Wanawake zaidi wanaamua kuwa wazazi katika miaka ya 30's. Kuna imani kuwa mwanamke hawezi tunga mimba katika miaka yake ya 30's, hiyo ni imani tu. Hata hivyo, nafasi zake za kutunga mimba zinapunguka na huenda akachukua muda zaidi. Hata hivyo, anaweza kuongeza nafasi zake za kushika mimba katika umri wa 30's kwa kufanya hivi!
Kushika Mimba Katika Umri Wa 30's

Lishe ni ina jukumu kubwa katika kumsaidia mwanamke kutimiza lengo la kushika mimba. Kuna baadhi ya vyakula vinavyo msaidia mwanamke kushika mimba kwa kasi. Hakikisha kuwa sahani yako ina mboga na matunda, pia punguza ulaji wa vitamu tamu, vyakula vilivyo chakatwa na vyenye ufuta mwingi.
- Koma kutumia vileo na kuvuta sigara

Sigara na vileo vimedhihirishwa kupunguza nafasi za wanawake kujifungua kwa urahisi. Katika wanaume, sigara na pombe zinapunguza idadi ya manii na hivyo basi kupunguza uwezo wao wa kuzalisha mkewe. Kushika mimba kunafuzu kufuatia juhudi za mwanamke na mwanamme. Kwa hivyo wachumba wanapaswa kupunguza utumiaji wa sigara na pombe.
- Koma kutumia uzazi wa mpango

Baadhi ya mbinu za kupanga uzazi huchukua muda kabla ya homoni mwilini kurudi kawaida. Hasa mbinu za kupanga uzazi zenye homoni. Mwanamke anaye jaribu kutunga mimba anapaswa kukoma kutumia uzazi wa mpango. Wasiliana na daktari wako, anaweza shauri dawa za kusaidia kurejesha viwango vya homoni mwilini kawaida.

Maisha yana changamoto nyingi na ni vigumu kuto sombwa na mawazo katika wakati mmoja maishani. Mawazo ya kikazi, kifamilia, uhusiano ama gharama ya maisha kwa jumla. Kusombwa na mawazo kuna athari hasi mwilini na kupunguza nafasi za mama anaye tamani kushika mimba kwa kufanya iwe vigumu kwake kutimiza malengo yake.
- Wasiliana na mtaalum wa afya ya kike

Kumtembelea mtaalum wa afya ya kike kabla ya kuanza juhudi za kushika mimba ni muhimu. Atafanya vipimo kuhakikisha kuwa mwanamke hana matatizo ya kiafya. Na iwapo ana matatizo ya kiafya, atamshauri anacho paswa kufanya ili kumsaidia kushika mimba kwa urahisi. Kliniki ni muhimu hata baada ya kushika mimba ili kufuatilia ukuaji wa mtoto na kukabiliana na matatizo yoyote ya kiafya.

Mazoezi ni muhimu katika umri wowote ule na kwa kila mtu. Ila, kwa mwanamke anayetaka kushika mimba, mazoezi ni muhimu sana. Kufanya mazoezi kunaupa mwili nguvu za kustahimili safari ya ujauzito. Misuli ya pelviki inapata nguvu za kumwezesha mama kujifungua kwa urahisi. Hata baada ya kushika mimba, mwanamke anahimizwa kuzidi kufanya mazoezi ili kupunguza maumivu ya mwili na kumwezesha kulala vizuri. Ni rahisi kwa mama anayefanya mazoezi kupunguza uzani wa mwili baada ya kujifungua.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Hatari Na Faida Za Kushika Mimba Baada Ya Miaka 35