Ujauzito ni kipindi kilicho jazwa na furaha, mapenzi, kugundua mambo mapya na pia kina changamoto zake. Mwili wa mama unabadilika kwa njia nyingi. Uterasi inavyo zidi kukua na kuwa kubwa, ndivyo mama anavyo zidi kutatizika kufanya baadhi ya majukumu. Anaweza tatizika kulala. Kuna baadhi ya vitu vinavyo tumika kurahisisha safari ya ujauzito. Soma zaidi!
Kurahisisha Safari Ya Ujauzito

- Vitamini za kabla ya kujifungua
Vitamini hizi ni muhimu kwa mama ili atimize kiwango kinacho hitajika cha vitamini cha kila siku. Ni vigumu kupata virutubisho vyote na idadi tosha kutoka kwa vyakula ambavyo mama anakula kwa siku. Tembe za vitamini zinamsaidia kupata virutubisho vyote. Pia zinasaidia katika ukuaji wa mtoto na kumwepusha mtoto kutokana na changamoto ya maumbile.
2. Mto wa ujauzito wa kulalia
Ujauzito ni safari ya kupendeza ila huandamana na changamoto zake. Mojawapo ya changamoto zilizoko ni kutatizika kulala. Tumbo la mama linazidi kukua na kuifanya iwe vigumu kwake kupata namna ya kulala kwa starehe. Kuna mito maalum ya wanawake wajawazito. Mto huu unawekwa katikati ya miguu na chini ya tumbo na kumwezesha mama kulala kwa starehe zaidi.
3. Sindiria mpya
Ujauzito huandamana na mabadiliko mengi mwilini. Kama vile matiti ya mama kuongezeka kwa saizi. Mama anahitaji kuwa na sindiria zinazomtoshea vizuri katika safari ya ujauzito. Kuna sindiria za ujauzito, spesheli za wakati mama anapokuwa na mimba na hata anaponyonyesha mtoto.

4. Mavazi ya ujauzito
Mwanamke huongeza uzito na kuwa mnene anapokuwa na mimba. Kwanza, uzito wa mtoto kisha anakula chakula zaidi katika kipindi hiki. Mambo yanayomfanya kuwa mnene kuliko alivyo kwa kawaida. Ni muhimu kwa mama kuhakikisha kuwa anavalia mavazi yasiyom-bana, tumbo ama sehemu nyingine. Mavazi bora kuvalia katika kipindi hiki ni rinda ama suruali za mama mjamzito.
5. Viatu vyenye starehe
Ujauzito unavyo zidi kukua, mama huenda akaanza kuumwa na miguu. Ni vyema kuwa na viatu vyenye starehe na saizi moja kubwa kuliko viatu vyake vya kawaida. Huu sio wakati wa mama kuvalia viatu vyenye visigino virefu, atashinikiza miguu yake ama kuanguka na kujiumiza. Huu ni wakati wa kuvalia viatu vyenye starehe kwake.
6. Krimu ya kupunguza alama za kunyooka
Mwili hupata alama za kunyooka mtu anapo kuwa mnene ama kukonda kwa kasi. Tumbo la mama hukua kubwa kadri siku zinavyo zidi kusonga na kumfanya apate alama za kunyooka. Kupaka krimu za kudhibiti athari za alama hizi kunasaidia ngozi yake izidi kupendeza. Mama anashauriwa kuanza kujipaka krimu hii punde tu anapofahamu hali yake ya mimba.
Chanzo: healthline
Soma Pia: Vidokezo Vya Kuwa Mama Mwema Kwa Watoto Wako: Sifa 5 Za Mama Mwema