Kusoma Charti Za Ukuaji Wa Mtoto Vibaya Huenda Kukachangia Uzito Mwingi Kwa Mtoto

Kusoma Charti Za Ukuaji Wa Mtoto Vibaya Huenda Kukachangia Uzito Mwingi Kwa Mtoto

Umeambiwa kuwa lazima mtoto wako awe mnene. Kwa hivyo unamlazimisha kula chakula kingi na formula ili anenepe. Walakini, huenda ukawa unahatarisha maisha yake ni uzito mwingi.

Kwa watu wazima, kuongeza uzito sio jambo nzuri ila ni tofauti kwa watoto kwani ongezeko la uzito ni kipimo cha jinsi wanavyo kua. Mtoto anapo ongeza uzito, sifa zina ingia. Una pongezwa kwa jinsi unavyo fanya vyema katika nyanja ya ulezi, kumlisha mtoto vyema na yote yale yanayo andamana nayo. Baadhi ya watu wataenda umbali wa kukwambia usoni mwako kuwa wanapendelea watoto wanene zaidi. Kwa sababu hii na zingine, wazazi huwalazimisha watoto kula ili kufikisha malengo fulani ya uzito. Ila, kuwalisha zaidi husababisha uzito mwingi kwa watoto. Pia, wana tatizika na uzito mwingi maishani mwao wanapo kuwa wakubwa.

Mbali na kuwafanya wamama ambao watoto wao sio wakubwa kwenye kipimo kuonekana kana kwamba wamefeli, matokeo ni kuwa kupenda ongezeko la uzito na watoto wanene kunasukuma fikira kuwa ongezeko la uzito ni nzuri. Ila hiyo sio kesi. Ina hatari zake. Kwa zaidi ya mwongo mmoja, watafiti wamefahamu kuwa, kuwa mkubwa na kukua kwa kasi hufanya watoto wachanga kuwa katika hatari ya kuwa na uzito mwingi wanapokuwa wachanga, wakikomaa na wakiwa watu wazima. Usoni mwa ushuhuda huu, ni vyema kufahamu kuwa ujumbe haujakuweko kwa wataalum wa afya. Na ndiyo sababu wazazi wana shauriwa.

Kwa nini wazazi wengi wanakosea kusoma charti za ukuaji vizuri? 

overfeeding leads to childhood obesity

Huenda lika husishwa kwa wazazi wengi kushindwa kusoma charti za ukuaji vyema inavyo faa kulingana na mwongozo wa shirika la WHO. Charti ya WHO inaeleza jinsi ukuaji wa mtoto unapaswa kuwa kutoka kuzaliwa hadi akiwa na miaka mitano. Kwa hivyo, ukuaji wa mtoto unapaswa kufuata curve sawa na iliyo dhihirishwa kwenye charti iliyopatianwa.

Walakini, sio wazazi tu wanao paswa kutazamiwa juu. Inasemekana kuwa wazazi wengi wangefuata charti ikiwa walifahamu kuihusu. Lakini wengi wao hawafunzwi jinsi ya kusoma charti hiyo vizuri. Kinacho fanyika ni kuwa wazazi wanafikiria kuwa ufuatiliaji wa mtoto juu ya 50th percentile ni nzuri na chini yake ni mbaya. Lakini njia sawa ya kusoma charti ni kuwa nusu ya idadi yote inapaswa kuwa juu ya 50th na nusu hiyo ingine chini yake.

Nini kinacho tendeka mzazi anaposoma charti za ukuaji vibaya?

Matokeo ya kusoma vibaya ni kuwa wazazi kuteseka wakiwalisha watoto chakula kingi ili wawe zaidi ya asilimia 50. Na kuenda zaidi ya asilimia ya 50 kuna ashiria ukuaji wa kasi, kunako ongeza nafasi za mtoto kuwa na uzito mwingi wangali wachanga, wanapo komaa na wakiwa watu wazima.

Mfano mmoja wa hii ni wakati ambapo wamama huonekana kukosa maziwa ya mama tosha ya kuwalisha watoto wao. Wana shauriwa wachanganye na formula ya watoto wachanga. Lakini formula hii ya watoto tayari huongeza viwango vya protini, na kufanya mtoto apate uzito zaidi. Na tatizo hapa ni kuwa viwango vya juu vya protini katika miaka ya kwanza miwili ya maisha ya mtu husababisha ongezeko la kasi la uzito na matatizo ya uzito maishani mwake.

Nini Kinaweza Fanywa Kutatua Tatizo Hilo?

overfeeding leads to childhood obesity

Kulingana na wana sayansi wengi, matokeo yaliyo patikana kwenye utafiti hayaja chunguzwa kwa kina na kuwasilishwa kwa matumizi ya kila siku. Na iwapo matokeo haya yana patianwa, mambo yanapo badilika, hakuna njia sawa ya kuwajuza wataalum wa afya wanapo wasiliana na wamama kila siku.

Kilicho muhimu ni kuwa una mtoto aliye na afya. Kwani kuwalisha chakula kingi husababisha uzito mwingi kwa watoto, na kuwa tatizo kupunguza uzito wa mwili. Kwa kufahamu haya, wanasayansi wanahitaji kutafuta njia za kusema walicho kipata. Huenda ikahusisha masomo ya mtandao kuhusu lishe ya mtoto mchanga. Na kwa wazazi, mtoto anaposema kuwa watoto wao sio wanene vya kutosha, waulize vipimo walivyo tumia kufika kwenye tamatisho hilo.

Soma pia: Mbadala Bora Wa Maziwa Na Wenye Afya Kwa Watoto Wachanga

Written by

Risper Nyakio