Chanzo Cha Kusongwa Na Mawazo Baada Ya Kujifungua Na Suluhu Lake!

Chanzo Cha Kusongwa Na Mawazo Baada Ya Kujifungua Na Suluhu Lake!

Japo sio jambo linalo zungumziwa kwa sana, kusongwa na mawazo baada ya kujifungua ni tatizo sugu linalo waathiri wanawake wengi.

Japo sio jambo linalo zungumziwa kwa sana, kusongwa na mawazo baada ya kujifungua ni tatizo sugu linalo waathiri wanawake wengi na pia wanaume. Na hasa kwa wazazi wa mara ya kwanza. Ni muhimu kwa marafiki na jamaa kumsaidia mama na kuhakikisha kuwa ana mtu wa kuongea naye kupunguza hatari ya kuugua maradhi haya.

Dalili za kusongwa na mawazo

kusongwa na mawazo

Ishara maarufu za kuwa na mawazo mengi ni kama vile kukosa nishati ya utendaji kazi, kuhisi uchovu, kulia, mhemko wa hisia, kuto kula ama kutatizika kulala. Mara nyingi wiki za kwanza chache baada ya kujifungua. Kwa mama aliye athiriwa na mawazo mengi, huenda ukashuhudia kuwa ana huzuni, kukosa matumaini maishani ama kuonekana kuwa na mawazo mengi.

Chanzo cha maradhi haya

Hakuna chanzo hasa cha hali hii, ila mara nyingi:

  • Ikiwa mama alikuwa na mambo yaliyokuwa yakimtatizika katika ujauzito, huenda yaka zidi baada ya kujifungua. Ikiwa mama alikuwa ameugua maradhi haya hapo awali, ako katika hatari ya kuugua tena.
  • Kukosa watu wa kuegemeza baada ya kujifungua. Kujifungua ni jambo kubwa na mama anastahili kuwa na watu tosha wa kumsaidia.
  • Kukosa maziwa tosha ya mama. Na kusababisha kuwa na shaka kuhusu shibe ya mwanao.
  • Kukosa fedha za kukimu mahitaji yako.

kuchelewa kwa kipindi chako cha hedhi

Kutatua hali hii

  • Ni muhimu kwa mama kuwa na kundi la watu wanao msaidia na kazi za nyumbani na kumshauri jinsi ya kuishi maisha mapya na mtoto
  • Kutumia dawa za kutatua hali hii zinazo sawazisha homoni mwilini

Kumbuka kuwa hii ni hali ya kiafya sawa na magonjwa mengine na inaweza rekebishwa. Kwa hivyo usione haya kwenda hospitalini kupata matibabu.

Mbali na hayo, mama anastahili kufanya mazoezi mara kwa mara kwani ni muhimu sana katika kutuliza akili na mwili. Pumzika vya kutosha na uhakikishe kuwa unalala kwa angalau masaa manane kwa siku. Piga ngumzo na wanawake wengine, usikie wanacho pitia maishani na upate motisha kuwa siku moja shida zitapungua. Kula lishe yenye afya na ule mara zinazo faa kwa siku.

Ichunge afya yako vyema na ufanye mambo yanayo kupendeza mara kwa mara. Ikiwa una jambo linalo kusumbua, ni vyema kuzungumza na mtu unaye mwamini.

Soma pia:Tumbo La Mama Baada Ya Kujifungua Na Jinsi Ya Kulipunguza!

Written by

Risper Nyakio