Jinsi Ya Kupima Mimba Nyumbani Ukitumia Chumvi Bila Gharama Yoyote

Jinsi Ya Kupima Mimba Nyumbani Ukitumia Chumvi Bila Gharama Yoyote

Kuna njia tofauti ambazo mwana dada anazoweza kutumia kupima mimba. Miongoni mwa njia hizi ni kutumia chumvi. Anafanya hivi akiwa nyumbani bila kwenda hospitalini ama kutumia pesa zozote.

Ushawahi tamani kujua kwa urahisi ama una mimba ama la? Henda ikawa huna wakati wa kutosha wa kwenda kwa duka la dawa kununua vipimo vya mimba na daktari wako ako mbali sana nawe. Katika kesi hii, unaweza tamani kujua kwa haraka ama una mimba au la. Ndio, kuna uwezekano wa kupima mimba ukitumia chumvi na kujua hali yako!

Mbona ujishughulishe na kipimo cha kinyumbani?

Sawa, najua unashangaa mbona usitumie njia iliyo dhibitishwa kujua iwapo una mimba. Kupima mimba ukiwa nyumbani inakusaidia kuliweka jibu siri. Mchakato huu wote unaweza kuwa wa kuhangaisha ikiwa Unatamani kupata mtoto ama la.

Kipimo cha nyumbani kitasaidia kudhihirisha udadisi wako kwa mbio na kupata majibu ya kipimo ukiwa kwa mazingara ambayo umeyazoea- nyumbani mwako.

how to test pregnancy with salt

Vitu vya kufanya kabla ya kupima mimba ukitumia chumvi

Ili kupata matokeo kamili, unahitajika kungoja hadi wakati ambapo mwili wako una toa idadi ya kutosha ya homoni ya HCG. Hii itatendeka wiki moja baada ya kukosa majira yako ya hedhi. Kujipima kabla ya wiki moja hautapata matokeo kamili. Matokeo kamili pia itategemea na wingi wa mkojo wako, hii inamaanisha haupaswi kunywa maji mengi kabla ya kujipima. Maji mengi yatafanya mkojo wako kuwa mwepesi na itakuwa ngumu kupata matokeo kamili. Hili ni jambo la muhimu kujua iwapo unataka kupima mimba kutumia chumvi.

Je kipimo hiki kina fanya kazi aje?

Ni kawaida kushangaa namna kipimo hiki kinavyo fanya kazi kama huu ni wakati wako wa kwanza kujua kuhusu kipimo hiki cha chumvi. Unaweza kosa kuamini mwanzoni, lakini hilo ni sawa pia. Ukweli ni kuwa chumvi, kiungo ambacho kila mtu ako nacho nyumbani mwake- inaweza kuwa kipimo bora cha uja uzito halikai jambo la kuaminika. Homoni ya HCG itakuwa na tokeo baada ya kuwekwa kwa chumvi na hili litakusaidia kujua iwapo una mimba ama la.

Vitu unavyo hitaji vya kipimo cha nyumbani cha chumvi

Habari njema ni kuwa hakuna haja, kukimbia nje ya nyumba kununua chochote kile. Unapo soma jinsi ya kupima mimba ukitumia chumvi, Unafaa kuja ukijua kuwa vyovyote vile unavyo hitaji, viko jikoni mwako.

Utakavyo hitaji:

 • Saa ya kujua muda wa kipimo kile (simu yako itafanya kazi njema)
 • Mkojo wako wa kwanza (haswa wa asubuhi)
  • kikombe chepesi ama chupa
  • Pinchi mbili za chumvi

Jinsi ya kupima mimba na chumvi- maelekezo

 1. kojolea kichupa kikombe chako ama (kumbuka kutumia mkojo wa asubuhi kwani huwa na matokeo bora zaidi)
 2.  Ongeza pinchi mbili za chumvi kwenye mkojo ule.
 3. Changanya vitu hivi viwili vizuri.
 4. Eka saa yako ilie baada ya dakika 5 na ungoje wakati huu.
 5. Yatazame mabadiliko.

 

Je una mimba ama la?

Ukiona vitu vilivyoko kwa chupa lako limeanza kuwa rangi ya maziwa, hiyo ni ishara kuwa una mimba. Kama mkojo ule unabaki bila kutoa sauti yeyote ama kubadili rangi, ni dhibiti kuwa hauna mimba.

Je, nini baada ya hili?

Kujua jinsi ya kupima mimba kutumia chumvi ni njia rahisi na isiyo ghali ya kujua kama una mimba ama la. Ijapokuwa, bado unaweza hitajika kupata kipimo cha damu hospitalini ili kuhakikisha. Vipimo vya nyumbani vinaweza kuwa bora, ila si njia iliyo dhibitishwa ya kisayansi. Ni vyema kupata kit ya kipimo cha mimba ama umtembelee daktari wako ili kupata dhibitisho kweli.

Read Also: How to test pregnancy with sugar in 3 simple steps.

 

Written by

Risper Nyakio