Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Jinsi Ya Kupunguza Uzito Ukiwa Na Mimba

3 min read
Jinsi Ya Kupunguza Uzito Ukiwa Na MimbaJinsi Ya Kupunguza Uzito Ukiwa Na Mimba

Kufuatia utafiti unaozidi kufanyika kila uchao, imedhihirika kuwa kupunguza uzito katika mimba kuna wezekana na huenda kukawa na faida kwa wanawake wenye uzito mwingi.

Katika dunia ambapo kila kitu kiko shwari na hakuna doa wala kasoro, ni ndoto ya kila mwanamke kuwa amejipanga vilivyo kuhusu mimba yake. Mipango kama vile kuwa na uzani unaofaa kabla ya kupata mimba. Lakini, kwa wanawake wengi, jambo hili haliwezekani. Ujauzito hata kama ni kipindi cha kufurahisha, kinaweza leta utata wa uzito mwingi wa mwili kwa wanawake walio na uzani wa juu. Kufuatia kuongeza uzito kunako husishwa na kubeba mtoto tumboni.

Kufuatia utafiti unaozidi kufanyika kila uchao, imedhihirika kuwa kupunguza uzito katika mimba kuna wezekana na huenda kukawa na faida kwa wanawake walio na uzani mwingi. Kumbuka kuwa, kupunguza uzito hakushauriwi kwa wanawake ambao walikuwa na uzani wenye afya kabla ya kupata mimba. Ikiwa ungependa kujihusisha katika kupunguza uzito katika mimba, ni vyema kuwasiliana na daktari wako, ili kuhakikisha kuwa kiinitete chako hakiathiriwi.

Kuwa na mpango mahususi kuhusu kupunguza uzito katika mimba

kupunguza uzito katika mimba

Ukuaji na maendeleo ya mtoto tumboni hutegemea mama, virutubisho anavyo tia mwilini na kisha kumfikia mtoto. Kuwa na uzani wa mwili wa kupindukia, kunaweza sababisha matatizo kama vile:

  • Kujifungua kabla ya wakati
  • Matatizo ya moyo kwa mtoto
  • Mtoto kuugua kisukari baadaye maishani
  • Mama kuwa na shinikizo la damu la juu
  • Kukosa usingizi
  • Kufura miguu ama damu kukosa kuzunguka
  • Maambukizi kwa mama
  • Kifo cha mtoto tumboni
  • Kujifungua kupitia kwa upasuaji wa c-section

Hata na hatari hizi, kumbuka kuwa haupaswi kukimbilia mbinu zinazo kuahidi matokeo ya kasi. Hakikisha kuwa unatumia mpango kabambe na wenye afya unao angazia mabadiliko ya mitindo yenye afya ya maisha. Daktari wako akikuruhusu kupunguza uzani katika ujauzito. Unaweza fanya haya.

  1. Fahamu kiasi cha uzito unacho hitajika kuongeza

Hakikisha kuwa hautabadili kupunguza uzito kuwe lengo lako kuu. Kila mwanamke mjamzito huongeza uzito wa mwili, kwa hivyo, usiwe na shaka kubwa. Kuna mwongozo kutoka kwa Shirika Kuu la Kisukari na Magonjwa yanayo husika na Figo na Uchakataji unao kusaidia kujua uzito unaopaswa kuongeza unapokuwa na mimba.

2. Punguza wanga unao kula

Sharti la kwanza la kukata uzito ukiwa na mimba huwa kupunguza kiwango cha wanga unacho kila. Hakikisha kuwa unakula kiwango kidogo cha wanga kila siku kwani mtoto wako bado ana hitaji virutubisho kutoka kwa wanga. Kumbuka kuwa wanawake wajawazito hawapaswi kula chini ya kalori 1,700 kwa siku. Ili kuhakikisha kuwa mwili wako unapata nishati.

3.  Fanya mazoezi angalau dakika 30 kwa siku

kupunguza uzito katika mimba

Kuna imani kuwa wanawake wajawazito hawapaswi kufanya mazoezi kwani huenda waka mwumiza mtoto. Imani hii sio kweli. Kuna baadhi ya mazoezi ambayo sio salama ukiwa na mimba, lakini mazoezi kwa ujumla yana manufaa mengi. Mazoezi yata kusaidia kupunguza maumivu ya mwili, na kukusaidia usiongeze uzani mwingi. Kumbuka kufanya mazoezi mepesi.

Soma Pia: Dalili Za Mimba Ya Kiume: Jinsi Ya Kufahamu Jinsia Ya Mtoto Unaye Mtarajia

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Pregnancy
  • /
  • Jinsi Ya Kupunguza Uzito Ukiwa Na Mimba
Share:
  • Njia 3 Bora Za Kupunguza Uzito Katika Uhusiano

    Njia 3 Bora Za Kupunguza Uzito Katika Uhusiano

  • Lishe Na Mazoezi Ya Kukusaidia Kupoteza Uzito Wa Mwili Kwa Kasi

    Lishe Na Mazoezi Ya Kukusaidia Kupoteza Uzito Wa Mwili Kwa Kasi

  • Kupunguza Ufuta Kwenye Tumbo: Masharti 5 Ya Kufuata Kupunguza Uzito Kwa Kasi

    Kupunguza Ufuta Kwenye Tumbo: Masharti 5 Ya Kufuata Kupunguza Uzito Kwa Kasi

  • Jinsi Ya Kupunguza Uzito Baada Ya Kujifungua: Vidokezo Vya Nyumbani

    Jinsi Ya Kupunguza Uzito Baada Ya Kujifungua: Vidokezo Vya Nyumbani

  • Njia 3 Bora Za Kupunguza Uzito Katika Uhusiano

    Njia 3 Bora Za Kupunguza Uzito Katika Uhusiano

  • Lishe Na Mazoezi Ya Kukusaidia Kupoteza Uzito Wa Mwili Kwa Kasi

    Lishe Na Mazoezi Ya Kukusaidia Kupoteza Uzito Wa Mwili Kwa Kasi

  • Kupunguza Ufuta Kwenye Tumbo: Masharti 5 Ya Kufuata Kupunguza Uzito Kwa Kasi

    Kupunguza Ufuta Kwenye Tumbo: Masharti 5 Ya Kufuata Kupunguza Uzito Kwa Kasi

  • Jinsi Ya Kupunguza Uzito Baada Ya Kujifungua: Vidokezo Vya Nyumbani

    Jinsi Ya Kupunguza Uzito Baada Ya Kujifungua: Vidokezo Vya Nyumbani

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it