Jinsi Ya Kupunguza Uzani Baada Ya Kujifungua

Jinsi Ya Kupunguza Uzani Baada Ya Kujifungua

Baada ya miezi tisa ya kuwa kwa mwili unao badilika mara kwa mara, kila mama ana hamu ya kumwona mtoto wake. Pia unataka kuyakumbatia maisha ya kuwa mama. Kwa wakati huo huo, kuna sisitizo kubwa kwa miili baada ya kujifungua ya watu mashuhuri. Na jinsi walivyo kata uzani kwa kasi baada ya kujifungua. Na huenda ikaonekana kana kwamba kuna siri za kupunguza uzani baada ya kujifungua kwa kasi. Kukata uzito baada ya kujifungua sio rahisi.

Kwa wanawake wengi, kupata uzito wenye afya baada ya kujifungua sio rahisi. Huenda ikawa vigumu kumchunga mtoto mchanga, kuwa na ratiba jipya na kupona baada ya kujifungua. Walakini, ni muhimu kurudia uzito wako wa hapo awali baada ya kujifungua, hasa ikiwa unapanga kupata mimba ingine siku za usoni.

Tazama vidokezo hivi vya kupunguza uzani baada ya kujifungua

kupunguza uzani baada ya kujifungua

Kuwa na lengo maalum

Haijalishi majarida yanavyo kufanya uamini, kupunguza uzito baada ya kujifungua kunaweza chukua muda. Somo lililofanyika na Shirika la Afya Duniani la wamama 1,743 kutoka nchi tofauti lilipata kuwa wanawake wengi walikata  wastani wa kilo 44.7 katika muda wa wiki mbili na miaka miwili baada ya kujifungua.

Ni lengo linalo timizika kuamini kuwa baada ya mwaka mmoja ama miwili utapunguza karibu kilo 4.5. Ikiwa uliongeza uzito zaidi, huenda ukapata kuwa una kilo chache zaidi kuliko ulivyo kuwa kabla ya kupata mimba. Na lishe nzuri na mazoezi, unapaswa kutimiza lengo unalo tamani. Wakati ambapo uzito unao kata baada ya kujifungua huenda uka tofautiana. Cha maana ni kuwa unabaki katika kiwango chenye afya.

Kunyonyesha

kupunguza uzani baada ya kujifungua

Kunyonyesha mtoto wako baada ya kujifungua kuna manufaa mengi kwa mama na mtoto. Huku mtoto akipata virutubisho vinavyo faa vya kuegemeza mfumo wake wa kinga, mama ana nufaika kwa kupunguka kwa saizi ya uterasi. Hatari ya mama na mtoto ya kuugua pia inapunguka. Mama anapo zidi kunyonyesha, ana punguza uzito wake.

Kula protini zenye afya

Kuongeza protini kwenye lishe yako ni muhimu katika kuboresha mfumo wako wa kuchakata chakula, kupunguza hamu ya kula na ulaji mwingi wa kalori. Mwili unatumia nishati nyingi kuzichakata ikilinganishwa na vyakula vya aina zingine, na kufanya kalori zaidi zitumike mwilini. Protini zenye afya ni kama vile nyama laini, mayai, samaki, njugu, na bidhaa za maziwa.

Mbali na mbinu tulizo angazia, mama anashauriwa kufanya mazoezi mepesi, kunywa maji kwa wingi na kuhakikisha kuwa ana kunywa maji tosha. Ili kuongeza kasi mchakato wa kupunguza uzani baada ya kujifungua.

Chanzo: Healthline

Soma Pia:Tatizo La Upungufu Wa Damu Mwilini Baada Ya kujifungua

Written by

Risper Nyakio