofauti kabla ya kuongeza kwenye bakuli iliyo na sukari
 • Kutumia mkojo wako wa pili ama wa tatu wa siku
 • Kunywa maji mengi kulazimisha mkojo kuja asubuhi huenda kuka athiri matokeo yako. Hii ni kwa sababu mkojo wako utakuwa na viwango vichache sana vya HCG na kuathiri matokeo yako
 • Kipimo kinapaswa kufanywa baada ya kuwa na uhakika kuwa umekosa kipindi chako cha hedhi. Pia, usifanye mapema sana baada ya kukosa kipindi chako. Angalau siku kumi

Je, matokeo ya kipimo cha mimba kutumia sukari ni sahihi?

Ujauzito ni kipindi kinacho badilisha maisha ya mwanamke. Ina eleweka kuwa una hamu ya kujua hali yako ya mimba, lakini kuendea kipimo kinacho dhihirika zaidi kuna shauriwa.

Hakuna utafiti wa kisayansi unao dhihirisha ikiwa kipimo cha mimba na sukari ni sahihi na cha kuaminika. Lakini unaweza fanya kipimo hiki ukingoja kuenda hospitalini kupima.

Chanzo: Healthline

Soma Pia: Ishara 5 Kuwa Unapaswa Kufanya Kipimo Cha Mimba

 

Written by

Risper Nyakio