Yote Unayo Paswa Kujua Kuhusu Kutembea Ukiwa Umelala Na Matibabu Yake

Yote Unayo Paswa Kujua Kuhusu Kutembea Ukiwa Umelala Na Matibabu Yake

Kutembea ukiwa umelala kuna hatari nyingi hasa kwa watoto. Tuna angazia matibabu yake na jinsi ya kuwasalimisha watoto wanao fanya hivi.

Tatizo la kutembea ukiwa umelala huwafanya watu kuamka na kutembea wakiwa wamelala. Hutendeka pale ambapo mtu hutoka usingizi mzito kwa uzito mwepesi ama hali ya kuamka. Anaye tembea akiwa amelala hawezi sikia akiwa katika kitendo hicho na mara nyingi huwa hakumbuki. Kwa visa vingine, huenda akaongea vitu visivyo na maana. Bila shaka hili ni jambo hatari. Tuna angazia hatari za kutembea ukiwa umelala. Mara nyingi, huku hutendeka ungali mchanga kati ya umri wa miaka 4 hadi 8. Ila, watu wazima pia wanaweza fanya hivi. Watoto wanapo endelea kukua, huacha kufanya hivi. Lakini kufanya hivi ukiwa mkubwa huenda kuka ashiria tatizo kubwa la kulala.

Hatari za kutembea ukiwa umelala: Ishara zake

kutembea ukiwa umelala

Tatizo hili huwa na tabia za kushangaza, zisizo za kawaida na huenda zika husisha mambo ya vurugu. Mtu anaye fanya hivi huenda:

 • Kutoka kitandani na kutembea
 • Kuamka na kukaa kitandani na kurudia mwendo, kama vile kusugua macho
 • Kuangusha vitu
 • Kuto itika unapo mwongelesha
 • Kutatizika kuamka
 • Kuongea akiwa amelala
 • Kukojoa mahali pasipo faa
 • Kuchanganyikiwa
 • Kurudi kulala mbio
 • Kuto kumbuka kilicho tendeka
 • Kushtuka akiota

Katika visa nadra, mtu anaye tembea akiwa amelala anaweza:

 • Toka kwenye nyumba
 • Endesha gari
 • Kufanya tabia zisizo za kawaida kama vile kukojoa chumba cha kulala
 • Kuhusika katika matendo ya kimapenzi bila kujua
 • Kuumia
 • Kuanza vurugu

Vyanzo vya kutembea ukiwa umelala

kutembea ukiwa umelala

Kuna sababu nyingi zinazo wafanya watu kuwa na uraibu huu.

Huenda ikawa kwa familia. Mapacha wanao fanana huwa na nafasi zaidi za kufanya hivi. Ikiwa una mzazi ama ndugu ambaye hufanya hivi, una nafasi 10 zaidi za kufuata nyayo zao ikilinganishwa na mtu asiye na mwanajamii ambaye hufanya hivi.

Huenda ukawa na tatizo hili ikiwa:

 • Kukosa usingizi ama kuchoka
 • Usingizi unao katizwa ama kutopata usingizi wa kutosha
 • Kuwa mgonjwa na joto jingi
 • Baadhi ya madawa
 • Kuenda kulala bila kuenda haja ndogo
 • Mazingira yenye kelele na yasiyo himiza kulala kwa amani
 • Fikira nyingi
 • Kulewa

Hali za kimatibabu zinazo husishwa na jambo hili ni kama vile:

 • Joto jingi
 • Kiungulia
 • Asthma ya jioni
 • Seizure za usiku
 • Apnea- kukosa kupumua kwa muda ukiwa umelala
 • Post traumatic stress

Hatari Za Kutembea Ukiwa Umelala

Baadhi ya watu wanao fanya hivi huwa na ishara nyepesi na watakaa kitandani ama waanze kuongea wakiwa wamelala. Watu wanao amka na kuanza kutembea wakiwa katika usingizi mzito wanaweza jihatarisha. Wanao fanya hivi wamejulikana kuamka na kwenda kutembea kwenye bara bara. Baadhi yao wamejaribu kuendesha gari wakiwa wamelala. Ili kupunguza hatari hizi, ni muhimu kutengeneza mazingira salama ya kulala. Vitu ambavyo vinaweza vunjika vinapaswa kutolewa karibu na kitanda. Kuepuka kuanguka, milango inaweza fungwa pamoja na madirisha ili kuwazuia kutoka kwenye nyumba.

keeping your toddler safe in bed

Matibabu

Hakuna matibabu hasa ya kusuluhisha tatizo hili. Katika visa vingi, kuimarisha afya yako ya kulala, kuna weza suluhisha. Ikiwa unashuhudia ishara, unapaswa kuongea na daktari ama mtaalum wa usingizi kuhusu njia za kuepuka ajali katika vipindi hivyo na kuangalia iwapo una ugonjwa unao sababisha.

Jinsi ya Kukoma Kutembea Ukiwa Umelala

Ikiwa mtoto wako ama mchumba wako ana athiriwa na jambo hili, hapa kuna baadhi ya hatua ambazo unaweza chukua:

 • Anza kwa kuangalia mambo anayo fanya kabla ya kulala na utengeneza ratiba ya kwenda kitandani na kuamka wakati sawa kila siku.
 • Jaribu kuoga na maji moto na kusoma kidogo kabla ya kulala.
 • Tengeneza mazingara salama ya kulala, hasa kwa watoto wanao tembea wakilala. Ondoa vitu vikali na ufunge madirisha na milango.
 • Uliza ushauri kutoka kwa daktari wako

Sleep Foundation

WebMD
Soma Pia:Utafiti Wa Kisayansi Waonyesha Faida Za Kiafya Za Kulala Mchana

Written by

Risper Nyakio