Vidokezo 3 Muhimu Kwa Mama Anaye Pona Baada Ya Upasuaji Wa C-section

Vidokezo 3 Muhimu Kwa Mama Anaye Pona Baada Ya Upasuaji Wa C-section

Baada ya upasuaji wa c-section, jitenge na mambo yatakayo shinikiza kidonda chako kama vile kucheka, kuchemua ama kuinama sana.

Kipindi baada ya kujifungua na huwa chenye furaha kwa kila mama. Baada ya miezi tisa iliyo jawa na hisia tofauti, za furaha, mhemko wa hisia, kusoma mambo mapya kila uchao na hata kupona baada ya upasuaji wa c-section. Na baada ya masaa machache ama mengi kwenye chumba cha uzazi, mama anapo mshika mwanawe, maumivu yote aliyo yapitia husombwa na hisia za furaha baada ya kumpakata mwanawe.

Haijalishi mama alivyo jifungua, kupitia kwa njia ya kawaida ama upasuaji, bora ana jifungua kwa njia salama na kuweza kwenda nyumbani na mtoto wake mikononi mwake. Ikiwa mama amejifungua kupitia kwa njia ya upasuaji, kuna mambo ambayo anapaswa kuzingatia ili kukisaidia kidonda chake kupona kwa kasi.

Vidokezo 3 Vya Jinsi Ya Kupona Baada Ya Upasuaji

kupona baada ya upasuaji

  1. Pumzika vya kutosha

Upasuaji wa c-section ni upasuaji mkubwa. Mama anapaswa kujilinda zaidi kwani kidonda hiki huwa na uchungu mwingi. Baada ya mama kufanyiwa upasuaji, anapaswa kujitenga na kufanya kazi za nyumba. Mchumba wako anaweza kusaidia ama utafuta mtu atakaye kusaidia kufanya kazi nyumbani mwako hadi pale utakapo pona.  Ili wakati anao pata uwe wake na wa mwanawe. Lala mtoto anapo lala kwani nafasi kubwa ni itakuwa vigumu kulala anapo amka.

2. Kula vyema

Lishe ni muhimu kwa mama baada ya kujifungua. Kwani anacho kula ndicho kinacho mlisha mtoto wake. Lishe bora yenye afya inausaidia mwili wa mama kupona kwa kasi. Matunda na mboga za kijani zinapaswa kuongezewa kwenye sahani ya mama kila anapokula. Kwa vitafunio, chagua vyenye afya kama vile kula tufaha badala ya vibanzi.

3. Usi shinikize kidonda

kupona baada ya upasuaji

Jitenge na mambo yatakayo shinikiza kidonda chako kama vile kucheka, kuchemua ama kuinama sana. Ilhali kuna mambo ambayo ni magumu kujidhibiti, unapo cheka ama kuchemua, uekelee mto kwenye kidonda chako ili kupunguza uchungu kwenye sehemu hiyo. Usipo ishinikiza sehemu hii, itakuwa rahisi kupona na itapona kwa kasi.

Unapo toka hospitalini, epuka kupanda na kushuka ngazi, hamia chumba kilicho karibu kufikia kwa urahisi. Jitenge na kufanya mazoezi hadi utakapo pona ama baada ya daktari wako kukushauri kuwa ni salama kurudia mazoezi.

Wasiliana na daktari wako bila site unapo gundua kuwa una uvimbe kwenye kidonda, kuvunja damu kwenye sehemu hiyo ama kuhisi maumivu kwenye chuchu zako.

Mama, huu ni wakati wako kujitunza zaidi, kwa afya yako na ya mwanao. Na zaidi, kuwa na kikundi cha marafiki walio pitia upasuaji wa c-section upate maarifa kutoka kwao. Watakupa motisha na kukusaidia katika kipindi hiki unapo zidi kupona!

Soma Pia:Usifanye Vitu Hivi Baada Ya Kufanyiwa Upasuaji Wa C-section!

Written by

Risper Nyakio