Je, Ulijua Kuwa Kusukuma Wakati Wa Uchungu Wa Mama Husababisha Kuraruka Kwa Uke?

Je, Ulijua Kuwa Kusukuma Wakati Wa Uchungu Wa Mama Husababisha Kuraruka Kwa Uke?

Soma ujue kinacho tendeka wakati wa kujifungua.

Sisi sote tume angalia sinema ama vipindi ambapo sura ya mwanamke inakunjika kwa uchungu akisukuma mtoto wakati wa uchungu wa uzazi huku akizingirwa na kiitikio cha 'sukuma, sukuma sukuma! Ila, ulijua kuwa kusukuma huku kusiko faa wakati wa uchungu wa uzazi huenda kukasababisha kukatika? Ndio, na kwa macho yako pia. Ila, hasa tunaongelelea kuharibika kwa uke wako. Hii ndiyo sababu ni muhimu kusoma jinsi ya kusukuma wakati wa uchungu wa uzazi bila kuraruka.

Kwa Nini Unapaswa Kujua Jinsi Ya Kusukuma Wakati Wa Uchungu Wa Uzazi Bila Kuraruka

how to push during labor without tearing

Tisa kati ya kila wanawake 10 wanateseka kutokana na baadhi ya aina ya kuraruka kwa uke wakati wa kujifungua kwa kawaida. Uharibifu huu hutofautiana kwa kiasi kikuu. Ila, katika visa vilivyo zidi zaidi, wanawake huenda wakabaki wakiteseka kutokana na matatizo ya neva ya muda mrefu ama maishani yao yote.

Kati ya mwaka wa 2013 na 2014, kulikuwa na ongezeko la idadi ya nambari ya wanawake huko Uingereza walio teseka kufuatia kuraruka kwa aina hii. Perineum ambayo ni sehemu ya ngozi na tishu kati ya uke na sehemu ya kupitisha haja. Huku kulifanya Chuo Kikuu cha Royal cha Wakunga kuchukua aina ya hatua.

Na msaadanwa Royal College of Obstetricians and Gynecologists, walifanya programu ya majaribio katika Medway Maritime Hospital huko Kent.

Wakati wa majaribio haya, kusukuma kwa kawaida katika uchungu wa uzazi hakukushauriwa. Mabadiliko machache kama kuto washinikiza wanawake kulala kwa migongo yao na kusukuma kulisaidia pakubwa. Kwa ujumla, jinsi ya kusukuma wakati wa uchungu wa uzazi bila ya kuraruka kulikua na maana ya kupunguza kuraruka.

Hospitali ilipunguza idadi ya digri ya shahada ya tatu na ya nne ya kuvunjika kwa sehemu ya perineal mara saba kutoka kwa asilimia 7 hadi 1.

Mkuu wa ukunga wa hospitali, Dot Smith alihusisha kiwango cha kuongezeka kwa idadi ya wanawake wanao shuhudia kuraruka kwa uke na imani zisizo za kweli kuwa wanawake wana hitaji la "kusukuma, sukuma na kusukuma" zaidi katika uchungu wa uzazi.

"Tulipo ona visa 22 vya kuraruka kwa shahada ya tatu katika mwezi mmoja, tulisema, hii sio njema kiasi tosha," Smith alisema.

Wakati wa programu hii ya majaribio, hospitali pia ilihimiza wanawake wajifungue wakiwa wamesimama ama kuchuchumaa kwenye magoti yao. Hii ni kawaida na kufanywa sana katika kipindi cha miaka ya 1950.

Wakunga pia walihimiza kupumua kwa kawaida kama njia ya kubanwa kama njia ya kusukuma wakati wa uchungu wa uzazi bila kuraruka.

how to push during laboor without tearing

Kwa kuongeza, mbadala ya njia ya kawaida ya kuvuta watoto punde tu kichwa chao kinapo tokea ama kuonekana, wakunga walikubalisha watoto kufuata njia asili ya mwito wa kujifungua na kutoka pole pole kwa mwendo wao. Wali egemeza uzito wa mtoto ili kupunguza shinikizo kwenye perineum.

Kama vile utakavyo dhani, programu hii iliwapendeza wengi. Ili kuwa yenye mafanikio kiasi kwamba mapato yake yalichapishwa kwenye Makala ya European Journal of Obstetrics and Gynaecology. Pia kuna mipango ya kufanya vitu vilivyo chapishwa katika taifa lote.

 Kipimo kidogo kimefanya athari kubwa sana katika kupunguza hatari zisizo kusudiwa kwenye mili ya wanawake katika uchungu wa uzazi kwa asilimia 85 katika baadhi ya vyumba vya kujifungua.

Jinsi ya kusukuma wakati wa uchungu wa uzazi bila kuraruka? Kusukuma ama kutosukuma...

woman in labour

Katika makala yake ya Kusukuma ama Kuto Sukuma, Mickey Morgan, mwanzilishaji wa HypnoBirthing, asema kwamba kusukuma wakati wa uchungu wa uzazi kuna enda mrama na matarajio.

"Kusukuma kwa kulazimisha kulitengeneza fikira nyingi kwa mama anaye jifungua, jambo ambalo linajishinda kwa huku, kufunga sphincters za uke mbele ya mtoto anaye karibia kutoka."

Karibia miaka 25 iliyo pita, Morgan ali anzisha jambo la kupumua kunako ongozwa na mama, mbadala ya kupumua kunako ongozwa na wafanya kazi.

Amepata ushuhuda tosha kuwa kusukuma kuliko elekezwa ama kulazimishwa:

  • Uchovu wa mama katika uchungu wa uzazi
  • Kuongezeka kwa vifo vya mama na mtoto
  • Kubanwa kusiko tosha kwa uterasi
  • Hatari zilizo ongezeka za hypoxia (kukosesha hewa tosha kuto ingia)
  • Matatizo ya mpigo wa moyo wa kiinitete
  • Kuharibu misuli ya sakafu ya pelviki ya mama
  • Kuharibika kwa vessels za macho na za damu ya uso
  • Kuraruka kwa perineum
  • Kuongezeka kwa kuhitaji episiotomy (surgical cut katika mlango wa uke)

Matokeo ya somo hili yanashtua wakunga na wataalum wa afya ya wanawake. Ila, ni habari kuu kwa wanawake kila mahali na njia hizi zinapata kujulikana kwa kirasmi. Kusukuma wakati wa uchungu wa mama huenda kukawa kuharibifu na kuna njia zilizo salama zaidi kwa wanawake wakati wa uchungu wa uzazi.

Ni vyema kuwa na maarifa kuhusu vitu kama hivi kwa wamama wengi wanao jifungua ama kutayarisha kuenda chumba cha kujifungua bila kujua cha kutayarisha. Weka haya akilini siku yako kuu ikifika!

Kumbukumbu: Cochrane Library

Written by Nasreen Majid and republished with permission from theAsianparent and

Soma pia: Causes And Treatment Of Childbirth Tears

Makala haya yalichapishwa kwa mara ya kwanza kwenye kurasa ya Nasreen Majid kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio