Jinsi Ya Kupima Mimba Ya Wiki Moja Bila Kutumia Vifaa Vyovyote

Jinsi Ya Kupima Mimba Ya Wiki Moja Bila Kutumia Vifaa Vyovyote

Iwapo ni vigumu kuthibitisha iwapo una mimba katika wiki ya kwanza kuna njia za kupima mimba ya wiki moja.

Unapokuwa na mimba ya wiki moja, huenda ikawa kuwa hauna mimba kwani vipimo vyote havioneshi kuwepo kwa mimba. Tuna taka kuangazia jinsi ya kupima mimba ya wiki moja.

Mimba wiki moja inaonekana vipi

Hakuna ishara dhibiti katika wiki hii za kujua iwapo una mimba ama la kwani huenda ukawa umekosa hedhi yako tu. Mwili wako unajitayarisha kuwa na mimba. Ishara maarufu ni kamakupima mimba ya wiki moja

 • Kuhisi kufura kwa tumbo
 • Kuwa na upele kwenye uso
 • Mhemko wa hisia
 • Kubadilika kwa mwendo wa tumbo, kukosa maji mwilini na kuharisha
 • Mabadiliko ya hisia za kufanya mapenzi
 • Kuwa na fikira nyingi
 • Uchovu
 • Mtamanio wa chakula
 • Kuumwa na chakula
 • Kuto kuwa na hamu ya vileo
 • Uchungu kwenye misuli
 • Kuumwa na tumbo
 • Chuchu laini
 • Kuongezeka kwa uzito

Jinsi mwili wako unavyo jitayarisha kubeba mimba: kupima mimba ya wiki moja

Iwapo ungependa kuwa na mimba, ni vyema kuhakikisha kuwa unaanza kula vitamini za wakati kabla ya mimba. Vitamini hizi ni muhimu katika kuhakikisha kuwa mtoto wako hatakuwa na matatizo anapo zaliwa.

Kunywa maji nyingi

Katika wiki ya kwanza, ni wazo la busara kuanza mitindo ya afya itakayo hakikisha kuwa una safari njema ya mimba. Huenda ikawa ni vigumu kuwachana na pombe iwapo ulikuwa na uraibu huu. Ila, ni vyema kwa kila mama anaye tarajia ama ambaye angependa kuwa na mimba kutupilia uraibu huu mbali.

Ni vyema pia kutupilia mbali vitu vilivyo chakatwa na vyakula vyenye sukari nyingi. Sio jambo rahisi ila lazima lifanywe.

kupima mimba ya wiki moja

Kula vyakula vyenye afya

Unapokuwa na mimba, ni vyema kula vyakula vyenye afya kwani saa hii una kiumbe kingine ndani ya tumbo yako na ni vyema kuhakikisha kuwa mtoto wako ana shiba. Kula vyema ni muhimu ili mtoto wako awe na afya bora. Hakikisha kuwa unakula vyakula vyenye afya, freshi na lazima bakuli yako iwe na mboga nyingi na matunda na pia nafaka.

Katika wiki ya kwanza huenda ukaanza kuwa na hamu ya kula vyakula fulani. Ili kuepuka kula viwango vingi vya chakula, hakikisha kuwa unatembea mara kwa mara.

Kufanya mazoezi mara kwa mara

Huenda kufanya mazoezi kukawa sio jambo unalo tamani kufanya hasa unapokuwa na vipindi vyako vya hedhi. Ila utafiti unadhibitisha kuwa huenda uchungu wako wa hedhi ukapunguka unapo fanya mazoezi. Mazoezi yatasaidia kuhakikisha kuwa wewe na mtoto wako mko salama. Ila, ni vyema kuhakikisha kuwa haufanyi mazoezi magumu.

Hakuna vipimo dhabiti ambazo zinaweza kuonyesha iwapo una mimba katika wiki moja. Usikize mwili wako na uwe makini kuona tofauti zozote.

Written by

Risper Nyakio