Ishara Za Kupoteza Mimba Ya Wiki Mbili

Ishara Za Kupoteza Mimba Ya Wiki Mbili

Ini ameshuhudia kuharibika kwa mimba mara sita. Kati ya mara hizi sita, angalau nne zilifanyika mapema sana, hata kabla atambue kuwa ana mimba. Hakukuwa na ishara mapema hivyo kwenye ujauzito; ama hakugundua. Ila, ishara za kupoteza mimba ya wiki mbili ni kama zipi?

Mara nyingi, kuharibika kwa mimba hufanyika trimesta ya kwanza kati ya wiki 1-12. Angalau asilimia moja ya mimba huharibika baada ya wiki 20. Aina hii ina julikana kama stillbirth.

"Kwa wanawake wengi, kuharibika kwa mimba mapema huwa kama ndoto mbaya. Huchukua muda kabla ya kukubali matokeo," alisema Prisca Obi mkurugenzi mkuu, Obstetrician katika hospitali ya mafunzo ya Chuo Kikuu cha Uyo. "Nafikiria ni kwa sababu wanawake hawaelewi mabadiliko yote yanayo fanyika kutoka wakati wanapo tunga mimba. Iwapo moja ya hatua zote zinazo fanyika baada ya kutunga huenda mrama, mama hupoteza mimba."

Ishara maarufu za kupoteza mimba ya wiki mbili

2 weeks miscarriage

Tofauti na imani nyingi, kufika kilele wakati wa ngono, kufanya mazoezi ama fikira nyingi za kazini hazi sababishi kupoteza mimba kwa mapema.

"Wanawake wanapo kuwa kwa kipindi cha maombelezi ya mtoto wao kwa muda mrefu, nawakumbusha kuwa kuharibika kwa mimba ni njia ya mwili ya kutoa fetusi ambayo haijakuwa ikikua ipasavyo," alisema Prisca Obi. Bila shaka mi huwaeleza sababu ambazo huenda zika sababisha kuharibika kwa mimba. Na muhimu zaidi kuwafanya waelewe kuwa sio lawama yao.

Ishara tano maarufu za kuharibika kwa mimba

miscarriage symptoms

1. Kuumwa na tumbo

Wakati ambapo baadhi ya wanawake hushuhudia kuumwa na tumbo sana, wengine hawatambui hata. Hii ni ishara moja ambayo kila mwanamke mwenye mimba hapaswi kupuuza. Ona daktari wako ukihisi maumivu ya tumbo mapema katika safari yako ya mimba. Huenda ikawa ishara mbaya.

2. Kichefu chefu ama kutapika

Mara nyingi huenda ukafikiria ni ugonjwa wa asubuhi, kuhisi kutapika baadhi ya wakati ni mojawapo ya ishara za mapema za kupoteza mimba ya wiki mbili zinazo puuzwa baada ya kutunga. Wakati ambapo ni salama kuwa na fikira chanya kuhusu mimba yako, ni muhimu kujua kuwa kutapika huenda pia kukawa ishara ya kupoteza mimba.

3. Kamasi nyembamba ya pinki

Iwapo pap smear inatoka na kamasi ya pinki, madaktari watafanya uchunguzi zaidi kuona iwapo una dalili zingine za kuharibika kwa mimba ya wiki mbili baada ya kutunga.

4. Kutoa damu inayofanana na tishu

Hii ni mojawapo ya ishara maarufu zaidi za kupoteza mimba mapema. Wanawake mara nyingi huona uchafu kutoka kwa uke wao unaotoshana na tishu. Hii bila shaka ni ishara kuwa mwili wako unatoa fetusi. Ukishuhudia ishara hii, tafadhali wasiliana na daktari wako.

5. Dalili zote za mimba hupotea baada ya wiki mbili

Baadhi ya wakati, ugonjwa wa asubuhi na kuumwa na chuchu ni ishara nzuri. Zina dhihirisha kuwa mimba yako ina afya. Wakati ambapo ishara hizi za mimba zinapotea, huenda ikawa ni ishara ya kuharibika kwa mimba kwa mapema.

6. Kuumwa sana ama kidogo na mgongo ama mimba

Ishara za mapema za kupoteza mimba huiga ishara za uchungu wa uzazi. Hii ni kwa sababu una shuhudia uchungu wa uzazi mdogo. Tofauti ni kuwa haujabeba mimba hadi ikakomaa ama mtoto wako hajafikisha wiki 20.

Kuumwa na tumbo na mgongo katika wiki za kwanza 12 za mimba huenda kukawa ishara mbaya. Mtembelee daktari wako ukishuhudia mojawapo ya ishara tulizo taja.

Vidokezo vya kuepuka kupoteza mimba

how to prevent miscarriages

Wataalum wa afya wanaamini kuwa kuharibika kwingi kwa mimba hakuwezi epukika. Walakini, kunasaidia kujua sababu zinazo sababisha hatari kuongezeka.

Hapa kuna baadhi ya njia zinazo aminika kusaidia kuepuka kuharibika kwa mapema kwa mimba:

• Epuka matibabu yaliyo na uwezo wa kufanya upoteze mimba. Soma maagizo yaliyoko ndani ya kontena ya kila dawa. Wasiliana na daktari wako kabla ya kukunywa dawa zozote. Dawa nyingi za malaria na typhoid husababisha kuharibika kwa mimba.

• Kuwa na uzito sawa wa mwili

• Tayarisha mwili wako kutunga kwa kuchukua vitamini na madini ya mimba. Mifano ya hizi ni kama vile vitamini B, folic acid na Vitamini C.

• Epuka maambukizi yanayo pitishwa kupitia ngono. Iwapo una maambukizi haya, chukua hatua kuyatibu kabla ya kujifungua.

Kumbukumbu: NHS

Soma pia: Miscarriages myths and facts: Is it easier to get pregnant after a miscarriage?

Written by

Risper Nyakio