Utafiti Wapendekeza Kuwa Kushikana Mikono Kunasaidia Kupunguza Uchungu Wa Uzazi

Utafiti Wapendekeza Kuwa Kushikana Mikono Kunasaidia Kupunguza Uchungu Wa Uzazi

Utafiti wa hivi maajuzi umedhihirisha kuwa kushikana mikono kati ya wanandoa kunasaidia sana kupunguza uchungu wa uzazi.

Kushikana mikono na umpendaye huenda kukakujaza na amani nyingi. Inakuashiri mapenzi na utunzi wao. Ila, utafiti mpya unasema kuwa kuna enda zaidi ya starehe za hisia. Unapomshika mwenzako mkono, inaweza saidia kupunguza uchungu wa kifizikia – hata wakati wa uchungu wa uzazi!

Kushikana mikono na mwenzi wako kutakusaidia kupunguza uchungu wa uzazi!

delivery support

Utafiti ulio fanywa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Colorado una sema kuwa mguso huo una nguvu za kufanya kazi ya dawa za maumivu.

Karatasi hii ina ashiria nguvu na umuhimu wa mguso wa binadamu, “mwandishi mkuu wa utafiti huu Pavel Goldstein anaeleza Medical Daily, huku akiongeza jinsi alivyo soma na maisha yake ili kufanya utafiti huu.

Bibi yake daktari Goldstein alikuwa akikifungua alipogundua jinsi kumshika mkono kulisaidia kupunguza uchungu!

Kwanza akaanza kufanya utafiti wa nadharia hii. Na usaidizi wa timu kutoka Chuo Kikuu cha Haifa, alipata wanandoa wa jinsi mbili tofauti wa umri wa kati ya miaka 22 na 32 na kuwa fanyia vipimo jinsi akili iliitikia mguso walipokuwa wakihisi uchungu.

Ukimshika mwenzi wako mkono, akilini zenu zita kuwa na usawazishaji

hold hands during labour

Holding your partner’s hand is a loving sign of empathy that causes brainwaves to fall in sync. Picha: UNICEF

Wakati wa masomo haya, wanandoa hawa – wote ambao walikuwa pamoja kwa angalau mwaka mmoja –  waliulizwa washikane mikono na wanawake waka fanywa wahisi uchungu kiasi. Joto ya kiwango cha chini ulishinikizwa kwenye upande wa mbele wa mkono wao huku mwitikio wa akili zao ukichunguzwa kwa makini kupitia electroencephalography (EEG) walipokuwa wakishiana mikono na walipokuwa wameachana.

Haya ndiyo matokeo waliyo pata:

 • Unapo mshika mwenzi wako mkono, kupumua kwako, mpigo wa moyo na akili zako huwa na usawazishaji.
 • Hata bila ya kugusana, EEG iligundua kuwepo kwa aina ya usawazishaji wa kiakili.
 • Kadri kiwango cha juu cha ukarimu unachohisi kwa mwenzi wako, ndivyo kiwango cha juu cha athari kwenye usawazishaji wa kiakili.
 • Wakati ambapo akili za wanandoa hukua katika usawa, huenda uchungu ukapungua.
 • Utafiti huu ni wa mwisho katika masomo mengi yanayo angazia usawazishaji kati ya binadamu.

Cha kupendeza, siyo?

Jinsi Mabwana wanaweza kuwa wa egemezo zaidi katika uchungu wa mama na kujifungua

kushikana mikono

Isipokuwa kama umejifungua, hakuna njia unaweza elewa jinsi uchungu wa mama unavyokuwa ama kuhisi. Ila wachumba wanaweza fanya kadri wawezavyo kuegemeza mama mtarajia – kutoka kuwa hapo kifizikia na kuwasikiza.

Mbali na kushikana mikono kwa mara kwa mara, hapa kuna vitu muhimu vya kutia akilini kwa baba watarajiwa ambao pia ni wazazi wa mtoto mtarajiwa.

 • Hakikisha kuwa bibi yako hayuko peke yake na uwe naye na uwasaidie kuburudika wakati huu wa hatua za mapema za uchungu wa uzazi.
 • Panguza uso wa bibi yako unapohitajika na umempe maji ya kunywa (kulingana na ulivyo shauriwa na daktari wenu.
 • Mpe bibi yako masi kwenye mgongo na mabega.
 • Msaidie bibi yako kutembea tembea na kumgeuza upande aliolala inavyo hitajika.
 • Mpatie egemeo la kihisia kwa kumjaza na maneno ya kumhimizi kadri uchungu wa mama unavyo zidi.
 • Wasaidie kutumia mbinu za kupumzika na kupumua.
 • Kuwa egemeo lake, hata kunapokuwa na mabadiliko ya mpango wa kujifungua (kama vile kuchagua mbinu tofauti za kupunguza uchungu.
 • Hakikisha kuwa una zungumza na mtunzi wako wa afya katika mchakato huu wote – waambie mahitaji ya mkeo na hata hofu zake.
 • Kuwa kama “daraja’ kati ya bibi yako na daktari wake, kwa sababu kujifungua huenda kukamzidia. Jibu maswali yake kuhusu mchakato wa kujifungua na umwambie kinacho endelea mtoto wako anapo zaliwa.
 • Usisahau kujitunza, pia! Unaweza kuwa mwenzi bora zaidi wa kujifungua ukijitunza kwanza – kama vile, kula na kupumzika – pia.

 

Vyanzo: Medical Daily, University of ColoradoProceedings of the National Academy of Sciences (PNAS), National Hospital Services UK

SOMA HAYA PIA: Pooping During Labor And Delivery: 6 Tips For Avoiding It

Makala haya yaliandikwa na Bianchi Mendoza na kuchapishwa tena na idhini ya  theAsianparent kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio