Kutayarisha Lishe Kwa Ajili Ya Covid-19 Ambazo Zitakaa Kwa Muda Mrefu

Kutayarisha Lishe Kwa Ajili Ya Covid-19 Ambazo Zitakaa Kwa Muda Mrefu

Jangala covid 19 maarufu kama homa ya korona lime athiri nyingi duniani kote. Katika nchi zingine kama Uchina, Umarekani na Uitaliano, wamefunga mahali kwingi na kuwaagiza wakae nyumbani mwao bila kutoka nje. Unahitaji kibali ili utoke nje kuenda dukani kununua vyakula. Kwa kuwa virusi hivi vimefika nchini Kenya, ni vyema zaidi kwa wananchi kuwa tayari na kujua chakula kilicho sawa cha kuweka wakati huu wa janga hili. Tunaangazia kutayarisha lishe kwa ajili ya covid-19.

Orodha muhimu ya kuangazia ya kutayarisha lishe kwa ajili ya Covid-19

 • Githeri

Viungo

 • 400 g mahindi yaliyo chemshwa
 • 600 g maharagwe yaliyo chemshwa
 • 2 nyanya za wastani
 • 1 kitunguu
 • 3 vitunguu saumu
 • 2 tangawizi
 • ½ pilipili
 • 1 kijiko cha mafuta ya kupika
 • 1 kijiko kidogo cha chumvi
 • Dhania
 • Hoho nyekundu

Maagizo

 1. Ipashe sufuria yako joto kwa moto wa kiwango cha wastani kisha uongeze mafuta, ongeza kitunguu chako. Kipe wakati kiive hadi kinapo geuka kuwa rangi ya hudhurungi.
 2. Ongeza kitunguu saumu na tangawizi zipike kwa angalau dakika moja. Ni muhimu ili kuongeza ladha kwa chakula chako.
 3. Ongeza nyanya zako kisha upunguze moto kuzipatia wakati ziive vizuri. Zipike kwa angalau dakika 5 ama hadi mchanganyiko huu unapo punguka na kuwa mnene.
 4. Ongeza karoti na kitunguu cha chemchemi kisha ufunike kwa angalau dakika moja kabla ya kuongeza mahindi na maharagwe.
 5. Ongeza chumvi na pilipili iliyo katakatwa.
 6. Zifunike ziive kwa angalau dakika 10 ili ziwe nene na zipate ladha.
 7. Hatimaye, ongeza dhania na hoho nyekundu ziive kwa dakika moja kisa uzime moto wako.

Kitu cha kupendeza zaidi na chakula hiki ni kuwa unaweza kitayarisha kwa njia tofauti. Kama vile kupika kwa nyama, kabichi, sukuma wiki, viazi na vinginevyo.

Ukiwa na githeri kwa nyumba yako, bila shaka hauna wasiwasi kwa siku kadhaa kwani kinaweza kusukuma kwa angalau dakika 3. Pia ni vigumu chakula hiki kuharibika, hakikisha tu umekiweka kinavyo stahili.

Kutayarisha Lishe Kwa Ajili Ya Covid-19 Ambazo Zitakaa Kwa Muda Mrefu

 • Maharagwe

Kuna njia nyingi za kutayarisha maharagwe. Ukiwa na maharagwe nyumbani mwako, una mchuzi tosha, kazi ambayo utakuwa nayo ni kutafuta kitu cha kuula mchuzi huo.  Maharagwe haya haribiki kwa urahisi.

Njia iliyo kawaida kabisa ya kutayarisha maharagwe ni maharagwe ya nazi. Mtindo huu uliibuka upande wa pwani ambako chakula hiki kinasifika sana na bila shaka ni kitamu kupindukia.

Viungo

 • 2 bakuli za maharagwe nyekundu
 • Maziwa ya nazi iliyo nyembamba
 • 1 kitunguu
 • 2 pilipili
 • Chumvi
 • ¾ vikombe vya maziwa ya nazi iliyo nene
 • 1 kijiko cha unga
 • Poda ya turmeric

Maagizo:

 1. Safisha maharagwe yako kishe uweke kwenye chungu.
 2. Kata kitunguu chako kwa sehemu ndogo na uongeze maharagwe na pilipili, poda ya turmeric na chumvi.
 3. Ongeza kiwango tosha cha maziwa ya nazi iliyo nyembamba kisha ufunike maharagwe yako yaanze kuiva.
 4. Pika maharagwe yako hadi wakati ambapo kiwango cha maziwa kita punguka na maharagwe imepikika vyema.
 5. Kwa chungu ama sufuria nyingine, ongeza maziwa ya nazi iliyo nene, ongeza unga na uanze kupika hadi inapokuwa nene zaidi.
 6. Mwaga maharagwe iliyo pikwa kwenye bakuli kisha uongeze ile maziwa ya nazi juu ya maharagwe haya.

Kula kwa wali ama chapati. Pika maharagwe yako njia tofauti kila siku kuepuka kuboeka na chakula chako.

