Tofauti na siku za hapo kale ambapo mabinti walioleka mapema hata kabla ya kufikisha miaka 20, siku hizi wanawake wengi wanafanya uamuzi wa kuoleka wanapo hisi wako tayari. Wanawake wengi wanafanya uamuzi wa kuoleka wanapofikisha miaka 30. Anapofanya uamuzi wa kushika mimba katika miaka ya 30's, mwanamke huwa amejipanga kimaisha, kifedha na kutimiza malengo yake ya kikazi na kimasomo. Ana ujuzi zaidi kuhusu changamoto za kuwa mama na ana kikundi cha watu watakao msaidia.
Hata hivyo, nafasi za kutunga mimba baada ya miaka 30 huanza kupunguka kufuatia mabadiliko ya kibiolojia. Ikiwa ungependa kuwa mama na bado unachelewesha kutunga mimba, ni vyema kufahamu athari hasi na chanya kisha ufanye uamuzi wako.
Nafasi za kushika mimba katika miaka ya 30's

Mwanamke ana nafasi za asilimia 86 kutunga mimba kwa urahisi anapokuwa katika miaka yake ya kati ya 30-34. Athari hasi ni kuwa nafasi zake za kupoteza mimba ni asilimia 20. Mwanamke anashauriwa kuwasiliana na mtaalum wa afya ya wanawake kabla ya kutunga mimba anapokuwa katika miaka yake ya 30.
Katika miaka ya 35-37, asilimia ya mwanamke kutunga mimba huwa 78. Ila katika miaka hii, nafasi za matatizo katika mimba kuibuka huongezeka. Changamoto kama vile mimba kuharibika, mtoto kuwa na ulemavu ama Down's syndrome. Pia, wao huchukua muda zaidi kushika mimba ikilinganishwa na wanawake wa umri wa chini.
Mazuri na Mabaya Ya Kutunga Mimba Katika Miaka Ya 30's

Mazuri yake
Mojawapo ya sababu kuu ambazo wanawake hufanya uamuzi wa kupata watoto baadaye maishani. Wanawake wengi huwa wamefanya uamuzi wa njia ya kikazi wanayo taka kufuata na wana maarifa zaidi. Kulea watoto ni gharama kubwa, na wazazi wanapaswa kuwa wamejipanga kifedha kukimu mahitaji ya watoto.
Unapokuwa mchanga, katika miaka yako ya mapema ya 20's hauna maarifa kuhusu vitu vingi maishani. Unapofikisha miaka ya 30's, umeona vitu vingi na kuelimika zaidi. Unapofanya uamuzi, unafikiria kwa kina na kuangalia pande zote kisha kuamua kitakacho faa zaidi.
Nafasi kubwa ni kuwa, unapokuwa katika miaka ya 30's, utakuwa katika uhusiano bora ama ndoa. Baadhi ya wanandoa hungoja miaka michache baada ya kufunga ndoa kabla ya kupata watoto.
Mabaya yake
Mwanamke ako katika hatari ya juu ya kupata matatizo anapokuwa na mimba kama vile shinikizo la juu la damu. Ana shauriwa kula lishe bora na kufanya mazoezi mara kwa mara.
- Kuchukua muda kushika mimba
Tofauti na mwanamke anapo jaribu kushika mimba anapokuwa katika miaka yake ya 20's, katika 30's, unachukua muda mrefu kushika mimba.
- Nafasi ya juu ya kupoteza mimba
Nafasi za mimba kuharibika ama mama kujifungua mtoto aliye aga dunia huwa zaidi katika miaka hii.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Aina Ya Maumivu Ya Matiti Yanayo Ashiria Ujauzito: Aina Na Matibabu Yake!