Kutapika Katika Mimba Ni Ishara Kuwa Huenda Mtoto Wako Akawa Mwenye Maarifa

Kutapika Katika Mimba Ni Ishara Kuwa Huenda Mtoto Wako Akawa Mwenye Maarifa

Kutapika katika mimba hakuna athari hasi kwa mtoto, mbali kunamsaidia kuwa na ushupavu zaidi ikilinganishwa na wanarika wake.

Inaonekana kama wana sayansi wamepata baadhi ya faida za watu wanao tatizika na kichefu chefu na kutapika katika mimba. Na unajua wanavyo sema, "kukosa uchungu, kukosa mafanikio."

Kutapika katika mimba: Wanasayansi wanagundua kuwa wamama wanao tatizika na magonjwa ya ujauzito huenda wakawa na watoto wenye maarifa

Signs of high IQ

Utafiti umegundua kuwa ukitatizika na magonjwa ya ujauzito, huenda ukawa na mtoto aliye na maarifa (IQ) ikilinganishwa na wenzake. IQ (intelligent quotient) ni njia ya kupima maarifa katika watu. Huku kuna maana kuwa mtoto wako atakuwa shupavu akilinganishwa na watoto wengine wa umri wake. Mara nyingi, wamama wengi huwa na shaka kuwa ugonjwa wa asubuhi una athiri kiwango cha virutubisho kinacho mfikia mtoto. Na kuwa na shaka kuwa huku kuna athiri ukuaji wa mtoto. Watafiti katika hospitali ya Watoto Wagonjwa Toronto huko Canada walipata kuwa badala ya kuathiri mtoto kwa njia hasi, ugonjwa wako wa asubuhi na kutapika kuna ongezea ushupavu wa mtoto.

Kwa utafiti huo, wana sayansi wali chunguza watoto 121. Watoto hawa walikuwa kati ya umri wa miaka 3 na 7. Mama zao wali hangaika na ugonjwa wa asubuhi na kutapika katika mimba. Badala ya kubaki nyuma kama mama wengi wanavyo ogopa, iligunduliwa kuwa watoto hawa wangefuzu zaidi katika majaribio ya IQ, kukumbuka na lugha. Mtafiti mkuu, daktari Irena Nulman aliiambia Reuters Health kuwa matokeo yali pendekeza kuwa kichefu chefu na kutapika katika ujauzito sio hatari na huenda kukawa na athari chanya katika ukuaji wa kiakili wa mtoto.

Walakini, haija julikana chanzo cha kichefu chefu na kutapika kwa wanawake wenye mimba ni nini hasa. Lakini ni kawaida sana kwa wamama wanao tarajia, hasa katika trimesta ya kwanza. Ime husishwa na homoni zinazo husika na ukuaji wa mtoto. Walakini, vyanzo bado havija dhibitika.

Jinsi ya kupunguza kichefu chefu katika mimba

Vidokezo hivi vitakusaidia kupunguza hisia za kutapika na ugonjwa wa asubuhi katika ujauzito.

  • Kula vyakula vinavyo shibisha

kutapika katika mimba

Kichefu chefu huwa kibaya zaidi unapo kuwa na njaa. Utahisi kana kwamba utatapika viungo vyako vya ndani. Kuepuka haya, kula vyakula vinavyo kaa kwa mwili kwa muda. Hizi ni kama vile maharagwe, samaki, nyama, parachichi na maziwa ya bururu.

  • Mazoezi

kujitayarisha kuwa mama, mimba, mazoezi

Kufanya mazoezi kutakusaidia kupigana dhidi ya ugonjwa wa asubuhi na hisia ya kutaka kutapika. Tembea asubuhi ama jioni. Kupata hewa ni muhimu sana katika kipindi hiki.

  • Tangawizi

Kula tangawizi ni njia ya kupunguza ugonjwa wa asubuhi na kichefu chefu. Pia ni rahisi kupata na kutengeneza. Toa ngozi yake, safisha vyema kisha ukate na uongeze kwenye maji yanayo chemka. Ipe muda kisha utoe motoni na unywe. Hakikisha kuwa yamepoa kidogo.

  • Kuwa na vitamu tamu karibu

Ni muhimu hasa kwa sababu baadhi ya wakati, kichefu chefu huenda kikaja ukiwa mbali na nyumba na hauna chakula karibu nawe. Kuhisi kutapika ni hisia mbaya zaidi ukiwa njaa. Kwa hivyo, kuwa na vitamu tamu karibu ni muhimu sana. Kuepuka hisia ya kutapika, beba baadhi ya vitamu tamu kwenye mkoba wako, gari na kando ya kitanda chako.

  • Oga kwa maji baridi

Kuoga kwa maji baridi kunaweza punguza kichefu chefu. Kwa hivyo unapo hisi kutapika, jaribu kukoga kwa maji baridi. Sio lazima iwe ni kukoga mwili wote. Unaweza weka kichwa chako kwenye mfereji wenye maji baridi, kisha ungoje maji hayo yakuoshe kwa dakika chache.

  • Mafuta ya peppermint

Harufu kali ya mafuta haya inaweza punguza kichefu chefu. Kiwango kidogo cha mafuta haya kwenye kitambaa chako kitakusaidia sana. Weka kitambaa hicho kwenye mkoba wako kwa wakati wowote unapo hisi kutapika. Chukua kitambaa hicho kisha unuse mafuta hayo.

Kuwa na uhakika kuwa, kutapika katika mimba hakuta athiri fizikia ya mtoto wako. Mbali na kutokuwa na starehe, utahisi kuumwa na misuli ya tumbo. Lakini kutapika kukizidi kwa muda mrefu, hakikisha umemwona daktari.

Soma Pia:Vitamu Tamu Vitano Wakati Wa Ujauzito

Written by

Risper Nyakio