Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Je, Ulifahamu? Kusukuma Katika Uchungu Wa Uzazi Kunaongeza Nafasi Za Uke Kuraruka Kwa Asilimia 700!

3 min read
Je, Ulifahamu? Kusukuma Katika Uchungu Wa Uzazi Kunaongeza Nafasi Za Uke Kuraruka Kwa Asilimia 700!Je, Ulifahamu? Kusukuma Katika Uchungu Wa Uzazi Kunaongeza Nafasi Za Uke Kuraruka Kwa Asilimia 700!

Tofauti na njia ya kuvuta mtoto atoke punde tu kichwa chake kinapo onekana, wakunga waliwakubalisha watoto kufuata njia asili ya kutoka katika mwendo wao.

Nafasi kubwa ni kuwa sote tumeona sehemu ya sinema ambapo mwanamke ameukunja uso wake huku akilia kwa uchungu anapo sukuma katika uchungu wa uzazi. Huku amezingirwa na watu wengi wanao mhamasisha asukume! Lakini, ulifahamu kuwa kusukuma kusiko faa katika uchungu wa uzazi kunaweza sababisha kuraruka? Naam, kuraruka kwa uke. Hii ndiyo sababu kwa nini ni muhimu kujifunza jinsi ya kusukuma katika uchungu wa uzazi bila kuraruka.

Kwa nini unapaswa kufahamu jinsi ya kusukuma katika uchungu wa uzazi bila kuraruka

kusukuma bila kuraruka katika uchungu wa uzazi

Tisa kati ya wanawake kumi huumia kutokana na aina ya kuraruka kwa uke katika kujifungua kwa kawaida. Uharibifu hutofautiana kwa sana. Lakini katika kesi sugu, wanawake wanaweza baki wakitatizika na kuto dhibiti mkojo na matatizo ya muda mrefu ya neva.

Kati ya mwaka wa 2013 na 2014, kulikuwa na ongezeko kuu la nambari ya wanawake huko England walio tatizika na kuraruka kwa perineal. Perineum ni sehemu ya ngozi kati ya uke na sehemu ya nyuma.

Ili kupunguza nambari hii, madaktari wali washauri wamama wasi sukume katika uchungu wa uzazi. Kisha waka wahamasisha kujifungua wakiwa wame chuchumaa ama kusimama. Kama ilivyo kuwa miaka ya hapo kale hadi miaka ya 1950s.

Wakunga waliwashauri wamama kupumua kwa njia ya kawaida kama njia ya kusukuma katika uchungu wa uzazi bila kuraruka.

Tofauti na njia ya kuvuta mtoto atoke punde tu kichwa chake kinapo onekana, wakunga waliwakubalisha watoto kufuata njia asili ya kutoka katika mwendo wao. Waliegemeza uzito wa mtoto kupunguza shinikizo kwenye perineum.

Bila shaka programu hii ilikuwa na mafanikio makubwa. Na matokeo yake yalichapishwa kwenye Makala ya European Obstetrics na Gynaecology. Kuna mipango ya kuanzisha mambo haya nchini kote.

Jinsi ya kusukuma katika uchungu wa uzazi bila kuraruka? Kusukuma ama kuto sukuma..

what not to do after c-section

Katika makala yake, Kusukuma ama Kuto sukuma, Mickey Morgan, ambaye ni mwanzilishaji wa HypnoBirthing, alisema kuwa kusukuma katika uchungu wa uzazi kuna punguza juhudi.

"Kusukuma kwa lazima kuna anzisha shinikizo kwa mama anaye jifungua, na kushinda juhudi wanazo fanya.

Karibu miaka 25 iliyo pita, Morgan alianzisha jambo la kupumua kunako anzishwa na mama, badala ya kuagizwa na wauguzi.

Kusukuma kwa kulazimishwa kunasababisha:

  • Uchovu kwa mama anaye shuhudia uchungu wa uzazi
  • Kubanwa kusiko tosha wakati wa kusukuma
  • Hatari iliyo ongezeka ya hypoxia(mwili kukosa hewa ya kutosha)
  • Matatizo ya mtima wa mtoto
  • Kuharibika kwa misuli ya pelvisi ya mama
  • Kuharibu misuli ya damu ya macho na uso
  • Kurarua perineum
  • Hatari iliyo ongezeka ya episiotomy (kukatwa kwa mlango wa uke)

Mapato ya somo hili haya kushtua wakunga na wataalum wa afya ya uke. Lakini, ni habari nzuri kwa wanawake kila mahali kuwa mbinu hizi zina fahamika kirasmi zinavyo paswa. Kusukuma katika uchungu wa uzazi kunaweza kuwa na athari hasi na kuna njia salama kwa wanawake kupitia hatua ya uchungu wa uzazi.

Ni vyema kufahamu mambo haya kwa wamama wa mara ya kwanza wanao ingia chumba cha uchungu wa uzazi bila kufahamu cha kutarajia.

Vyanzo: Cochrane library

Soma Pia: Wakunga Hawa Wanafukuza Uwoga Wako Wa Kujifungua: Waamini

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Becoming a Mama
  • /
  • Je, Ulifahamu? Kusukuma Katika Uchungu Wa Uzazi Kunaongeza Nafasi Za Uke Kuraruka Kwa Asilimia 700!
Share:
  • Kunya Katika Uchungu Wa Uzazi Na Kujifungua: Vidokezo 6 Vya Kuepuka Jambo Hili

    Kunya Katika Uchungu Wa Uzazi Na Kujifungua: Vidokezo 6 Vya Kuepuka Jambo Hili

  • Je, Ulijua Kuwa Kusukuma Wakati Wa Uchungu Wa Mama Husababisha Kuraruka Kwa Uke?

    Je, Ulijua Kuwa Kusukuma Wakati Wa Uchungu Wa Mama Husababisha Kuraruka Kwa Uke?

  • Ishara Za Uchungu Wa Uzazi: Jinsi Ya Kujua Kuwa Mtoto Ako Njiani

    Ishara Za Uchungu Wa Uzazi: Jinsi Ya Kujua Kuwa Mtoto Ako Njiani

  • Mbinu 5 Salama Za Kuanzisha Uchungu Wa Uzazi

    Mbinu 5 Salama Za Kuanzisha Uchungu Wa Uzazi

  • Kunya Katika Uchungu Wa Uzazi Na Kujifungua: Vidokezo 6 Vya Kuepuka Jambo Hili

    Kunya Katika Uchungu Wa Uzazi Na Kujifungua: Vidokezo 6 Vya Kuepuka Jambo Hili

  • Je, Ulijua Kuwa Kusukuma Wakati Wa Uchungu Wa Mama Husababisha Kuraruka Kwa Uke?

    Je, Ulijua Kuwa Kusukuma Wakati Wa Uchungu Wa Mama Husababisha Kuraruka Kwa Uke?

  • Ishara Za Uchungu Wa Uzazi: Jinsi Ya Kujua Kuwa Mtoto Ako Njiani

    Ishara Za Uchungu Wa Uzazi: Jinsi Ya Kujua Kuwa Mtoto Ako Njiani

  • Mbinu 5 Salama Za Kuanzisha Uchungu Wa Uzazi

    Mbinu 5 Salama Za Kuanzisha Uchungu Wa Uzazi

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it