Tumbo La Mama Baada Ya Kujifungua Na Jinsi Ya Kulipunguza!

Tumbo La Mama Baada Ya Kujifungua Na Jinsi Ya Kulipunguza!

Kupunguza tumbo la mama huwa mojawapo ya malengo makubwa kwa wanawake wengi baada ya kujifungua. Tazama vidokezo muhimu vya kukusaidia kutimiza lengo lako.

Sio jambo jipya kupata mama aliye jifungua akiwa na shaka nyingi kuhusu tumbo lake na jinsi ya kupunguza tumbo la mama. Kwani siku chache baada ya kujifungua, tumbo lake linazidi kuwa kubwa na kuonekana kana kwamba bado ana mimba. Mama, usiwe na shaka, ilichukua tumbo lako miezi tisa kuwa kubwa hivyo kwa hivyo haitachukua usiku mmoja kwa tumbo lako kurudi kuwa lilivyo kuwa hapo awali.

Tumbo La Mama Baada Ya Kujifungua

Tumbo lako lilikuwa limezoea kiumbe ndani na kuwa na umbo hilo. Mstari mweusi uliopo katikati mwa tumbo ya mama maarufu kama linea nigra na michirizi ama alama za kunyoosha bado zita zidi kuonekana. Kwa hivyo usitie shaka tumbo lako lina onekana lingali kubwa. Usijikwaze kimawazo kuhusu tumbo lako, baada ya muda, litaanza kupungua. Pia mstari mweusi katikati ya tumbo utaanza kupungua baada ya miezi michache.

Baada ya mtoto kuzaliwa, mwili wako utashuhudia mabadiliko mengi ya homoni. Mabadiliko haya yatalifanya tumbo lianze kupunguka baada ya muda. Mfuko wa uzazi ama uterasi inapo anza kubana, tumbo yako itaanza kupungua. Seli zilizokuwa mwilini wakati wa ujauzito zitaanza kutolewa mwilini kupitia kwa mkojo, ama uchafu unapo toa jasho. Katika kipindi hiki mama anapo anza kumnyonyesha mtoto, ufuta ulio ongezeka mwilini utaanza kupunguka na kwa kasi zaidi kama anafanya mazoezi mepesi.

Inachukua muda upi tumbo kuanza kupungua?

tumbo la mama

Ni vyema kwa wanawake kukumbuka kuwa miili yao ni tofauti. Kuna baadhi ya wanawake ambao hawatatiziki kurudia miili yao ya hapo awali, huku wengine wakichukua miaka na mikaka miili yao ya hapo awali kurejea. Kuna uwezekano wa umbo lako kuwa limebadilika sana wakati wa ujauzito. Kuwa na subira na mwili wako.

Njia za kupunguza tumbo la mama baada ya kujifungua

Kuna njia tofauti ambazo zime tumika kupunguza tumbo kwa muda mrefu baada ya kujifungua. Njia maarufu ni kama vile:

Kukanda tumbo: Mbinu hii ya kupunguza tumbo inafahamika sana hasa katika upande wa pwani. Kumkanda mama aliye jifungua kunasaidia tumbo kurejea kwa umbo la hapo awali, anaweza kulala vyema zaidi, kunatuliza misuli yake na pia kuboresha utoaji wake wa maziwa.

Kumnyonyesha mtoto: Mama anapo nyonyesha mtoto, anapunguza ufuta zaidi ulio tumboni. Ni vyema kukumbuka kuwa hili halitafuzu ikiwa mama anazidi kula vitafunio vyenye ufuta na sukari nyingi.

tumbo la mama

Mazoezi mepesi: Baada ya kujifungua, ni vyema kwa mama kuanza kufanya mazoezi mepesi. Wasiliana na daktari wako ili akupatie kibali cha kurejelea kufanya mazoezi. Mbali na kusaidia na mzunguko wa damu mwilini, kupunguza ufuta na kuboresha mhemko wa hisia, mama anaweza kupumzika vyema.

Lishe: Lishe ni muhimu sana kwa mama katika kupunguza tumbo la mama baada ya kujifungua. Pia, mtoto ana nufaika kutokana na virutubisho vilivyo kwenye lishe ya mama.

Chanzo: healthline

Soma PiaJinsi Ya Kufurahia Mapenzi Baada Ya Kujifungua Kupitia Upasuaji Wa C-section

Written by

Risper Nyakio