Kichefu chefu ni mojawapo ya ishara za mapema za kuashiria kuwa mama ana mimba. Mbali na mama mjamzito, kuna baadhi ya watu wanao sumbuliwa na hali hii wanapo safiri. Na kuwa lazimisha wakati wote kuchukua dawa za kukabiliana na hisia hii kabla ya kusafiri. Tatizo ni kuwa dawa hizi mara nyingi huwa na athari hasi kama vile kuhisi kulala ama mwepesi kichwani. Kuna njia dhabiti za kupunguza kichefu chefu bila kutumia dawa.
Tazama orodha yetu ya matibabu ya kinyumbani ya kupunguza kichefu chefu kwa kutumia bidhaa za nyumbani.
- Kula Tangawizi

Tangawizi inafahamika sana kama dawa ya kutibu kichefu chefu. Wataalum wana amini kuwa kiungo hiki kina vitu vinavyo fanya kazi sawa na dawa dhidi ya kichefu chefu. Kwa hivyo, ikiwa una tatizika na kichefu chefu katika ujauzito, hakikisha kuwa unakula tangawizi mara kwa mara. Kwa wanao hisi kichefu chefu baada ya matibabu ya saratani (chemotherapy), kiungo hiki kitakusaidia kukabiliana na hali hiyo.
Kwa wanao kuwa na shinikizo la chini la damu ama sukari ndogo kwenye damu, una shauriwa kudhibiti ulaji wa tangawizi.
2. Kunusia peppermint
Kunusia harufu ya peppermint kume husishwa na kutibu hali ya kuhisi kichefu chefu. Kwa wanawake walio jifungua kupitia upasuaji wa C-section na walio kuwa na mimba, kunusia harufu hii kuliwa saidia kupunguza hisia za kichefu chefu.
3. Kata ndimu

Imedhihirika kuwa harufu ya tunda hili imesaidia kupunguza hisia za kutapika katika wanawake walio wajawazito. Kukata kipande cha ndimu ama kutoa maganda yake huenda kukafanya kazi kwa njia sawa kwa sababu mafuta muhimu yana achiliwa hewani. Ikiwa uko mbali na nyumbani, unaweza tumia mafuta yaliyo na harufu ya ndimu.
4. Dhibiti kupumua kwako
Kupumua pole pole na kwa ndani kume dhihirika kusaidia kupunguza kichefu chefu. Unapo pumua pole pole kupitia kwa mapua na kisha kutoa pumzi kupitia kwa mdomo angalau mara tatu, utakuwa ukipunguza hisia za kutapika.
5. Tumia viungo vya kupika
Viungo vingi vya kupika ni matibabu ya kinyumani ya kutibu hali ya kichefu chefu.
Poda ya fennel, cinnamon na cumin, zote ambazo zinatumika katika mapishi ni muhimu kupunguza kichefu chefu katika mimba, na katika kipindi cha hedhi.
Mbali na hayo hakikisha kuwa:
- Una epuka kula vyakula vyenye pilipili ama vilivyo na ufuta mwingi. Badala yake, kula vitu kama wali na ndizi
- Ongeza protini kwenye lishe yako
- Epuka kula vyakula vingi, badala yake, kula chakula kidogo mara nyingi kwa siku
- Kunywa maji tosha
- Fanya mazoezi
Chanzo: Webmd
Soma Pia: Ishara Za Kuwacha Kufanya Kazi Unapokuwa Na Mimba