Vidokezo Muhimu Vya Kupona Baada Ya Upasuaji Wa C-section

Vidokezo Muhimu Vya Kupona Baada Ya Upasuaji Wa C-section

Itachukua muda kupona. Uponaji wa c-section huchukua muda. Kwa hivyo kuwa mkarimu kwako. Chukua muda upone na uelewe hali yako mpya.

Uponaji wa c-section sio jambo ambalo huenda ukawa umejatayarishia. Mara nyingi, hauwezi tabiri jambo hili kukufanyikia. Una hisi uchungu na kujua jinsi ya kuishi katika hatua hii. Makala haya yana kuelimisha jinsi unavyo paswa kufanya ili kuongeza kasi ya kupona kwako baada ya c-section. Soma zaidi!

vidokezo vya kupona baada ya C-section

  1. Lishe

 

faida za scent leaf unapokuwa na mimba

Daktari Tan ana shauri kula protini nzuri na ufuta mzuri ili kupona vyema. Ana endelea kuongeza kuwa zinc na vitamini C ni virutubisho vinavyo saidia na kupona kwa tishu.

Baadhi ya madaktari wana shauri vitamini E kusaidia na mchakato wa kupona baada ya upasuaji wa C-section. Haijalishi tembe za virutubisho ulivyo shauriwa uchukue, tafadhali hakikisa umezichukua! Ni vyema pia kujitenga na vyakula vya baharini katika kipindi hiki.

2. Tunza kidonda chako

Vidokezo Muhimu Vya Kupona Baada Ya Upasuaji Wa C-section

Unapo kuwa hospitalini, wauguzi watasafisha kidonda chako wakitumia bidhaa za antiseptic kila siku. Utatumwa nyumbani na vitu ambavyo vitaweka kidonda chako kikiwa kimekauka. Mara nyingi, kuna plaster spesheli inayo epusha maji kuto gusa kidonda chako. Haupaswi kugusisha sabuni kwenye kidonda chako katika hatua hii.

Mahali kati ya siku saba na kumi baada ya upasuaji wako, uzi zako zitatolewa. Daktari wako atashauri krimu ya collagen na zingine za kuepusha keloids kuwa kwenye kidonda. Pia kufanya hivi kunasaidia na uponaji wa upande wa nje wa kidonda hiki.

Baada ya kutoa uzi, unaweza koga na kukubalisha maji na sabuni kupita kwenye kidonda. Walakini, tahadhari usi jisugue kidonda hicho. Katika hatua za kwanza za uponaji wa kidonda chako cha c-section, ni vyema kuto tumia maji moto sana kwenye kidonda chako.

3. Kutumia binda ya upasuaji

Siku baada ya upasuaji wako, daktari wako anaweza kuuliza uweke surgical binder. Ina manufaa mengi katika uponaji wa kidonda chako cha c-section. Kwanza, ina egemeza na kuepusha mwendo mwingi. Unapo hitaji kukohoa, inasaidia sana.

Ina kusaidia kukumbuka kuwa kidonda hicho hakita pasuka ama kufunguka. Pia, inasaidia kukaza ngozi iliyo legea na kuepusha tumbo iliyo legea kuumiza kidonda chako. Shinikizo kutoka kwa binder hiyo inapunguza kuwa na alama ya kidonda hicho.

Hitimisho

Haya ndiyo maneno ya daktari Tan kwa mama wanao pona kutokana na c-section.

"Kuwa mvumilivu. Mtoto alichukua miezi tisa kukua ndani yako. Abs zako zime nyooshwa kiasili. Wakati ambapo c-section huenda ikaonekana kana kwamba mtoto wako alitoka kwa mkoba, sio dhamana kuwa misuli yako ya tumbo itarudi tena. Haifanyi kazi hivyo.

Itachukua muda kupona. Uponaji wa c-section huchukua muda. Kwa hivyo kuwa mkarimu kwako. Chukua muda upone na uelewe hali yako mpya.

Soma PiaYote Unayopaswa Kujua Kuhusu Kupata Nafuu Baada Ya Upasuaji Wa C-section

Written by

Risper Nyakio