Kupoteza Uwezo Wako Wa Kunusa Ni Ishara Ya Homa Ya Korona Kulingana Na Madaktari

Kupoteza Uwezo Wako Wa Kunusa Ni Ishara Ya Homa Ya Korona Kulingana Na Madaktari

Huku madaktari waki angalia kupoteza uwezo wako wa kunusa kama mojawapo ya ishara kuu za virusi vya homa ya korona. Watu wazima wanao ishuhudia hujifariji kwa kujua kuwa hawapotezi uwezo muhimu ama utimamu wao. Hivi majuzi, madaktari wanao ongoza ENT huko Britain wali sema kuwa, kupoteza uwezo wa kunusa ni ishara ya virusi vya korona hata kwa wagonjwa wasio dhihirisha ishara zingine. Wakati ambapo ishara kuu bado ni joto jingi, kikohozi, kutatizika kupumua na kupoteza uwezo wa kunusa ndiyo ishara ya hivi majuzi. Makala haya yana angazia zaidi kuhusu kupoteza uwezo wa kunusa na homa ya korona.

Kwa Nini Madaktari Wanadhani Kupoteza Uwezo Wa Kunusa Kuna Husiana Na Homa Ya Korona

kupoteza uwezo wa kunusa na homa ya korona

Katika kauli yao ya hivi majuzi, wataalum wa ENT UK, wana waonya watu kuwa kuna utafiti ulioko kuwa kupoteza uwezo wako wa kunusa huenda ikawa ishara ya COVID-19. Na hii ni kweli ikiwa mtu anaonyesha ishara zingine ama la. Waandishi wa kauli hii, Clare Hopkins, kiongozi wa British Rhinological Society; na Nirmal Kimar, rais wa British Association of Otorhinolaryngology, wame endelea na kuwashauri watu walio poteza uwezo wao wa kunusa kuji karantini kwa siku saba.

"Nafikiria wagonjwa hawa ni miongoni mwa wanao beba virusi hivi walio changia katika kusambaa kwa kasi kwa virusi vya homa ya korona," madaktari waliandika. "Kwa bahati mbaya, wagonjwa hawa hawafuzu kwenye vigezo vya kupimwa ama kuji karantini."

Kulingana na waandishi hawa, visa vya ishara hii vinaongezeka kwa kasi sana. Asilimia 30 ya kesi zilizo dhibitishwa South Korea zilikuwa na ishara hii. Katika kesi ambapo virusi vya korona ni vyepesi, ishara hii ilishuhudiwa pamoja na ishara zingine chache.

Madaktari walizidi kusema kuwa ishara hii ina jadiliwa kwa sana na madaktari wa upasuaji kutoka pande mbali mbali.

Kwa sababu watu hawana ishara zingine, bila ufahamu wao, wanazidi kusambaza virusi hivi. Wakati ambapo sote tunapaswa kuzingatia umbali kati ya watu, madaktari wanasema kuwa, ni muhimu kwa yeyote ambaye kwa ghafla anashindwa kunusa ama kuonja, kubaki nyumbani.

Je, kupoteza uwezo wa kunusa kwa ujumla ni ishara ya magonjwa ya virusi?

ncdc ban gatherings covid-19

Kulingana na daktari Alfred Iloreta, asilimia 40 ya watu wazima wanao poteza uwezo wao wa kunusa wana aina ya virusi vya mfumo wa kupumua.

Hata kama wataalum bado hawaja dhibitisha kwa uhakika kinacho sababisha wagonjwa wa COVID-19 kupoteza uwezo wao wa kunusa na kuonja; baadhi ya virusi huathiri neva za uwezo mwilini, alisema daktari Donald Wilson.

Mambo ya kufanya unapo shuhudia haya

Wagonjwa wanao poteza uwezo wao wa kunusa na kuonja wanapaswa kurejesha uwezo huu ikiwa unahusika na COVID-19 ama ugonjwa wowote ule. Lakini jambo la kuweka akilini hata kukiwa na shaka za COVID-19 ni kuwa: Kwa kasi ukipoteza uwezo wako wa kunusa kahawa yako asubuhi, wasiliana na daktari wako kwa kasi, na uanze kujitenga na watu. Kisha uwe makini kuona iwapo utashuhudia ishara zingine za homa ya korona.

Chanzo: Health Washington Post

Written by

Risper Nyakio