Jinsi Ya Kupunguza Tumbo Baada Ya Kujifungua Kutumia Mbinu Rahisi Za Nyumbani

Jinsi Ya Kupunguza Tumbo Baada Ya Kujifungua Kutumia Mbinu Rahisi Za Nyumbani

Kunywa maji tosha kuna saidia na uzito baada ya kujifungua. Kwa sababu kunapunguza ulaji wako wa kalori kwa kusawazisha hamu yako ya kula.

Tumbo kubwa huwa chanzo cha shaka kwa wamama wengi baada ya kujifungua na wanao azimia kupata mimba. Wamama wengi huwa na shaka kuhusu wakati wa wastani watakao kuchukua kupoteza uzito walio pata baada ya kujifungua, wakati ambapo wengine huwa na shaka kuhusu jinsi miili yao itakavyo kaa baada ya kujifungua na jinsi ya kupunguza tumbo baada ya kujifungua.

Wanawake huwa na wakati tofauti inapofika kwa kupoteza uzito baada ya kujifungua. Hata kama wanawake wengi hujipata katika shinikizo la kibinafsi baada ya kuona picha za watu mashuhuri kwenye magazini ambao walirudia miili zao kabla ya kujifungua kwa muda mfupi.

Wakati wa wastani wa kupunguza tumbo baada ya kujifungua ni upi?

kupunguza tumbo baada ya kujifungua

Kwa kawaida, inapaswa kuchukua kati ya miezi 6-12 kupunguza tumbo na uzito baada ya kujifungua. Kwa hivyo unapaswa kuweka kipindi chako kati ya muda huo. Baadhi ya wanawake wanaweza punguza hadi nusu ya uzito walio pata katika mimba wiki 6 baada ya kujifungua. Walakini, huku kuna lingana na sababu nyingi kama aina ya mwili na uzito ulio ongeza katika mimba. Ikiwa uzito ulio ongeza ni zaidi ya unao shauriwa kati ya pounds 25-35 (kilo 11.5-16), unapaswa kuwa mvumilivu zaidi na mchakato wa kupunguza uzito. Kupoteza uzito huenda kukachukua muda zaidi.

Uzito baada ya kujifungua hutoka wapi?

Uzito baada ya kujifungua sio miujiza kwa njia yoyote ile. Ni kufuatia tishu za matiti, amniotic fluid, kupanuka kwa uterasi, mzunguko wa damu, placenta na hifadhi za ufuta.

Kiasili, utapoteza kati ya kilo 5-6.5 baada ya kujifungua. Hii inahusisha amniotic fluid, placenta na uzito wa mtoto.

Je, kuna athari za kiafya usipo punguza tumbo na uzito baada ya kujifungua?

Ikiwa una panga kupuuza uzito baada ya kujifungua, fikiria tena. Uzito baada ya kupata mtoto huwa na hatari za muda mrefu kwa afya yako. Ikiwa unahitaji shauku zaidi, ndiyo hii.

Vidokezo vya jinsi ya kupunguza tumbo na uzito baada ya kujifungua salama

  • Zingatia lishe bora

kupunguza tumbo na uzito baada ya kujifungua

Inaonekana kama jambo la kawaida kugeukia vyakula vilivyo na kiwango kidogo cha kalori ili kupunguza uzito baada ya kujifungua kasi iwezekanavyo. Lakini hili sio wazo la busara.

Lishe zenye kalori ndogo hazina virutisho muhimu ambazo zinaweza saidia mwili wako kupona baada ya kazi kubwa ya kujifungua. Na mbali na hayo, unapo nyonyesha mwili wako unahitaji virutubisho hivi muhimu kutoa maziwa tosha.

  • Kuwa na lengo halisi kuhusu mchakato huu

Wanawake wengi wanataka kuona matokeo ya kasi. Hisia hii inaweza ibuka kutoka kuona marafiki zako wakipunguza tumbo na uzito baada ya kujfiungua kwa muda mfupi. Unahitaji kuelewa kuwa mifumo ya miili hutofautiana.

