Mambo ya kuvutia ambayo wanandoa wanaweza jaribu kitandani

Mambo ya kuvutia ambayo wanandoa wanaweza jaribu kitandani

Kufanya mapenzi ni muhimu kati ya wana ndoa. Kuna baadhi ya mambo ambayo wana ndoa wanaweza fanya kuyasisimua maisha yao ya kimapenzi. Kama vile kutumia vidoli vya mapenzi.

Kusisimua maisha ya mapenzi kati ya wanandoa ni jambo la busara. Iwapo umekuwa na mwenzi wako kwa wakati mwingi, kuna uwezekano kuwa maisha yenu ya kimapenzi haina ladha kama mlivyo kuwa mkianza safari yenu ya mapenzi. Kuna umuhimu kuongeza ladha katika maisha yenu ya kimapenzi. Ila unapo hisi kuwa maisha yenu yako sawa na kuna mambo ungependa kuongeza, kuna baadhi ya mambo ambayo unaweza kuongeza.

Wanandoa wengi baada ya kufunga pingu za maisha, wana sahau umuhimu wa kuwa na maisha mazuri ya kimapenzi. Wanalegea na kuyatupilia maisha haya. Wana pofanya mapenzi, hakuna ladha na kutamani mwingine kati yao. Huenda wakati mwingine wanafanya mapenzi juu wako pamoja na ni jambo linalo fanywa na wana ndoa. Ama wanapo kumbana na mambo magumu maishani, wana tumia ngono kama njia ya kuepuka mawazo na hisia hizo. Na wengine wanatupilia wazo la kufanya ngono kabisa katika ndoa hadi mmoja wao anapo mnasihi mwingine. Ni muhimu kwa wana ndoa kufanya mapenzi mara nyingi. Haya ni baadhi ya mambo ambayo wanaweza kufanya.

mapenzi kati ya wanandoa

Njia Za Kusisimua Maisha Ya Mapenzi

  • Kucheza na nguvu

Je, mnapo fanya mapenzi, nani anaye ongoza? Nani anaye anza kumvutia mwingine ili waanze tendo hili? Kuna ndoa ambazo mwanamke ndiye anaye anza na zingine mwanamme. Huenda ikawa, hamtaki hili libadilike. Ila ni muhimu kwa Nyinyi wote wawili kujaribu, mke anapo anza leo, mume ajaribu keshoye pia. Kwa anaye ongoza, jua mpenzi wako anacho taka. Kuna wanaume wanao pendelea kama wana wake wao ndiyo wana nguvu katika tendo hili. Na wengine wana wake wanao wapa nafasi ya kuongoza. Ni muhimu kujua matakwa ya mpenzi wako ili kusisimua maisha ya mapenzi yenu.

  • Mvutie mpenzi wako

Watu wanapo endelea kukua pamoja, kufanya mapenzi inakaa jambo la kawaida. Kwa upole, hamu ya kitendo hiki inadidimia. Ni muhimu kuirudisha. Jaribu mambo tofauti kitandani ili kuleta ladha kwa mapenzi yenu. Pia mnaweza jaribu mambo mapya kama vile kufanya mapenzi jikoni, kwa bafu ama pia sembuleni. Cha muhimu kabisa ni kuwa na mawasiliano mwafaka na mwenzio. Mweleze unacho taka ama kutamani mfanye. Iwapo pia kuna jambo unalo fanya na hafurahikii, pia ni muhimu kumweleza.

  • Tumia midoli ya ngono

Kuna aina nyingi ambazo wana ndoa wanaweza tumia kuongeza ladha wanapo fanya ngono. Kuna maduka tofauti ambazo wana uza vifaa hivi. Inasaidia kutoka kwa mapenzi ya kawaida na kuifanya ivutie na kutumia mbinu tofauti. Kwa njia hii, hamu ya kufanya mapenzi inaongezeka. Hata kama hamvitumii vifaa hivi kila siku, ni vyema kuvitumia mara kadha wa kadha.

 

  • Fanya mapenzi kwa kawaida

Watu husema kuwa kufanya mapenzi ni kama kufanya mazoezi. Unapo fanya mazoezi alafu uwache kwa muda mrefu inakuwa vigumu kuanza tena. Kufanya mapenzi ni vivyo hivyo, unapo kaa kwa muda bila kufanya tendo hili, inakuwa tatizo kujipa hamu. Kuna watu wanapo zeeka wana lipuuza jambo hili na kukosa kufanya mapenzi kwa hofu kuwa watakapo fanya mapenzi, hayatakua na ladha. Kwa wasi wasi huu wanaendelea kukosa kujiingiza katika tendo hili. Wana ndoa wana shauriwa kufanya tendo hili hata kama ni kwa wakati mchache lakini mara nyingi.

 

  • Kuwa mnyonge

Kuna wapenzi ambao wanapenda kuzingatia matakwa yao wakati wote. Jambo hili linaweza fanya mpenzi huyo mwingine akaboeka na kukosa hamu ya kufanya mapenzi kwani matakwa yake haizingatiwi. Ni muhimu mara kwa mara kuwa mnyonge na kumkubali mpenzi wako afanye linalo mfurahisha kwani kufanya mapenzi ni tendo la watu wawili na wote hawa wana paswa kuhisi kuwa mahitaji yao yame timizwa. Jambo hili linasaidia kusisimua maisha ya mapenzi.

 

  • Usijifanye kujua kila kitu

Unapo jifanya kuwa unajua mambo yote kitandani, mapenzi itakuwa ya kawaida. Hakutakuwa na mabadiliko yoyote kwani utaishi kurudia jambo ambalo umeishi kufanya. Unapo kubali kuwa haujui chochote, unafanya utafiti kuhusu mbinu mpya za kufanya ngono na unasoma mambo mapya. Kuna mbinu tofauti ambazo unaweza kutumia kujua mambo mapya kuhusu ngono. Kusoma vitabu, magazini ama pia kutumia mtandao. Geuza mbinu mlizo zoea na mtumie mpya ili kuongeza ladha kitandani mwenu.

 

  • Lala na nguo chache

Wana ndoa wengi wana uzoefu wa kulala na nguo nyingi wakati wa kitandani. Baada ya kuingia kitandani, wana lala bila ya kugusa wapenzi wao. Ni muhimu kwa wana ndoa kulala na nguo chache ama jinsi ulivyo zaliwa.

Ni jambo muhimu kwa wanandoa kuongeza ladha kwa maisha yao ya mapenzi. Kuna mbinu tofauti wanazoweza kutumia kama tulivyo angazia. Tumia njia tofauti na la muhimu zaidi ni kuwa na mawasiliano mema na mpenzi wako. Hakikisha mnaongea mnapo kuwa na wakati mchana, pia mtenge wakati wa kuwasiliana kila siku.

Read Also: 4 Sex positions with handcuffs for adventurous couples

 

Written by

Risper Nyakio