Unaweza fanikiwa kukata uzito wa mapaja yako kwa kasi kwa kuchanganya mazoezi na lishe. Kuna misuli aina tatu zilizo kweny makalio yako: gluteus maximus, gluteus minimus na gluteus medius. Ni vigumu kupoteza uzito kwa sehemu moja ya mwili pekee, ila mazoezi tutakayo angazia ya kupunguza uzito haraka yatakusaidia kuwa na sehemu hizi za mwili zilizo na umbo bora.
Jinsi ya kuchoma ufuta wa mwili kwa kasi
Makala haya yana kuelimisha kuhusu kula lishe yenye afya na kufanya mazoezi ili kukata uzito wa mapaja kwa kasi.
Mazoezi ya kukusaidia kupunguza uzito haraka hasa kwenye mapaja yako

Kuna aina tofauti ya kuchutama kwa sababu tofauti, ila hii ina lenga mapaja na makalio yako. Tenganisha mguu wako umbali sawa na bega lako, kisha uiname kana kwamba unachutama huku makalio yako yakiwa yameinuka na uwe makini usijiumize magoti. Baki hivi kwa sekunde chache kabla ya kurudi ulivyo kuwa. Unaweza jaribu aina nyingine ya kuchutama. Jaribu kufanya zoezi hili kwa miundo tofauti.
Kucheza michezo na kikundi cha marafiki ni bora kwako. Ukiwa na marafiki wako hauchoki. Huenda ukahisi una hamu zaidi na kufanya hivi kila mara. Ila, iwapo hauna hamu ya kujiunga na mchezo, unaweza tembea. Kutembea hupuuzwa sana, ila kunaweza kusaidia kuchoma kalori nyingi mwilini kwa kutembea tu.
Lishe zinazo kusaidia kupunguza uzito haraka

- Punguza vinywaji vyenye sukari na unywe maji kwa wingi
Kunywa maji kwa wingi. Huwezi kosea kwa kunywa maji tu. Ni bei ya chini na yana patikana kwa urahisi. Yanatoa sumu mwilini na yana ladha nzuri. Nini isiyo ya kupendeza ya maji? Pia, maji husaidia na mzunguko wa virutubisho kwenye seli. Wataalum wana shauri ukunywe hadi lita 1.9 kwa siku. Vinywaji kama soda na sharubati zinapaswa kuepukwa. Zina kiwango kikubwa cha sukari na kalori na huenda zika ziba juhudi zako za kufanya mazoezi.
Walakini, sio vinywaji vyote ambavyo ni vibaya kwako. Unaweza kunywa chai ya kijani. Chai ya kijani ina polyphenols zinazo usaidia mwili kulinda seli. Pia, ni vyanzo vikuu vya antioxidants.
Kuchagua kwa umakini unacho tia mdomo huenda kukakusaidia kupunguza uzito wa mapaja. Usile chakula kingi mara maoja, jaribu kusawasisha lishe yako kwa kula vyakula vya makundi tofauti unapo kula. Kwa protini, chagua nyama laini kama vile samaki, na kwa wanga, chukua wanga kama oats na ngano. Pia, kwa matunda na mboga, kula sukuma wiki na blueberries, na kwa bidhaa za maziwa, chagua maziwa ya bururu.
-
Kula lishe yenye kalori kidogo
Hesabu ni rahisi. Utapoteza uzito zaidi ukichoma kalori zaidi kuliko ya unazo zikula. Punguza kiwango cha ufuta unao kula hadi gramu 35-60 kila siku. Badala yake, jaribu kula wanga wa matunda, mboga na nafaka nzima. Angalau gramu 170-240 kila siku, ambazo zinakupa asilimia 40-65 ya kalori za kila siku.

Ukitaka kupunguza uzito haraka hasa kwa mapaja yako, unapaswa kutafuta ulio salama kwa afya yako. Hadi pale ambapo daktari wako atakushauri, huenda ikawa sio salama kupoteza zaidi ya kilo mbili kila wiki.
Soma pia: Trying To Lose Weight After The Baby? These Home Remedies Are Cheap And Effective.