Kutatizika kupunguza uzito kunakusumbua, licha ya kufanya mazoezi kila siku ya wiki? Kipi kinachosababisha kukosa kupunguza uzito wa mwili?
Vyanzo vya Kutatizika Kupunguza Uzito wa Mwili
- Chakula

Chakula unachokila huchangia pakubwa katika kupunguza ama kuongeza uzito licha ya kufanya mazoezi. Ikiwa unakula chakula kisicho na afya, haijalishi masaa unayofanya mazoezi kwa siku. Ukweli ni kuwa, hautaona tofauti yoyote kwenye inchi za kiuno. Huenda zikaongeza hata.
Ikiwa lengo lako ni kupunguza uzito, lazima uangazie kalori unazotia mwilini. Punguza kiwango cha kalori unachokila. Zingatia kula kiwango kidogo cha kalori ikilinganishwa na nishati unayotumia kila siku. Pia, hakikisha kuwa unakula tu unapohisi njaa.
Jitenge na ulaji wa vitamu tamu vilivyo chakatwa, badala yake, kula njugu. Punguza ulaji wa vitu vilivyokaangwa kwa ufuta mwingi kama vile vibanzi.
2. Mtindo wako wa maisha

Kupunguza uzito wa mwili huwa juhudi za vitu vingi tofauti. Kufanya mazoezi na kuwa na mtindo duni wa maisha hakutakuwa na faida zozote. Mtindo wa maisha huchangia pakubwa katika kupunguza ama kuongeza uzito licha ya kufanya mazoezi magumu kila siku. Kutopata usingizi tosha kwa siku na kusombwa na mawazo husababisha kutopunguza uzito. Unaposombwa na mawazo, huenda ukatamani kula chakula kisicho na afya ili kujituliza. Unywaji wa pombe ili kupunguza fikira nyingi pia kutapunguza juhudi zako za kupunguza uzito.
3. Mazoezi

Ikiwa unafanya mazoezi na huoni mabadiliko yoyote, angalia mazoezi unayo yafanya. Usifanye cardio na kukimbia peke yake, hakikisha kuwa unainua chuma ama uzito pia.
4. Maumbile na jeni
Ikiwa umezaliwa katika familia ambapo kuna watu wanene. Huenda ikakuchukua muda zaidi ikilinganishwa na watu wengine kupunguza uziyo. Usikate tamaa na kutupilia mbali ufanyaji wa mazoezi. Badala yake, zidisha juhudi zako na uwe mtulivu.
5. Homoni

Homoni huashiria akili kupunguza uzito. Ikiwa homoni za cortisol na thyroid hazifanya kazi ipasavyo, kupunguza uzito wa mwili kutakutatiza. Kuwa na hali za kiafya kama uzito zaidi, shinikizo la juu la damu na kisukari hutatiza upunguzaji wa kilo mwilini.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Jinsi Ya Kupunguza Uzito Wa Mwili Kwa Kutumia Lishe Ya Alkaline