Kutatizika kulala katika mimba husababishwa hasa na fetusi inayo zidi kukua kwenye uterasi ya mama. Na kuifanya iwe vigumu kwake kulala kama alivyo kuwa amezoea hapo awali. Hasa kwa wanawake walio kuwa wamezoea kulala kwa tumbo ama mgongo kabla ya kutunga mimba. Kuanza kuzoea kulala kwa upande mmoja sio rahisi, ila hawana budi. Pia, hawana uhuru wa kujipindua wanavyo taka wakiwa na mimba.
Sababu Zinazo Athiri Uwezo Wa Kulala Vyema Katika Mimba

Kiwango cha damu kinacho tolewa mwilini huongezeka mama anapo kuwa na mimba. Ili kutosheleza mahitaji ya damu ya mama na mtoto. Kwa sababu hii, moyo utapiga kwa kasi zaidi ili ku pumpu damu zaidi, ya wote mama na mtoto. Inafanya iwe vigumu kwa mama kulala kwa starehe na urahisi alivyo kuwa amezoea hapo awali.
- Kuumwa na mgongo na miguu
Ongezeko la uzito wa mwili na uterasi inayo zidi kukua, hushunikiza miguu. Na kufanya iwe vigumu kwa mama kutembea ama kusimama kwa muda mrefu. Uzito kwenye uterasi pia unafanya mgongo wa mama kuuma anapo jilaza. Yote haya yana mtatiza mwanamke mjamzito kulala vyema.
- Kiungulia na ukosefu wa maji mwilini
Kiungulia na kukosa maji tosha ni tatizo ambalo wanawake wengi hukumbana nalo katika mimba. Mama mjamzito huchukua tembe za vitamini za kabla ya kujifungua ili kuboresha viwango vya virutubisho anavyo pata. Tembe hizi mara nyingi husababisha tatizo la ukosefu wa maji tosha mwilini.
Ongezeko la homoni mwilini kufuatia ujauzito hufanya iwe vigumu kwa mwanamke kupumua kwa kawaida. Anapumua kwa nguvu zaidi. Uterasi inayo zidi kukua inachukua nafasi zaidi na kushinikiza mafua. Na kufanya kupumua kuwe na shida zaidi.
- Hisia ya kwenda haja ndogo wakati wote
Mwanamke anapo kuwa na mimba huwa na hisia ya kwenda haja ndogo kila mara. Japo mimba inavyo zidi kukua, ina shinikiza kibofu chake zaidi na kumfanya ahisi haja ya kwenda msalani kila wakati, mchana na usiku. Wanawake wengi huhisi haja ya kwenda msalani wakati wa usiku. Kwa imani kuwa mtoto ako hai zaidi katika kipindi hicho. Ni vigumu kwa mama kulala kwa starehe anapo hisi haja ya kwenda msalani baada ya kila lisaa limoja.
Vidokezo vya kusuluhisha kutatizika kulala katika mimba

Mama anaweza:
- Kutumia mto wa kulala na kuuweka kati kati ya miguu yake anapo lala
- Kupunguza unywaji wa soda, kaffeini na chai anapo karibia kulala
- Kupunguza kiwango cha chakula anacho kula chajio. Kula masaa manne kabla ya kulala
- Kuzungumza na wanawake walio jifungua ili wampe mawaidha na kupunguza woga wa kujifungua
- Punguza kufanya mazoezi magumu katika mimba. Fanya mazoezi mepesi na kuwasiliana na mtaalum wa mazoezi
Chanzo: Healthline
Soma Pia:Chakula Cha Mama Mjamzito: Je, Mjamzito Anapaswa Kula Nini?