Jinsi Ya Kupima Mimba Na Chumvi

Jinsi Ya Kupima Mimba Na Chumvi

Ushawahi penda kujua kwa mbio iwapo una mimba ama la? Ndio, unaweza, kwa kujua jinsi ya kupima mimba na chumvi! Hii ni iwapo hauna wakati wa kukimbia kwenye zahanati kupata vifaa vya kupima ujauzito ama iwapo daktari wako ako mbali sana.

Kwa nini ujishughulishe na kipimo cha mimba cha nyumbani?

Ni sawa, huenda ukawa unashangaa kwa nini usiendee vipimo vilivyo jaribiwa na kudhibitishwa na kuaminika vya kupima ujauzito. Kupima mimba ukiwa nyumbani kutakupatia matokea unayo hitaji kwa siri na ukiwa nyumbani. Mchakato huu wote huenda ukawa na uwoga mwingi haijalishi iwapo ungependa kupata mtoto ama la.

Kipimo cha mimba cha nyumbani kinapaswa kutosheleza maswali yako mbio na wakati huo huo kukupa jibu ukiwa katika mazingira uliyo yazoea – nyumbani mwako.

Mambo unayo paswa kufanya kabla ya kupima iwapo una mimba na chumvi

Ili kupata matokeo, unapaswa kungoja hadi mwili wako uanze kutoa viwango tosha vya homoni ya HCG. Hii itatendeka wiki ya kwanza baada ya kukosa kushuhudia kipindi chako cha hedhi. Kitu chochote kabla ya wiki moja huenda ukapata matokeo yasiyo ya kweli.

Matokeo sawa yata lingana kwa sana na wingi wa kukoleza kwa mkojo, iliyo na maana kuwa haupaswi kunywa maji mengi kabla ya kufanya kipimo hiki. Maji mengi huenda yakafanya mkojo wako kukosa kukoleza kunakohitajika. Hili ni jambo muhimu la kujua iwapo ungetaka kujua jinsi ya kupima mimba na chumvi.

Jinsi Ya Kupima Mimba Na Chumvi

Kipimo hiki kinafanya kazi vipi?

Ni kawaida kushangaa jinsi kipimo hiki kinafanya kazi iwapo hii ni mara yako ya kwanza kujua jinsi ya kupima mimba na chumvi. Huenda ukakosa kuamini kwa mara ya kwanza na hili ni sawa pia. Ukweli ni kuwa chumvi – kiungo ambacho kila mtu ako nachi nyumbani – kinaweza fanya kazi kama kipimo cha mimba lakini huenda kika sikika kama kitu ambaho sio cha kuaminika. Homoni ya HCG itakuwa na mabadiliko inapo patana na chumvi, na itakujulisha iwapo una mimba ama la.

Vitu unavyo hitaji kwa kipimo cha mimba na chumvi

Habari njema ni kuwa hauhitajiki kukimbia nje kununua kitu chochote cha kipimo hiki. Unapo soma jinsi ya kupima mimba na chumvi, unapaswa kuja na ufahamu kuwa kila kitu unacho hitaji kimo jikoni mwako.

Utahitaji:

• Saa ya kupima muda wa kipimo chako (simu yako itafanya kazi nzuri)!
• Mkojo wako wa kwanza (hasa wa asubuhi)
•  Kontene nyeupe isiyo na rangi ama kikombe
• Kiwango kidogo cha chumvi

kupima mimba na chumvi

Ongeza kiasi kidogo cha chumvi, unaweza pata kipimo chako cha mimba ukiwa nyumbani

Jinsi ya kupima mimba na chumvi – utaratibu/ maagizo

1.  Kojoa kwenye chombo cheupe ama kikombe (kumbuka kuwa mkojo freshi wa asubuhi ni bora zaidi)
2. Ongeza chumvi kidogo kwenye sampuli ya mkojo
3. Koroga ama uchanganye mkojo ule na chumvi vizuri
4. Pima muda wa dakika 5 kwa kutumia saa yako
5. Ngoja kuona mabadiliko

kupima mimba na chumvi

(picha shukrani kwa: Pixabay)

Kwa hivyo una mimba ama la?

Ukigundua povu ya rangi nyeupe kana kwamba maziwa, hiyo ni ishara kuwa una mimba. Ila, iwapo mkojo unabaki ulivyokuwa bila povu, bila shaka hauna mimba.

Kipi chafuata?

Kujua jinsi ya kupima mimba na chumvi ni njia ya mbio na isiyo ghali ya kujua iwapo una mimba. Walakini, huenda bado ukahitajika kupata vipimo vya damu kutoka hospitalini ili kuwa na uhakika. Vipimo vya nyumbani huenda vikawa sawa ila havina uhakika kabisa na havija dhibitika kisayansi. Ni jambo la busara kupata vifaa vya kupima mimba ama kumtembelea daktari kudhibitisha zaidi iwapo una mimba ama la.

Kumbukumbu: NHS

Soma pia: Things to add to your pregnancy shopping list

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio