Njia 4 Za Kupunguza Michirizi Mwilini Baada Ya Kujifungua

Njia 4 Za Kupunguza Michirizi Mwilini Baada Ya Kujifungua

Kupunguza michirizi mwilini huwa mojawapo ya matatizo yanayo msumbua mama baada ya kujifungua. Mbinu hizi za kinyumbani zitakufaa zaidi.

Michirizi ni urembo wa mama baada ya kujifungua. Ishara kuwa alibeba mtoto tumboni kwa miezi tisa, na hiyo ndiyo alama anayo baki nayo mwilini kumkumbusha safari yake ya ujauzito. Kwa sababu ya geni, kuna wanawake ambao wana bahati na kuepuka kupata michirizi hata baada ya kujifungua. Huku wengine wakitatizika jinsi ya kupunguza michirizi mwilini.

Michirizi huonekana kwenye matiti, tumbo, mapaja na sehemu zingine ambazo mama aliongeza ufuta alipokuwa na mimba. Baada ya kujifungua, ikiwa mama angependa kupunguza kuonekana kwa michirizi hii, kuna njia maalum ambazo anaweza kutumia kuzipunguza. Kumbuka kuwa ni vigumu kutoa kabisa michirizi hii na njia pekee ya kuitoa ni kwa kutumia mashine maalum inayo tumia miale ya moto. Hii ni njia ghali ambayo watu wengi hawana uwezo wa kugharamia. Tazama mbinu za kinyumbani zenye bei nafuu.

Njia rahisi za kupunguza kuonekana kwa michirizi mwilini

kupunguza michirizi mwilini

  1. Kutumia mafuta ya shea butter

Mafuta haya yanasifika kwa uwezo wake wa kupunguza alama za michirizi mwilini. Yametumika kwa muda mrefu kwa watu wakubwa na watoto pia. Chota kiwango kidogo cha mafuta haya na uweke kwenye kiganja chako. Sugua pamoja kutumia mkono mwingine. Kisha usugue kwenye sehemu iliyo na michirizi. Fanya hivi kila unapo koga. Ingawa itachukua muda kuanza kuona matokeo, zingatia mbinu hii kwa wakati bila kukoma.

2. Kutumia asali

Asali ina viwango vinavyo ondoa sumu na vinasaidia katika kupunguza kuonekana kwa michirizi katika sehemu fulani za mwili.

Chota kiwango cha asali na uweke kwenye kiganja chako. Kisha kwa upole, usugue sehemu ya mwili iliyo athiriwa na michirizi. Iwache hivi kwa angalau dakika 20 kisha usafishe sehemu hiyo kwa kutumia maji ya vuguvugu.

Rudia mbinu hii kila siku.

3. Aloe vera

homemade DIY moisturisers

Mmea huu una faida nyingi za kiafya. Hapo awali watu waliutumia kutatua hali tofauti za kiafya. Unatumika kupunguza hali ya upele usoni. Ili kutumia aloe vera kupunguza michirizi, kata sehemu ya mmea huu. Paka kwenye ngozi na uwache hivyo kwa dakika hadi 20. Safisha sehemu hiyo kwa kutumia maji ya vuguvugu.

Fanya hivi angalau mara 3 kwa wiki.

4. Sharubati ya ndimu

Tunda la ndimu lina asidi inayo saidia kupunguza michirizi. Jinsi ya kuitumia:

Paka juisi ya ndimu kwenye kiungo kilicho na michirizi. Iwache kwa dakika 10 kisha usafishe kwa kutumia maji yaliyo na joto. Ili kupata matokeo, rudia mbinu hii kila siku.

Soma Pia: Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kupunguza Tumbo Baada Ya Kujifungua!

Written by

Risper Nyakio