Jinsi Ya Kupunguza Uzito Baada Ya Kujifungua: Vidokezo Vya Nyumbani

Jinsi Ya Kupunguza Uzito Baada Ya Kujifungua: Vidokezo Vya Nyumbani

Kula vyakula vyenye afya, matunda na mboga kwa wingi. Hakikisha kuwa una kula matunda ama mboga angalau mara tano kwa siku.

Kama mama mpya, utagundua kuwa una mengi ya kufikiria kuhusu na mengi ya kubadili na kuya husisha maishani mwako. Na umejifungua tu juzi. Kuna mabadiliko mengi ya mitindo ya maisha yanayo andamana na kupata mtoto. Kama vile kukosa usingizi siku nyingi na kunyonyesha mtoto kusiko isha. Na kati ya malengo ya mama aliye jifungua tu ni kuregesha mwili alo kuwa nao hapo awali. Ni muhimu kurejelea uzani wenye afya baada ya kujifungua, hasa ikiwa una panga kupata mtoto mwingine wakati usio mbali. Tume kusanya vidokezo vitakavyo kusaidia kupunguza uzito baada ya kujifungua.

Ikiwa unashangaa jinsi ya kupunguza uzito baada ya kujifungua, fuata vidokezo hivi:

weight loss

  1. Jipe wakati wa kupunguza uzani wa mwili

Huenda ukawa una hamu ya kuanza kuvalia rinda lililo kufurahisha zaidi hapo awali kabla ya kupata mimba, lakini utahitaji kujipa wakati kufika hapo. Mwili wako una hitaji wakati wa kupona baada ya kupata mtoto, na daktari huenda akakosa kukushauri uanze utaratibu wa kupunguza uzito bado. Unapaswa kungoja angalau wiki sita hadi nane baada ya kupata mtoto, kisha uulize daktari wako kuhusu uchuguzi ulio nao wa kupunguza uzito. Huenda akakushauri kufanya kazi na mtaalum wa lishe atakaye kueleza kuhusu mbinu zaidi za kutumia kutimiza malengo yako. Pia ata kushauri jinsi ya kufanya mazoezi, kulingana na mbinu ya kujifungua uliyo tumia, kupitia kwa uke ama kwa upasuaji wa C-section.

         2. Kula lishe bora

ratiba ya vyakula vya kukata uzito

Kula vyakula vyenye afya, matunda na mboga kwa wingi. Hakikisha kuwa una kula matunda ama mboga angalau mara tano kwa siku. Ongeza vyakula vyenye fiber kama vile oats, maharagwe na nafaka. Vyakula hivi vitakusaidia na nishati unayo hitaji katika jukumu lako mpya la mama. Jaribu uwezavyo kujitenga na vyakula vyenye ufuta mwingi, mikate ya kuoka na vinywaji kama soda. Kuwa makini kula viwango vinavyo stahili.

          3. Kunywa maji kwa wingi

Kunywa maji mengi kuna usaidia mwili kuwa na viowevu tosha. Yana kusaidia kuhisi umeshiba ili usiwe na njaa wakati wote. Pia, baadhi ya utafiti umeonyesha kuwa vinywaji vyenye maji mengi vina saidia mwili kuchakata chakula na kuchoma kalori mwilini.

          4. Kunyonyesha kutakusaidia kupunguza uzito

Kunyonyesha kuna manufaa mengi kwako na kwa mtoto wako. Ikiwa unapanga kumnyonyesha mtoto wako, hivyo ni vyema! Kwa sababu mtoto wako hapati virutubisho tu, mbali unachoma kalori pia.

          5. Fanya mazoezi

Punde tu daktari anapo sema ni sawa kwako kuanza kufanya mazoezi. Kuzoea ratiba ya wakati wa kulala wa mtoto na wakati wa kula kunaweza kosa kukupa wakati tosha wa kujiunga na darasa za kufanya mazoezi. Lakini kuna video nyingi za maagizo kwenye mtandao.

           6. Pata usingizi wa kutosha

Huenda ikawa vigumu kufanya hivi kwani mtoto bado hajazoea tofauti ya mchana na usiku. Na huenda akakuamsha usiku ili anyonye. Lakini hata hivyo, kuto pata usingizi tosha kuta tatiza lengo lako la kupunguza uzito wa mwili baada ya kujifungua.

Usipatiwe shinikizo na picha za watu unazo ona kwenye mtandao baada ya kujifungua. Kuwa na malengo halisi na uupe mwili wako wakati tosha wa kupona baada ya kujifungua.

Vyanzo: WebMD, Healthline

Soma Pia:Kujifungua Njia Ya Kawaida Ama Kupitia Upasuaji: Gani Ni Chungu Zaidi?

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio