Kusafiri peke yako sio jambo linalokumbatiwa na watu wengi. Hasa kwa sababu unazuru sehemu mpya mbali na nyumbani kusipo na watu unaowajua. Jambo linalohusishwa na hatari zake. Kama vile kuibiwa, kupotea na maovu mengine. Hata hivyo, hofu nyingi zitakuzuia kufurahia vitu ambavyo sehemu tofauti zinazo, urembo, tamaduni mpya na mitindo ya maisha iliyo tofauti.
Unaposafiri peke yako, utasoma vitu vingi na kupata manufaa yatakayo kusaidia katika nyanja tofauti za maisha yako.
Manufaa ya kusafiri peke yako

- Unajiamini zaidi
Kusafiri peke yako hasa kama unapenda kuwa miongoni mwa watu wakati wote sio jambo rahisi. Ni jambo linalohitaji ujasiri mwingi. Utakapo safiri peke yako, utapata ujasiri zaidi wa kufanya vitu peke yako na kujiamini katika kila unalolifanya. Unapohisi hauna furaha, nenda mahali peke yako, inasaidia. Unaposafiri peke yako kwa mara ya kwanza, safiri mahali ambapo umekuwa hapo awali ama pasipo mbali na nyumbani. Utahisi vyema zaidi.
2. Kuwajibika
Kutoka kwa kupanga safari yako, mahali utakapo lala, utakachofanya na fedha hitajika za safari hiyo. Kufahamu kuwa wajibu wa kujilinda uko kwako, hasa katika sehemu mpya usipofahamu mtu yeyote. Kutakusaidia kuwajibika zaidi, katika safarini na maisha yako baada ya safari ile.
3. Unapata ujasiri zaidi
Hakuna kitu kinachokupatia ujasiri zaidi kama kufanya vitu peke yako. Unafahamu kuwa hakuna jambo usiloweza kufanya ukiwa peke yako. Unapotaka kusafiri mara nyingi, huenda ukagundua kuwa marafiki wako wako kazini, wana shughuli zao ama hawana pesa za kusafiri. Kuwaacha nyuma na kufanya uamuzi wa kusafiri peke yako ni ishara ya ujasiri. Hii itakuwa hatua ya kwanza ya hatua zaidi za ujasiri utakazochukua peke yako.

4. Unasoma vitu vingi
Kusafiri huimarisha mtazamo wako kuhusu maisha, watu na mambo tofauti. Unaposafiri, utapatana na watu kutoka sehemu tofauti, baada ya kuzungumza nao, utafahamu kuwa, ulikuwa na maoni yasiyo ya kweli kuwahusu. Pia utaweza kusoma kuhusu njia za maisha za watu wengine. Utagundua kuwa watu wengi wanalenga kukusaidia ikilinganishwa na watu wanaotaka kufaidika kwa njia isiyo halali.
5. Kutangamana na watu na tamaduni tofauti
Kujipata katika tamaduni mpya miongoni mwa watu wapya ni jambo la kuogopesha kwa mara ya kwanza. Kwa wasafiri, njia bora ya kufurahia safari yako ni kwa kutangamana na watu wa mahali uposafiri. Kumbatia tamaduni mpya na utasoma vitu vingi na kupata marafiki wapya.
6. Kuwa mtu binafsi
Kupanga safari kama kundi huwa jambo la kufurahisha na bila shaka mtakuwa n wakati mwema. Ila, unapopanga safari peke yako, utaweza kuwa mtu binafasi na kupata uhuru wa kufanya uamuzi peke yako. Utaweza kutatiza matatizo peke yako bila kumtegemea mtu yeyote. Pia, itakuwa rahisi kwako kuzungumza na kuingiliana na watu wengine.
Usiwe na hofu, chukua hatua ya kwanza kwenda safari ya kwanza ukiwa peke yako, bila shaka utakuwa na muda wa kipekee maishani mwako!
Chanzo: Africaparent
Soma Pia: Kusafiri Na Mtoto Mchanga: Kanuni Muhimu Za Kuzingatia