Kuna uhusiano mkubwa kati ya umri wa mwanadada na uzalishaji wake wa uzazi. Kadri mwanamke anavyozidi kuzeeka, ndivyo uwezo wake wa kupata mtoto unavyopunguka. Umri bora zaidi wa kubeba mtoto ni chini ya miaka 35. Baada ya umri huu, nafasi za kushika mimba kiasili hupunguka. Huchukua muda upi kushika mimba baada ya tendo la ndoa?
Wakati bora kutunga mimba

Mwanamke huwa na siku sita katika kila mzunguko wa hedhi kila mwezi wa kushika mimba kwa urahisi. Siku ya kupevuka kwa yai huwa bora kwa mwanamke kushika mimba kwa urahisi. Ikiwa mwanamke hana uhakika wa siku yake ya kupevuka kwa yai, anaweza kuwasiliana na daktari wake ama kutumia kifaa cha kubaini siku hii. Baadhi ya mabadiliko yanayo fanyika mwilini katika kipindi hiki ni:
- Ute kuongezeka
- Maumivu kwenye tumbo
- Matiti kuwa laini
- Kubadilika kwa kizazi
- Mabadiliko ya temprecha mwilini
Unapaswa kufanya ngono mara ngapi kushika mimba?
Kufanya ngono mara moja katika siku ambapo mwanamke anarutuba zaidi kunaongeza nafasi zake za kushika mimba. Kuwasiliana na mtaalum wa afya katika kipindi hiki ni bora zaidi ili awashauri kuhusu mara mnazopaswa kujihusisha katika tendo la ndoa.
Kuna uwezekano wa kushika mimba baada ya kufanya ngono mara moja
Naam. Ikiwa mwanamke alifanya tendo la ndoa siku alipokuwa na rutuba zaidi bila maarifa yake, bila shaka atapata mimba. Ni vyema wakati wote kutumia kinga iwapo hauko tayari kuwa mzazi.
Inachukua muda upi kushika mimba baada ya tendo la ndoa

Huenda ikachukua hadi siku tano kwa manii na yai kupatana. Kisha siku kati ya sita hadi kumi kwa yai lililorutubishwa kujipandikiza kwenye kuta za uterasi. Kisha safari ya ujauzito kuanza.
Kuboresha rutuba
Wanandoa wanaweza boresha rutuba ili kuwasaidia kushika mimba kwa urahisi kwa kufanya mambo yafuatayo.
Kuzingatia lishe bora. Iliyo na virutubisho muhimu, hakikisha kuwa lishe ina protini tosha.
Kuwa na uzito wa wastani. Uzito wenye afya huifanya rahisi kwa wanandoa kushika mimba kwa urahisi.
Kukoma kutumia bidhaa zilizo na nicotine nyingi kama sigara.
Kufanya mazoezi. Mazoezi yana saidia kuzibua mishipa inayosafirisha manii na kumfanya mwanamke kuwa na afya bora, hivi basi kuboresha uzalishaji wake.
Kufanya tendo la ndoa mara kwa mara ili kuongeza nafasi za wanandoa kushika mimba kwa urahisi.
Soma pia: Umuhimu Wa Mazoezi Ya Kuleta Uchungu Wa Uzazi Katika Ujauzito