Kutayarisha Lishe Kwa Ajili Ya Covid-19 Ambazo Zitakaa Kwa Muda Mrefu

 • Wali

Hata ingawa chakula hiki kimekuwa kikipikwa kwa wakati mwingi tangu miaka ya jadi, baadhi ya watu hutatizika kukitayarisha.  Ukiwa na wali nyumbani mwako, huenda ukala kwa siku angalau mbili.

Tunaangazia jinsi ya kutayarisha wali wako.

Viungo

 • 1 ½ kikombe cha mchele
 • 3 Vikombe vya maji
 • Chumvi

Maagizo

 1. Safisha mchele wako kwa maji ya mfereji hadi maji inapokuwa safi. Kisha uwache mchele wako kwa maji kwa dakika 20.
 2. Ongeza mchele wako kwenye chungu kisha uongeze vikombe 3 vya maji na chumvi. Chemsha kisha upunguze moto, kifunike chungu chako kwa dakika 12-14.
 3. Zima moto. Tayari chako ki tayari.

Unaweza tumia mchuzi ya nyama ya ng’ombe, kuku, mbuzi ama maharagwe ya nazi.

Kutayarisha Lishe Kwa Ajili Ya Covid-19 Ambazo Zitakaa Kwa Muda Mrefu

 • Mukimo

Hapo awali, chakula hiki kilikuwa maarufu sana katika familia ya Agikuyu, ila, siku hizi chakula hiki kinapikwa pande zote nchini Kenya.  Wakati wa jadi, chakula hiki kilipikwa na kukaa kwa siku nyingi, ambapo kingeliwa kama chamcha, chajio na kiamsha kinywa na chai.

Viungo

 • 1 kilo ya viazi
 • 2 vitita vya mboga za malenge laini
 • 3 vikombe vya mahindi laini
 • 1 kitita cha vitunguu chemchemi
 • 1 kijiko cha mafuta ya kupika
 • 1 kijiko kidogo cha chumvi

Maagizo

 1. Toa ngozi ya viazi vyako kisha uvikate viwe vidogo. Vioshe na uviweke kando.
 2. Tayarisha mboga za malenge kwa kuosha na kukatakata.
 3. Changanya mboga hizi na mahindi na viazi kwenye sufuria kisha uongeze maji kiasi kidogo ili viungo hivi viive.
 4. Wekelea chungu chako kwenye moto na ukipe wakati kichemke kwa dakika 30 kwa moto wa wastani. Ongeza chumvi ziendelee kuiva kwa dakika 10.
 5. Punguza moto kisha kwa kutumia mwiko, uchanganye viungo hivi hadi viwe sawa. Toa chungu chako motoni.
 6. Kwa chungu tofauti, mwaga kitunguu chako cha chemichem, ongeza mafuta ya kupika kisha uwekelee motoni. Changanya hadi viwe rangi ya dhahabu kisha upunguze moto hadi wa wastani na uongeze viungo vya chungu ulicho weka kando. Changanya kabisa.
 7. Chakula chako cha mukimo ki tayari- toa motoni.

Kula kwa mchuzi wa nyama ama maharagwe ya nazi.

kutayarisha lishe kwa ajili ya covid-19

 • Chapati

Viungo

 • 1 kilo ya unga ngano
 • Mafuta ya kupika
 • 4 vijiko vya sukari
 • 1 kijiko cha chumvi

Maagizo

 1. Changanya unga wako na mafuta ya kupika kwenye bakuli kubwa.
 2. Ongeza maji kidogo kidogo ukiendelea kuchanganya hadi uwe laini.
 3. Funika kwa dakika angalau dakika 30.
 4. Roll mchanganyiko huu kwa kutumia pini ya kusonga (rolling pin) kisha upake mafuta.
 5. Kata kwa viwango vidogo ambazo utatumia kutengeneza mpira.
 6. Kwa kutumia pini ya kusonga, tengeneza mpira wako uwe miundo ya kupendeza ya duara.
 7. Pasha joto sufuria yako ya kukaangaka na uweke moto wa wastani.
 8. Ongeza kiwango kidogo cha mafuta wa kupika na uwekelee unga uliofanywa kuwa duara.
 9. Geuza upande huo mwingine hadi pande zote mbili ziwe za hudhurungi ya dhahabu.

Kula kwa mchuzi wa maharagwe ya nazi ama nyama. Mbali na kula kama chajio ama chamcha, unaweza kula chapatti zako asubuhi na chai.