Kulingana na somo lililo fanyika na World Health Organization (WHO), karibu wanawake 1800 kutoka nchi tofauti hupoteza kilo 5.4 katika kipindi cha wiki mbili baada ya kujifungua.

  • Kunyonyesha

kukoma kunyonyesha mtoto

Ukichagua kunyonyesha, ina manufaa ya kiafya, kwako na mtoto wako. Mbali na kuwa na virutubisho, kuegemeza mfumo wa kinga wa mtoto, kunyonyesha kunasaidia na lengo lako la kupoteza uzito baada ya kujifungua kwa kupunguza saizi ya uterasi yako.

Kunyonyesha kunachoma idadi kubwa ya kalori, hadi 500 kwa siku. Kwa hivyo haupaswi kuwa na shaka kuhusu kiwango cha chakula unacho kula. Pia, ukiamua kuto nyonyesha ni sawa. Huku kuna maana kuwa mwili wako uta dumisha viwango vyake vya hamu ya kula.

  • Utaratibu wa kufanya mazoezi

Mazoezi yanakusaidia kwa njia kubwa. Ni njia ya kuchoma kalori zaidi. Lakini kabla ya kuanza mazoezi, wasiliana na daktari wako kuona kama uko mahali pazuri kufanya hivyo. Hasa kama ulijifungua kupitia upasuaji wa C-section.

Mazoezi yako sio lazima yawe magumu. Kumbuka kuwa, baada ya kujifungua, mwili wako huwa umechoka na kutatizika kulala wakati mwingi. Kwa hivyo mazoezi mepesi kama kutembea, kukimbia na kuogelea ni mazuri kwako.

  • Kaa mbali na vileo

Vileo huwa na kalori zaidi na unapo zichukua una ingilia kati ya mchakato wako wa kupunguza uzito wa mwili.

Na kwa wamama wanao nyonyesha, pombe inaweza ingilia kati utoaji wako wa maziwa ya mama. Na huenda ukakosa kuwa na maziwa tosha ya mtoto.

Vyakula rahisi ambavyo vinaweza kusaidia kupunguza tumbo na uzito baada ya kujifungua

Vifuatavyo ni vyakula vya kuongeza kwenye lishe yako ambavyo vinapatikana kwa urahisi nyumbani mwako ama karibu nawe. Na ikiwa hauna nyumbani, ni rahisi kuvipata kwa bei nafuu.

  • Maji

maji tosha mwilini ukiwa na mimba

Kunywa maji tosha kuna saidia na uzito baada ya kujifungua. Kwa sababu kunapunguza ulaji wako wa kalori kwa kusawazisha hamu yako ya kula. Lakini hasa kama wewe ni mama unaye nyonyesha, maji yanakusaidia kuwa na viowevu tosha mwilini baada ya kunyonyesha.

  • Matunda na mboga

Matunda na mboga kama machungwa, mchicha na tikiti maji huwa na viwango vidogo vya kalori na kuupa mwili wako madini muhimu.

  • Mayai na samaki

Mayai na samaki zina protini nyingi na ni rahisi kupata. Mimba huacha mwili wako ukiwa umenyooka sana na kulegea. Mwili wako hutumia protini kuregesha mwili wako kwa shepu yake ya kawaida baada ya kujifungua, ambapo ni mahali pazuri pa kuanza kupata shepu yako ya awali.

  • Vyakula vya nafaka nzima

Vyakula vya nafaka nzima kama vile oats na mtama ni rahisi kupata na sio bei ghali.

Vyakula hivi ni vizuri kwa mama anaye lenga kupunguza uzito baada ya kujifungua. Zina upa mwili wako fibre nyingi na kuepuka kupata uzito zaidi.

Kumbuka kuwa mvumilivu na mwili wako unapo anza juhudi za kupunguza tumbo na uzito baada ya kujifungua. Hakuna njia rahisi ya kupunguza uzito huu.

Soma Pia:Lishe Na Mazoezi Haya Yatakusaidia Kupunguza Uzito Wa Mwili Kwa Kasi

Written by

Risper Nyakio