Kwa Nini Napoteza Uzito Nikiwa Na Mimba?

Kwa Nini Napoteza Uzito Nikiwa Na Mimba?

Kupoteza uzito ukiwa na mimba ni jambo kawaida hasa katika trimesta yako ya kwanza ya ujauzito. Kipi kinacho sababisha.

Ikiwa historia yako ya kutafuta ujumbe kwenye mtandao imejazwa na 'kupoteza uzito nikiwa na mimba',  huenda ukawa na ama ukakosa hali sugu inayo paswa kuangaliwa kwa kina.

Kama ilivyo kawaida, ujauzito huja na ongezeko la uzito. Ongezeko katika kazi za homoni mwili kunaweza ongeza hamu ya mama ya kula. Pia kuna kula chakula cha watu wawili katika ujauzito. Wanawake wajawazito mara nyingi huongeza uzito, na ni kawaida, kwani kuna kiumbe kinacho kua tumboni mwao.

Ikiwa una tatizika kuongeza uzito ukiwa na mimba, hapa kuna njia ambazo unaweza tatua tatizo hilo.

Kupoteza Uzito Nikiwa Na Mimba: Kinacho Sababisha

weight loss

Ikiwa sio lengo lako kupoteza uzito, huenda kukawa na sababu fiche zinazo fanya upoteze uzito.

  1. Ugonjwa wa asubuhi

Kuhisi kichefu chefu na kutapika ni kawaida katika trimesta ya kwanza. Utafiti umedhibitisha kuwa asilimia 90 ya wanawake huugua ugonjwa wa asubuhi wakiwa na mimba. Wanawake wengi hushindwa kubaki na chakula katika kipindi hiki. Kichefu chefu hushuhudia sana wakati wa asubuhi, na kupatiwa jina ugonjwa wa asubuhi. Kutapika baadhi ya wakati huja na kupoteza hamu ya kula na kufanya iwe vigumu kwa mwili kupata virutubisho vinavyo hitajika.

2. Hyperemesis gravidarum

Hii ni hali sugu. Hata kama kutapika ni kawaida  ukiwa na mimba, HG ni hali ya dharura na nyingi kuliko ugonjwa wa asubuhi. Wanao kuwa na tatizo hili huenda waka lazwa hospitalini kufuatia kukosa maji tosha mwilini. HG huisha baada ya trimesta ya kwanza lakini kuna wanawake wachache ambao wanateseka na hali hii kipindi chote cha ujauzito.

3. Mazoezi na kubadilisha mtindo wa maisha

Kwa wanawake wengi, kipimo chanya cha ujauzito humaanisha mabadiliko katika mitindo yao ya maisha. Huu ndiyo wakati bora wa kula lishe zenye afya na kuhusisha mazoezi mepesi kwenye ratiba yao ya kila siku. Ikiwa una shaka ama kushangaa kwa nini unapoteza uzito ukiwa na mimba, unapaswa kufahamu kuwa huenda ikawa ni kufuatia kuishi maisha yenye afya.

4. Wakati mwingine, huwa kawaida kupoteza uzito katika trimesta ya kwanza

kupoteza mimba ya wiki mbili

Hakuna haja ya kuwa na shaka unapo pima uzito wako na kugundua kuwa umepunguza uzito. Hii ni kawaida sana hasa kwa wanawake walio na uzito zaidi wa mwili. Watakao gundua kuwa miili yao inatumia nishati nyingi kutengeneza nafasi ya mtoto anaye kua. Ikiwa kupoteza uzito haku andamani na matatizo ya kiafya, nafasi kubwa ni kuwa hauna kitu cha kuwa na wasi wasi. Walakini, unapaswa kuripoti kwa daktari wako ikiwa unaanza kupoteza uzito baadaye kwenye ujauzito wako.

Mambo yakufanya ikiwa unapoteza uzito katika ujauzito

  1. Kunywa maji

Kunywa maji angalau glasi nane kila siku kuna faida nyingi kwa afya yako. Ratibisha kunywa maji wakati ambapo hauhisi kutapika sana.

2. Kula wakati wowote unao weza

Baadhi ya wakati, ugonjwa wa asubuhi huwa mbaya sana hautaweza kufikiria kuhusu kula. Lakini unapaswa kuhakikisha kuwa unakula wakati ambapo tumbo yako inatulia kwa sababu wewe na mtoto wako mnahitaji virutubisho.

3. Lala vyema

Lala na upate usingizi mwingi uwezavyo. Kulala kunaweza punguza fikira nyingi na kuupa mwili wao mapumziko unayo hitaji.

Ikiwa unashangaa kwa nini unazidi kupoteza uzito ukiwa na mimba, ni vyema kukumbuka kuwa hauko peke yako. Na wanawake wengine hupitia jambo hili. Ni kawaida kuliko unavyo dhani. Ili kusuluhisha tatizo hili, ni vyema kufahamu chanzo cha kupoteza uzito ili upate suluhu bora kwa kesi yako.

Chanzo: NHS

Soma Pia:Vidokezo 5 Muhimu Kwa Wanawake Wanao Jaribu Kupata Mimba

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio