Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kupunguza Tumbo Baada Ya Kujifungua!

Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kupunguza Tumbo Baada Ya Kujifungua!

Maji ni muhimu sana katika kukusaidia kutimiza lengo lako la kupunguza tumbo. Maji yana saidia mwili kutoa toxins na kupunguza tumbo.

Kubali mama, kurejesha tumbo ya hapo awali baada ya kujifungua ni kitu ambacho kila mama hutamani. Wengine hujitahidi kuipata, huku wengine wakikata tamaa. Habari njema ni kuwa, ufuta huo zaidi sio vigumu kutoa mwilini. Hapa kuna baadhi ya matibabu ya kinyumbani yatakayo kusaidia kupunguza tumbo baada ya mimba.

Vidokezo vya kupunguza tumbo baada ya mimba

1.Kinywaji cha asali na ndimu

vyakula usivyofaa kuhifadhi kwenye jokofu

Hii ni njia rahisi ya kupunguza tumbo baada ya kupata mtoto. Unahitaji kuchemsha maji, kisha uongeze ndimu. Toa motoni kisha uongeze kijiko kimoja ama viwili vya asali. Ngoja yawe ya vuguvugu kisha uyanywe. Kunywa maji haya ukiwa njaa kabla ya kula chochote.

Ikiwezekana, kunywa kinywaji hiki mara tu unapo amka kabla ya kunywa ama kula kitu chochote. Kisha ukae lisaa limoja ama dakika 30 kabla ya kuchukua kitu chochote. Pia, unaweza ongeza mint leaves na cucumber kisha uwache zikolee usiku wote. Usinywe mint leaves sana kwani zinaweza dhibiti utoaji wako wa maziwa.

2. Chai ya kijani (green tea)

Kikombe cha chai ya kijana husaidia kupunguza ufuta tumboni. Sio siri kuwa chai ya kijani ina wingi wa antioxidants.

Kumbuka kuchukua chai hii kwa viwango visivyo vingi. Kuinywa sana sio salama kwako na unapaswa kudhibiti kiwango cha kaffeini unayo chukua uki nyonyesha.

Epuka kutumia sukari kwenye chai yako ya kijani, kwani ita punguza juhudi zako.

3. Tufaha

Tufaha hazimweki daktari mbali tu, mbali ni muhimu katika kupunguza ufuta zaidi ulio kwenye sehemu ya tumbo. Tufaha zina pectin ambayo ni muhimu katika kuchoma ufuta ulio kwenye tumbo. Sawa na chai ya kijani, tufaha zina antioxidants zinazo epusha ufuta zaidi.

4. Lishe bora

Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kupunguza Tumbo Baada Ya Kujifungua!

Una kumbuka jinsi sahani yenye afya inavyo paswa kuwa? Hakikisha kuwa unaongeza matunda na mboga kwa wingi kwenye lishe yako, kisha nafaka nzima na protini zenye afya.

Punguza kiwango cha chumvi na sukari kadri uwezavyo. Epuka kunywa soda. Matunda na mboga kama vile papaya, maembe, broccoli, na sukuma wiki ni nzuri katika kupunguza ufuta kwenye tumbo.

Hata ukitia juhudi kupunguza tumbo baada ya kujifungua, usipuuze mahitaji yako ya virutubisho tumboni. Ni muhimu katika uponaji wako huku ukiendelea kunyonyesha mtoto wako.

5. Kula chakula kidogo ila mara nyingi

Kujinyima chakula ni hatari katika kipindi hiki kwani una nyonyesha na utakosa nguvu. Kula kiamsha kinywa chako, kisha chamcha na chajio. Na ule mara tatu ama nne kati ya lishe hizo. Unapo kula vyema, utachoma kalori zaidi mwilini.

6. Fanya mazoezi

Bila shaka mwili wako unaonyesha chakula unacho kula. Lakini, hakikisha kuwa unafanya mazoezi mepesi kama vile kutembea ama kuogelea. Epuka kufanya mazoezi magumu kwani huenda ukaiumiza uterasi yako ambayo ingali inapona.

7. Kunyonyesha

Ikiwa bado hauku ng'amua, kunyonyesha huchoma angalau kalori 500 kwa siku. Na kuisaidia uterasi yako kupungua hadi kwa saizi kabla ya mimba. Kwa hivyo ni muhimu katika kukusaidia kupunguza tumbo baada ya kujifungua.

10. Maji

African woman drinking water in a field

Maji ni muhimu sana katika kukusaidia kutimiza lengo lako la kupunguza tumbo. Maji yana saidia mwili kutoa toxins na kupunguza tumbo. Pia ni muhimu ili upate viowevu tosha unapo nyonyesha. Hakikisha kuwa unakunywa maji tosha kila siku.

Chanzo: Mom Junction

Soma Pia:Lishe Na Mazoezi Haya Yatakusaidia Kupunguza Uzito Wa Mwili Kwa Kasi

Written by

Risper Nyakio