Wazo la mwisho akilini mwa mama aliyejifungua ni tendo la ndoa. Wiki za kwanza baada ya kutoka hospitalini na mtoto wake, mama ameyaanza maisha mapya. Ana majukumu mengi mapya na anapaswa kufanya vitu vingi. Katika kipindi hiki, wakati wake mwingi huwa wa kuwa na mtoto wake na kuboresha utangamano wake na mwanawe. Angali anajifunza kubadilisha nepi, na kumvalisha mavazi. Kumlisha mtoto baada ya kila masaa mawili ama matatu kuna maana kuwa mama hatapata wakati tosha wa kulala usiku. Pia, ana kuchukua muda huu kupona. Ni wakati upi bora wa kurejelea mapenzi baada ya c-section?
Mama huenda akashangaa jinsi kurejelea mapenzi baada ya c-section kutakavyokuwa. Mama aliyejifungua kupitia kwa c-section na aliyejifungua kwa njia ya kawaida kupitia kwa uke, wote huwa na matatizo kurejelea matendo ya kimapenzi. Wanawake wote huwa na changamoto wanaporejelea matendo ya kimapenzi baada ya kujifungua.
Wakati bora kwa mama kufanya mapenzi

Hakuna wakati hasa wa kurejelea kufanya mapenzi baada ya upasuaji wa c-section. Hata hivyo, wanawake wengi watangoja kati ya wiki nne hadi sita kabla ya kurejelea matendo ya kitandani. Ili kuupa uke muda tosha wa kupona.
Mama huvuja damu kiasi kidogo na upasuaji wa c-section na atapona katika kipindi cha wiki sita. Hata hivyo, ni vyema wakati wote kurejelea kufanya mapenzi baada ya kupatiwa kibali na daktari wake.
Uponaji wa kidonda cha C-section

Uterasi ya mwanamke huchukua kipindi cha wiki sita kurejelea saizi yake ya kawaida na kizazi chake kufungana. Katika kipindi hiki, mama atavunja damu, lakini hali hii hupungua. Mwanamke anastahili kurejelea matendo ya kindoa baada ya kizazi chake kufungana. Kabla ya wakati huo kufika, mama hapaswi kuweka kitu chochote kwenye kizazi chake. Ngoja kipau mbele kutoka kwa daktari wako kabla ya kurejelea kufanya mapenzi.
Wanandoa wanapaswa kuzungumza kuhusu mapenzi na wanaweza kujihusisha katika matendo yasiyo ya kufanya ngono. Ili kudumisha utangamano na mapenzi yao. Baada ya kurejelea matendo ya ngono, wanawake wanapaswa kutumia njia ya kupanga uzazi, kwani mama ako katika hatari ya kutunga mimba tena punde baada ya kujifungua. Daktari atamshauri njia bora za kupanga uzazi.
Ni muhimu kwa mama kuupa mwili wake muda tosha wa kupona kabla ya kuanza kufanya tendo la ndoa tena.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Jinsi Ya Kumdhamini Mchumba Baada Ya Kujifungua Mbali Na Kufanya Ngono