Mwanamke huongeza uzito mwingi katika kipindi cha ujauzito. Sio vyema kwa mama kuanza mikakati ya kupunguza uzito angali mjamzito. Kwa hivyo mwanamke anapojifungua, wengi wao huanza mikakati ya kukata uzani wa mwili. Kujifungua ni jambo kubwa na mwili huchukua muda kabla ya kupona. Mara nyingi mama hushauriwa kuchukua mapumziko ya miezi miwili baada ya kujifungua kabla ya kurejelea mazoezi. Ili kuupa mwili wakati tosha kupona. Hata hivyo, mazoezi baada ya kujifungua yanapaswa kuwa kwa uangalifu wa mtaalum ili kuhakikisha kuwa mama hatajiumiza na kuathiri utoaji wa maziwa tosha. Lishe bora iliyo kamili ni muhimu kwa mama kumsaidia kutimiza lengo lake la kupunguza uzani wa mwili baada ya kujifungua.
Mbinu za kupunguza uzani wa mwili baada ya kujifungua

- Kula chakula kidogo mara zaidi
Ni vigumu kwa mama aliyejifungua kukosa kula, na sio vyema kwa afya ya mtoto wake. Kwa mama aliye na lengo la kupunguza uzito wa mwili, anashauriwa kula chakula kidogo kwa mara zaidi siku nzima. Kwa njia hii, mwili unapata wakati tosha kukichakata chakula. Na pia kinaweza kutumika vyema zaidi mwilini. Chakula hiki kinapaswa kuwa chakula chenye afya. Ongeza mboga za kijani na protini kwenye lishe yako.
- Kupunguza chakula chenye mafuta
Mafuta yana athari hasi katika kutimiza lengo la kupunguza uzito wa mwili. Hakikisha unakula chakula ulichokipika nyumbani. Epuka ulaji wa vyakula vilivyo kaangwa kwa mafuta kama vile vibanzi. Badala yake, kula vyake vyenye ufuta wa afya kama njugu, samaki na kuku. Njugu hukufanya uhisi kushiba kwa muda mrefu.

Mazoezi yana manufaa mengi kwa mwili na kwa kila mtu. Kwa wanao lenga kukata uzito wa mwili, ni vyema kuhusisha mazoezi katika ratiba zao za kila siku. Kwa mama aliye jifungua, mazoezi mepesi ni bora kwake. Kutembea, kupanda ngazi za nyumba na kuogelea.
Kunywa maji kabla ya kula chakula. Mara nyingi tunapohisi njaa, huwa kiu na unapokunywa maji, njaa inapungua. Kunywa maji kabla ya kula kunasaidia kupunguza kiwango cha chakula unachobugia.
Kuna mbinu tofauti za kupunguza uzani wa mwili baada ya kujifungua, ila ni vyema wakati wote kutumia mbinu zilizo salama kwa afya yako na ya mtoto.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Ishara 4 Zinazodhihirisha Kuwa Mama Ana Ujauzito Wenye Afya