Kusafiri na mtoto wako sio jambo rahisi, kusafiri na watoto zaidi ya mmoja ni shida zaidi. Kusafiri na mtoto zaidi ya mmoja ni jambo linalomkwaza mzazi, hasa mama kwani yeye ndiye anayepanga vitu vingi. Tazama baadhi ya vidokezo kwa mama anayepanga kusafiri na mtoto zaidi ya mmoja.
Vidokezo vya matayarisho kabla ya safari

- Kusafiri na watoto ambao ni mapacha ama wasiokuwa katika umri mmoja, kuna maana kwamba kuna vitu zaidi unavyostahili kuangazia. Haijalishi iwapo mnasafiri kutumia gari la kibinafsi, ndege ama matatu.
- Ikiwa aliye mzee kwa watoto wako anaweza kukusaidia na baadhi ya mambo huku ukimchunga mdogo wake, mwambie unavyotaka kusaidiwa. Ila si hivyo, tafuta mtu mwingine ambaye mnaweza safiri naye ili akusaidie kuwatunza watoto.
- Ikiwa mtoto wako mmoja anapenda kulala mchana, ni vyema kupanga safari wakati utakao wafaa, ili wapumzike vya kutosha.
- Ukipanga kuanza safari kabla ya mtoto wako kulala, hakikisha kuwa unabeba vitu vinavyo wastarehesha kama vile vidoli. Huenda usingizi wa mtoto wako ukakatizwa katika safari na ni vyema kuhakikisha wana vitu vitakavyowafanya watulie wasilie ovyo.
- Ikiwa unapanga kusafari kwa ndege wakati wa usiku. Ni vyema kupanga safari na wakati ambao watoto wako watakuwa wamelala ili wapate usingizi tosha.
- Ikiwa safari yenu ya ndege ni fupi, masaa manne hivi, panga safari hii na wakati ambapo mtoto wako atakuwa amelala ama wakati wake wa kula. Mtoto mwenye njaa katika mazingira mapya atasumbua sana.
Panga vitu hivi kwenye begi la safari
Ili kuhakikisha kuwa unapanga kila kitu unachohitaji kwenye safari yako, hakikisha kuwa unaanza kupanga siku chache kabla ya siku utakayosafiri. Kwa kufanya hivi, unapokumbuka kuna kitu ulisahau, una wakati wa kukiongeza. Tofauti na kupanga siku utakayosafiri. Una nafasi zaidi za kusahau vitu vingine.

Vitu muhimu kubeba
Mavazi ya kila siku. Kulingana na hali ya anga ya mahali mnako zuru, beba mavazi ambayo ni bora. Kwa mfano, ikiwa mnasafiri kwenda mahali kuliko na joto jingi kama Mombasa, beba mavazi mepesi.
Mavazi zaidi. Ikiwa safari yenu ni ya siku mbili, beba mavazi ya nguo tatu ama nne, kwani mtoto huchafua nguo kwa urahisi.
Mavazi ya kulala ama pyjamas. Ni muhimu kuwa na mavazi ya kubadili kabla ulale, hakikisha mavazi haya yanajoto tosha.
Soksi, kofia na viatu, kulingana na hali ya hewa.
Taulo, yako na za watoto. Hata kama mnaenda kwa hoteli, ni vyema kuwa na taulo zenu ambazo ni safi.
Dawa za mtoto, iwapo kuna mtoto anayechukua dawa zozote zile.
Vidokezo mnapo safiri
Iwapo mnasafiri kwa ndege, shinikizo la ndege litamfanya mtoto akose starehe na ahisi uchungu kwenye masikio. Sawa na watu wazima, kutafuna na kumeza kitu kutamsaidia kupunguza shinikizo kwenye masikio.
Kumnyonyesha mtoto kunamsaidia ahisi vyema na awe na starehe zaidi kujua ako karibu na mamake. Iwapo mtoto wako analishwa kupitia kwa chupa, mpe anywe pamoja na vitamu tamu vyenye afya.
Mnapo wasili
Kusafiri na watoto zaidi ya mmoja kunahitaji ufahamu utu wa kila mmoja wao. Kwa njia hii, utaweza kupanga mambo mtakayo fanya mnapowasili, kulingana na vitu ambavyo kila mtoto hutaka.
Hakikisha kuwa wakati wote mnaposafiri, watoto wako katika umbali unaoweza kuwafikia kwa urahisi. Isizidishe urefu wa mkono wako. Usalama ni muhimu wakati wote. Panga michezo na mambo yanayowafurahisha watoto wako. Ikiwezekana, safiri na mtu mwingine atakayekusaidia kuwaangalia watoto wako.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Faida Za Kufanya Mazoezi Katika Mimba Kwa Mama Na Mtoto!