Jinsi tunavyozidi kukua ndivyo maisha yetu yanavyo badilika. Majukumu yanaongezeka na kutufanya tusiwe na wakati tosha wa kijamii, dakika chache tunazopata, tunajipata tukikaa mbele ya televisheni kutizama sinema ama vipindi tunavyo vifurahia. Tunavyozidi kuongeza umri, tunatengana na marafiki zetu, huku wengine wakihamia pande tofauti za dunia na kupata kazi tofauti na sisi, tunakosa utangamano ulokuwa hapo awali na marafiki wapya.
Haijalishi umri wetu, sote tunahitaji marafiki na kuwa na maisha ya kijamii. Hakuna umri ambapo mtu anaweza kosa kupata marafiki zaidi. Tazama baadhi ya njia za kutengeneza urafiki na kusaidia kudumisha urafiki wa hapo awali.
Jinsi Ya Kupata Marafiki Zaidi

- Kubali kuwa unahitaji marafiki
Kubali ukweli kuwa unahitaji marafiki maishani mwako. Kukubali hili kutakusaidia kupita kwenye imani ya kiakili inayokuzuia kupata marafiki wapya. Kuwa na marafiki kunakusaidia kuwa na watu ambao unaweza kuzungumza nao iwapo kuna jambo linalo kusumbua.
Kuzungumza kwa mtandao ni jambo zuri, lakini ni muhimu kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja. Hivi, unaeza kuwa na utangamano wa kihisia na mtu mwingine. Pia, unaweza kuzuru mahali mpya unapoenda kupatana na marafiki zako. Rafiki mpya atakuonyesha sehemu tofauti unazohitaji kutembea pia.

- Patana na marafiki wa hapo awali
Marafiki hutengana kwa sababu tofauti, kupata muda wa kuzungumza na marafiki wa hapo awali kunasaidia kurejesha uhusiano ulokuwa. Hata ingawa kutengeneza marafiki wapya ni jambo nzuri, hakuna kinachopiku kurudiana na marafiki wa hapo awali.
Wakati mwingi, urafiki hudidimia pale ambapo marafiki hawapati wakati tosha wa kuwa pamoja. Kwa hivyo rafiki yako anapokuuliza iwapo utapatikana kwenda kutizama kadanda ama kwenda sherehe, ni vyema kukubali mara kwa mara. Mbali na kupatana na marafiki zako, unapata muda wa kutoka nje na kuona kinacho endelea nje ya nyumba yako na pia kukutana na watu wapya.
Kuwa na marafiki kuna faida nyingi, na hakuna umri ambapo mtu hawezi kupata marafiki wapya. Ni vyema kuzidi kuongeza familia yako ya kijamii. Huku ukizidi kuongeza marafiki wapya, usisahau kurejesha utangamano uliokuwa hapo awali na marafiki zako wa awali.
Soma Pia:Sababu 3 Kwa Nini Bibi Yako Amekasirika Wakati Wote