Kutayarisha Lishe Kwa Ajili Ya Covid-19 Ambazo Zitakaa Kwa Muda Mrefu

Kuendeleza Mada ya kutayarisha lishe kwa ajili ya covid-19

 • Samaki

Samaki ni mojawapo ya vyakula vinavyo weza kukaa kwa muda mrefu baada ya kuhifadhiwa ipasavyo. Baada ya kuhifadhiwa vyema, unaweza pika samaki yako kwa njia tofauti. Njia mojawapo ya kutayarisha samaki wako:

Viungo

 • Samaki mbichi
 • 1 kitunguu
 • 3 nyanya
 • Mafuta ya kupika

Maagizo

 1. Hakikisha umetoa scales kwa samaki wako kisha uoshe vyema.
 2. Kata vipande vidogo kisha umwagilie chumvi na uweke nje kwenye jua angalau dakika 30 akauke.
 3. Pasha mafuta yako joto hadi iwete moto.
 4. Samaki wako akikauka, mweke kwenye mafuta iive hadi iwe ya rangi ya hudhurungi.
 5. Kaanga kitunguu chako na nyanya kwenye sufuria tofauti. Kisha uongeze kikombe kimoja cha maji kwenye mchanganyiko huu hadi zi chemke.
 6. Weka samaki yako kwenye supu hii ya kitunguu na nyanya na ufunike kwa dakika 10.
 7. Punguza moto.

Unaweza kula samaki wako kwa ugali.

Kutayarisha Lishe Kwa Ajili Ya Covid-19 Ambazo Zitakaa Kwa Muda Mrefu

 • Mandazi

Viungo

 • 3 vikombe vya unga ngano
 • ½ kikombe cha sukari
 • 1 ½ vijiko kwa poda ya kuoka (baking powder)
 • 2 vijiko vya cardamom
 • ½ kijiko cha chumvi
 • 1 yai
 • 1 cani ya maziwa ya nazi
 • Mafuta ya kukaanga

Maagizo

 1. Kwa bakuli kubwa, changanya unga, sukari, poda ya kuoka, cardamom na chumvi. Tengeneza kana kwamba dura kati kati kisha uongeze yai na maziwa ya nazi, changanya kisha uchanganye kwa pamoja viungo vyote.
 2. Toa mchanganyiko huo kwenye bakuli uwekelee kwenye sehemu laini. Knead hadi uwe laini. Kata sehemu nne. Tengeneza kana kwamba duara ya chapati, kisha ukate duara 8. Fanya hivi kwa dough iliyo baki.
 3. Pasha joto mafuta yako kwa kutumia sufuria kubwa.
 4. Kaanga mandazi yako dakika 2-3 kila upande. Baada ya kugeuka rangi kuwa hudhurungi, geuza upande mwingine. Wekelea kwenye vitambaa visafi kukausha mafuta yaliyo baki.
 5. Kula kwa chai. Mandazi yana uwezo kwa kukaa siku nyingi. Kwa hivyo una kiamsha kinywa tosha kwa siku chache zijazo.

Kutayarisha Lishe Kwa Ajili Ya Covid-19 Ambazo Zitakaa Kwa Muda Mrefu

 • Nduma

Viungo

 • Nduma
 • ½ kijiko cha chumvi

Maagizo

 1. Toa ngozi ya nduma kisha ukate vipande vidogo vidogo
 2. Weka maji kwa sufuria yako kiwango cha nduma
 3. Ongeza chumvi na ufunike bila kuacha nafasi yoyote.
 4. Weka moto wa wastani
 5. Pika kwa dakika 30 kisha uangalie ama zimeiva kwa kutumia kijiko cha uma ama kisu.
 6. Iwapo bado ngumu, zipe wakati zaidi ziive.

Unapokausha maji vizuri, utakuwa na chakula tosha kwa siku kadhaa. Zikiwa zimepikwa kwa njia hii, ziko sawa kuliwa kwa siku kadhaa. Kuna njia tofauti za kupika nduma. Pia unaweza pika ziwe kitoweo chako cha kula kwa sima ama wali.

 • Viazi vitamu

Viungo

 • Viazi vitamu
 • ½ kijiko cha chumvi

Maagizo

 1. Toa ngozi ya viazi vitamu na kisha ukate vipande vidogo vidogo
 2. Weka maji kwa sufuria yako kiwango cha viazi vitamu
 3. Ongeza chumvi na ufunike bila kuacha nafasi yoyote.
 4. Weka moto wa wastani
 5. Pika kwa dakika 30 kisha uangalie ama zimeiva kwa kutumia kijiko cha uma ama kisu.
 6. Iwapo bado ngumu, zipe wakati zaidi ziive.

kutayarisha lishe kwa ajili ya covid-19

 • Mihogo

Viungo

 • Mihogo
 • ½ kijiko cha chumvi

Maagizo

 1. Toa ngozi ya mihogo kisha ukate vipande vidogo vidogo
 2. Weka maji kwa sufuria yako kiwango cha mihogo
 3. Ongeza chumvi na ufunike bila kuacha nafasi yoyote.
 4. Weka moto wa wastani
 5. Pika kwa dakika 30 kisha uangalie ama zimeiva kwa kutumia kijiko cha uma ama kisu.
 6. Ikiwa mihogo yako bado ngumu, ipe wakati zaidi ziive.

kutayarisha lishe kwa ajili ya covid-19

 

Vyanzo: Kaluhiskitchen, Cookpad

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio