Jinsi Ya Kuachana Na Mtu Unaye Mpenda

Jinsi Ya Kuachana Na Mtu Unaye Mpenda

Kabla ya kufanya uamuzi wa kutengana na mchumba wako, ni vyema kuwa na mazungumzo na mchumba wako huenda mkatatua matatizo yenu.

Kushangaa mara kwa mara kama unapaswa kubaki katika uhusiano na mtu ama kuwachana ni kawaida kwa watu wengi katika uhusiano. Kila wanandoa haijalishi wanavyo onekana huku nje, hupitia mambo magumu. Na hata kama unampenda mchumba wako sana, sio jambo geni kushangaa kama uhusiano wenu unafaa. Kuelewa tofauti kati ya misuko suko ya kawaida ya uhusiano wenye afya na ishara kuwa uhusiano wenu unafika tamati sio rahisi. Lakini kuna dalili chache zitakazo kusaidia kujua kuwa ni wakati wa kutengana na mchumba wako.

Ishara kuwa ni wakati wa kutengena na mchumba wako

kutengana na mchumba wako

Ukiona baadhi ya ishara hizi katika uhusiano wako, ni wakati wa kutazama kwa kina kama kuna haja ya kuendelea kuwa katika uhusiano huo.

Mna tengana na kurudiana mara kwa mara

Kutengana na kurudiana mkiwa kwa uhusiano mngali wachanga ni sawa. Ila mambo yanapaswa kubadilika ukikomaa. Ni sawa kuwa na umbali mnapo pitia wakati mgumu. Lakini kama mnawachana na kurudiana mara kwa mara, kuna uwezekano kuwa hamtatui vyanzo vya matatizo yenu.

Unajitolea wakati wote

Ili uhusiano wowote ule ufuzu, wachumba wana stahili kujitolea lakini kwa njia yenye afya kuonyeshana mapenzi yao. Baadhi ya wakati, huenda ukamwacha mchumba wako achague mahali ambapo angependa mkule, kitu ambacho angetaka mfanye pamoja. Lakini huenda wakati mwingine kuna uamuzi mkubwa unao hitajika kufanyika. Wakati wote ukipata kuwa wewe ndiye unajitolea na kumpatia kila kitu bila kuhisi kama juhudi zako zina puuzwa. Huenda kukawa na umbali kati yenu ama hisia za chuki kuibuka.

Hauna imani kwao

Kuwa na shaka wakati wote kuwa huenda mchumba wako akawa ana danganya kuhusu mambo tofauti. Kuenda kuangalia rununu yao ni jambo litakalo kuhisi hauna imani. Ikiwa mchumba wako ana historia ya kutoka nje ya uhusiano, jambo hili lita sababisha kutengana kwenu baada ya muda.

Mmekuwa mkitengana

kutengana na mchumba wako

Unahisi kuwa mmetengana kiasi kwamba hauwezi elewa? Ni vigumu kuwasiliana ama kuongea kuhusu yanayo watatiza. Wanandoa wengi hukumbuka walivyo kuwa walipo patana mara ya kwanza na kupuuza vile ambavyo wamekua na mambo kubadilika. Kuhisi kuwa mnatengana huenda ikawa ni ishara kuwa hamtaki kushikilia ya kale.

Ishara zaidi kuwa mna umbali

  • Hamjali ama kutia juhudi kama uhusiano wenu
  • Una dhaliliwa kihisia na kifizikia
  • Hujipendi tena
  • Mnapigana kila wakati
  • Mahitaji yako haya toshelezwi
  • Unafikiria kuhusu kuwachana kila mara

Ikiwa umefanya uamuzi wa kutengana na mchumba wako, fanya haya:

Kabla ya kufanya uamuzi wa kutengana na mchumba wako, ni vyema kuwa na mazungumzo na mchumba wako huenda mkatatua matatizo yenu. Msamehe ikiwa amekukosea. Baada ya hayo yote kama ungali unataka kutengana naye fanya haya.

Panga vyema

Jua unacho stahili kufanya na wakati wa kukifanya. Ikiwa mnaishi pamoja, huenda likawa jambo la busara kutafuta nyumba ingine. Kisha umwelezee mchumba wako.

Chagua mahali pazuri pa kutengana

Chagua mahali ambapo mchumba wako hata ona haya baada ya kuwa na mazungumzo kuhusu uamuzi wako wa kutengana. Hakikisha kuwa una mazungumzo wazi naye.

Chanzo: WebMD

Soma PiaKinacho Fanya Uhusiano Kufuzu

Written by

Risper Nyakio