Je, Kushiriki Kitanda Kimoja Ni Salama Kwa Watoto Wachanga?

Je, Kushiriki Kitanda Kimoja Ni Salama Kwa Watoto Wachanga?

The reasons behind bed-sharing with your baby are understandable. However, there are also risks associated with this practise that you need to know.

Wazazi wengi hulala pamajo kwa sababu tofauti.  Wengi hufanya hivyo kwa vile wanaamini humfanya mtoto kujihisi yuko salama. Ila wengine hufanya hivyo kwa vile inatosheleza. Ingawaje kulala pamoja ni jina linalotumika kumaanisha kushiriki kitanda kimoja na mtoto wako. Lakini hayo ni mambo mawili tofauti.

Kushiriki kitanda kimoja na mtoto ni nini haswa?

Je, Kushiriki Kitanda Kimoja Ni Salama Kwa Watoto Wachanga?

Kushiriki kitanda kimoja na kulala pamoja ni majina ambayo hutumika sawai. Kushiriki kitanda ni kulala pamoja na mtoto wako kwa kitanda kimoja ilihali kulala pamoja ni kushirki chumba kimoja cha malazi na mtoto wako. Ilhali huenda pia ikamaanisha kuwa kulala chumba kimoja kwa kitanda kimoja. Kwa hivyo kulala pamoja hutumika kuelezea yote. Pia kunazo njia mbili za kulala pamoja: kulala kwa kitanda kimoja au kulala kwa chumba kimoja.

Mazoea yote yameleta na huzidi  kuleta mgawamyiko katika pande zote mbili. Kwa hivyo inaweza kuwa ngumu  kuafikia ni mtindo upi sawa wa kulala na mtoto wako.

Je, ni salama kushiriki kitanda kimoja na mtoto wako?

usalama wa mtoto mchanga

Jibu sawa kwa hilo swali ni hapana. Sababu za wewe kushiriki kitanda kimoja na watoto wako zinaeleweka. Nani hangependa kushikama na kituta chake cha furaha? Kumhisi mtoto wako akipumua usiku wote? Pia kuna sababu zingine zisizo za kimawazo.  Wazazi huchoka sana mchana na hivyo kulala karibu na watoto wao hurahisisha mambo usiku. Sababu zingine ni kama vile:

 • Huweza kufanya kunyonyesha rahisi.
 • Watoto huweza kuamka mara nyingi wakati muda wao wa kunyonyeshwa ni mdogo. Hii inaweza ongeza masaa ya kulala. Kwa hivyo kuwa karibu na kuwanyonyesha wanapohitaji huwasaidia kulala vizuri.
 • Kulala kitanda kimoja na mtoto wako humsaidia mzazi kulala sawia na mtoto wake.
 • Inafanya kulala iwe rahisi wakati ana mzazi karibu naye.
 • Wazazi hufanya kazi mchana kwa hivyo kushiriki kitanda kimoja husaidia kurejesha mshikamano.

Ingawaje, inaonekana nzuri kulala na mtoto wako si jambo salama. Humweka mtoto wako kwenye hatari ya Kukosa pumzi ama kufa ghafla. Kushiriki kitanda kimoja ndio sababu kuu zaidi ya vifo vya watoto wa miezi matatu na kwenda chini.

Kufa hutokea kwa sababu hizi:

 • Ukosefu wa pumzi kutokana na godoro, mto au blanketi Kuwa laini humwezesha mtoto kupinda na Kukosa hewa.
 • Kukosa hewa kutokana na kukwama kati ya godoro na ukuta au chago.
 • Hewa kuwa chache kwa sababu ya kushikika katika eneo au kamba kwenye kitanda.

Vidokezo juu ya kushiriki kitanda na mwanao

 

Kuna hatari za kushiriki kitanda na mwanao. Kwa hivyo American academy of Pediatrics(AAP) hushauri dhidi ya kushiriki  kitanda kimoja. Lakini kama bado unataka kuendelea iwapo kuna hatari lazima uzingatie mawaidha haya.

 • Jiepushe na kushiriki kitanda kimoja na mtoto wa umri wa miaka chini ya miezi nne. Badala kihero na uweke kando ya kitanda chako.
 • Mvalishe mtoto nguo chache. Kumweke mtoto na nguo nyingi husababisha mtoto kuwa na joto nyingi.
 • Mlaze mtoto wako kwa mgongo kupunguza hatari ya kufa kwa Kukosa hewa.
 • Usimfunike mtoto kichwa anapolala.
 • Hakikisha kuwa mtoto halali peke yake kwa kitanda chako.
 • Usimlalishe mtoto mahali laini kama vile kwa godoro au juu ya sofa.
 • Hakikisha kuwa hakuna mwanya kwenyechago yako ambayo inaweza kufunga mtoto.
 • Jiepushe na kunywa vileo ambavyo vinaweza kufanya kumlalia mtoto.
 • Weka kitanda chako mbali na pazia na blind ambazo zinaweza kumshika mtoto
 • Chunga kulala kama umemshika mtoto.

Vidokezo vya kushiriki chumba na mwanao

kushiriki kitanda kimoja

Kushiriki chumba na mwanao ni tofauti na kushiriki kitanda. AAP hupendekeza kushiriki chumba kimoja na mwanao bila ya kushiriki kitanda kimoja. Kulala na mwanao katika chumba kimoja lakini mahali tofauti hupunguza hatari  ya kufa ghafla. Vidokezo vifuatavyo vitakusaidia kushiriki chumba kimoja na mtoto wako.

 • Kama mnavyoshiriki chumba kimoja haimaanishi kuwa huwezi kumtengenezea nursery mtoto wako. Unaweza tumia kizuizi kilicho na rangi sawai na chumba chako ili mtoto awe katika chumba kimoja lakini sio kitanda kimoja.
 • Hata kama mnashiriki chumba kimoja, mtoto bado ana pahala pake katika kila chumba. Jiepushe na kuleta kitanda cha mtoto karibu na chako ubaki kumwangalia mtoto kila sekunde chache.
 • Zulia nzuri husaidia kupunguza makelele yanayoweza kumwamsha mtoto.
 • Mnaposhiriki chumba kimoja, usisahau kuthibitisha desturi ya kulala.
 • Makelele nyeupu husaidia mtoto kulala. Kuna mashine nyingi za kutoa makelele nyeupe unaweza kununua. Pia fani inaweza kufanya kazi hii.

 

Mtoto anafaa kushiriki chumba kimoja nawe mpaka baada ya mwaka mmoja.  Baada ya hapo unaweza fikiria kumbadilishia chumba.

Read also: 10 Safe sleeping for newborns tips mummies must know

Reference: Kids Health

Written by

Risper Nyakio