Lishe Na Mazoezi Haya Yatakusaidia Kupunguza Uzito Wa Mwili Kwa Kasi

Lishe Na Mazoezi Haya Yatakusaidia Kupunguza Uzito Wa Mwili Kwa Kasi

Kufanya mazoezi na kula lishe yenye afya ni muhimu sana katika kukusaidia kutimiza lengo lako la kupunguza uzito wa mwili.

Ikiwa wewe ni mojawapo ya watu wengi wanao tatizika na uzito mwingi wa mwili na unatafuta mbinu yenye mafanikio ya kupunguza uzito wa mwili. Usiwe na shaka, kwani makala haya yatakuwa na manufaa kwako.

Kosa ambalo watu wengi wanao azimia kupunguza uzito wa mwili hufanya ni kulenga sehemu moja ya mwili. Kama ungependa kupunguza uzito wa mwili, mara nyingi utakuwa makini sana na mazoezi yanayo lenga tumbo. Ukweli ni kuwa, mbinu hii ya kufanya mazoezi haina mafanikio. Kuna baadhi ya mazoezi yanayo lenga zaidi ya sehemu moja ya mwili na mara nyingi, mazoezi haya ndiyo yatakayo kusaidia kutimiza lengo.

Jinsi ya kupunguza uzito wa mwili

Makala haya yana kuelimisha kuhusu mazoezi na lishe yenye afya itakayo kusaidia kutimiza lengo lako la uzito hasa wa mwili.

  • Kuruka kutumia kamba

kupunguza uzito wa mwili

Haijalishi mahali ulipo. Hii ni mojawapo ya mazoezi rahisi zaidi. Chukua kamba yako kisha ujaribu kuruka kwa angalau dakika 20-30 kila siku. Huenda ikawa vigumu kuruka kwa dakika nyingi hivi mwanzoni lakini kadri unavyo zidi kuzoea ndivyo utakavyo weza kufanya kwa urahisi. Unaweza gawanya dakika hizi mara mbili na uruke wakati tofauti kwa siku.

  • Kutembea

 

umuhimu wa mazoezi

Kitu cha kwanza unacho shauriwa kufanya unapo azimia kupunguza uzito wa mwili ni kutembea. Amka kutoka kitini hicho ulicho zoea kuketi kila siku bila kufanya chochote. Anza kwa kutembea dakika chache kama vile 10 kwa siku, baada ya siku 7, unapaswa kulenga kutembea kwa kati ya dakika 40-60.

Hakikisha kuwa haukai mahali pamoja kwa muda mrefu bila kufanya chochote. Tembea kutoka mahali pamoja hadi pengine badala ya kutumia gari. Pia hakikisha kuwa unafanya kazi nyumbani kama vile kufagia uwanja.

  • Kufanya squats

Kuna aina tofauti ya squats, na kila aina hulenga sehemu fulani. Anza kwa kueneza miguu yako iwe na upana sawa na mabega yako, kisha ukae kana kwamba una chuchumaa. Baki hivyo kwa sekunde chache kisha uamke na kurudia hivi mara 20. Zoezi hili lina lenga tumbo yako, mapaja na sehemu ya nyuma.

  • Jiingize kwa mchezo wa riadha

weight loss

Kucheza michezo ya riadha na marafiki wako ama wafanya kazi wengine kutakusaidia sana. Utapata hamasisho la kuzingatia utaratibu ule wa kufanya mazoezi. Baadhi ya michezo ambayo unaweza cheza ni kama vile kadanda, mpira wa vikapu, dondi na kadhalika.

Lishe itakayo kusaidia kupunguza uzito wa mwili

  • Koma kuchukua vinywaji vyenye sukari

Badala ya vinywaji vyenye sukari kama vile soda na sharubati, kunywa maji. Sukari hii inaziba juhudi zako za kukata uzani. Una shauriwa kunywa hadi lita 1.9 za maji kwa siku. Badala ya sukari, unaweza ongeza asali kwenye vinywaji vyako. Ongeza maziwa ya bururu kwenye lishe yako.

  • Epuka kula vyakula vilivyo chakatwa

Vitamu tamu ni vizuri lakini hakikisha kuwa unakula vitamu tamu vya afya. Badala ya kununua switi, nunua tufaha ama tunda lingine. Kuwa makini kwani kula vitu vyenye ngano iliyo chakatwa na isiyo nzima pamoja na sukari kutakufanya usikate uzani wako.

  • Kula lishe yenye afya

Kuwa makini na vitu unavyo tia mdomoni. Zingatia kiwango cha chakula unacho kula kwa siku. Kula chakula kingi kutaingilia kati juhudi zako za kupunguza uzito. Kula vyakula vyenye wanga nzima, matunda kwa sababu ya vitamini, protini, madini na fiber.

Soma Pia:Fanya Mazoezi Kuboresha Afya Na Urefu Wa Maisha Yako!

Written by

Risper Nyakio