Kutingika Kabla Ya Uchungu Wa Mama Na Baada Ya Kujifungua

Kutingika Kabla Ya Uchungu Wa Mama Na Baada Ya Kujifungua

Utashuhudia kutingika kwa mwili iwapo unajifungua njia ya asili ama C-section!

Kwa sasa kwani uko katika trimesta yako ya tatu, huenda ukawa umesoma kila kitu kuhusu uchungu wa uzazi. Huenda pia ukawa umechukua madarasa kujitayarisha kwa siku yako kuu. Na umejihamia na maarifa ya ushuhuda wa kujifungua kwa kweli. Ila hakuna darasa ama kitabu ambacho kita kutayarisha kwa kipindi hiki kikuu cha kutingika wakati wa kujifungua, kabla ya kushuhudia uchungu wa uzazi na baada ya kujifungua pia.

Karibu wanawake wote hushuhudia kutingika wakati wa kujifungua kabla ya kujifungua. Jambo hili linaweza fanyika haijalishi mpango wako wa kujifungua.

Kwa hivyo iwapo una jifungua kwa kawaida ama kutumia epidural ama upasuaji wa C-section, nafasi kuwa utashuhudia kiwango cha chini cha jambo hili hakija dhibitishwa.

Ila hakuna haja ya kuwa na shaka. Huku hakuta tahadharisha maisha ya mtoto wako kwa njia yoyote.

Kutingika katika ujauzito kabla na baada ya uchungu wa uzazi: Ni jambo la asili

shaking before labour

Kutingika katika kujifungua ni matokeo ya kubadilika kwa homoni. Mabadiliko machacho katika viwango vya homoni huenda vikafanya mabadiliko kadhaa katika fizikia na kisykologia kwenye mwili. Na huku kunafanyika katika kujifungua.

Ili kuelewa kwa nini unashuhudia kutingika katika ujauzito kabla ya uchungu wa uzazi, kwanza tuelewe mchakato wa uchungu wa uzazi. Kwa ujumla kuna hatua tatu katika uchungu wa uzazi hai.

  • Hatua ya kwanza: Hatua hii inaanza na kukaribia kwa uchungu wa uzazi. Huenda ukashuhudia kubanwa kwa tumbo na kutaongezeka kwa karibu 10 cm. Hii ndiyo pande hai ya uchungu wa uzazi na kubanwa huwa kwa sekunde 60 hadi 90. Zinafanyika mara kwa mara baada ya kila dakika mbili.
  • Hatua ya pili: Katika hatua hii, unashuhudia kujifungua kwa kweli na unamsukuma mtoto nje. Ama unafanyiwa upasuaji wa C-section. Wanawake wengi hushuhudia kutapika na kichefu chefu wanapo anza kuhisi hivi. Haijalishi iwapo wamepatiwa dawa za kulala ama la. Pia hii hukuwa hatua ngumu zaidi ya uchungu wa mama.
  • Hatua ya tatu: Katika hatua hii ya tatu na ya mwisho, placenta yako inatoka. Kwa ujumla, mwili wako unatoa kila kitu kilicho baki ndani ya mwili wako baada ya mtoto kuzaliwa.

 Unaweza hisi kutingika wakati wa ujauzito kabla ya uchungu wa mama katika mojawapo ya hatua hizi. Kwa kawaida, kutingizwa huku kunashuhudiwa baada ya kujifungua tu.

Kwa kawaida hii huwa kufuatia adrenaline kwa sababu ya homoni kufuatia mabadiliko ya joto mwilini.

Hasa, utafiti ulio chapishwa kwenye PubMed pia unasema kuwa kutingika hakusababishwi na sababu kama joto ama kubadilika kwa homoni.

Somo hili lina sema kuwa kuonekana kwa kliniki kuwa kutingika kwa peripartum hakuwezi thibitika na kipima joto. Waandishi wengine walipata kutoa jasho isiyo ya kipima joto.

Uwingi wa kutingika wakati wa ujauzito kabla na baada ya uchungu wa mama ni upi?

Tena, huku kuna tofautiana katika kila mama kwenye uchungu wa mama. Kutingika huku hasa huisha baada ya sekunde chache hadi dakika chache. Ila, kama tulivyo taja, pamoja na kutingika wakati wa uchungu wa uzazi, wanawake wengi huhisi dalili zingine za kujifungua pia.

Hizi ni kama kutingika kwa baridi na kutoa jasho, kuhisi kujikuna, kutapika ama kulia.

Katika visa vingi, kuoga kwa maji moto ama kufunikwa kwa blanketi joto hupunguza kutingika. Kuna tuliza misuli na neva.

Wakati mwingine, matibabu kama Demerol (ambayo ni narcotic) ina peanwa. Ila, haipeanwi kwa visa nadra na chini ya kuangaliwa na mtaalum wa afya ya wamama.

 Sayansi nyuma ya kutingika wakati wa ujauzito kabla ya uchungu wa mama ni ipi?

Hata kama wana sayansi bado hawaja dhibitisha maana ya kutingika, sababu hizi zinajulikana kuwa vyanzo zaidi.

1. Homoni mwilini

Wakati wa uchungu wa uzazi, homoni ya oxytocin inapatiwa kwa mama ili kuanzisha uchungu wa mama. Maana ya homoni hii ni kupunguza uterasi na kuthibiti utoaji wa damu.

Homoni hii inasababisha kubanwa kwa uterasi na misuli ambazo wanawake wengi huhisi kwenye mikono na miguu.

Kwa kuongeza kubanwa huku, homoni za kukwaza kama vile epinephrine, cortisol na adrenaline huku ikibadili fluids za mwili. Jambo hili husababisha kutingika katika uchungu wa uzazi.

2. Exertion

Kusukuma mtoto nje ya uke wako ni kazi ngumu. Mwili wako wote unafanya kazi ili jambo hili litendeke na pia exertion nyingi ni kiwango kikubwa. Unapo weka shinikizo ili kusukuma mtoto nje, joto ya mwili wako unaongezeka.

Wakati ambapo mtoto wako anazaliwa, mwili wako unajaribu kurudi kuwa kawaida na hivi kwamba kuongeza joto mwilini. Kufuatia heat regulation, unahisi kutingizwa. Hii ni kawaida kwa fizikia yako mwilini. Unapaswa kuwacha kuhisi hivi baada ya dakika ama masaa machache.

3. Damu kuto kuwa aina sawa

Imani ingine ya hivi sasa pia inasema kuwa kutokuwa sawa kwa damu ni sababu ya kutingika katika uchungu wa uzazi. Wataalum wanasema kuwa katika uchungu wa uzazi, baadhi ya kiwango cha damu ya kiinitete hugusana na bloodstream wa mama.

Kwa hivyo kuna kutokuwa sawa kwa aina za damu kati ya mama mpya na mwanawe –  kwa mfano iwapo mama ana A+ na mtoto ana AB+ anaweza hisi kutingika, meno kutoa sauti na baridi katika kuzaliwa kwa mtoto.

shaking during pregnancy

Shaking during pregnancy before labour: Sometimes cold intravenous fluid administration can also cause shivering to some extent. | Image courtesy: Dreamstime

4. IV Fluids

Katika baadhi ya visa, kupatiwa kwa intravenous fluid huenda kukasababisha kutingika. Kwa mfano, wakati ambapo mama anapatiwa epidural ama dawa yoyote ile katika kujifungua, kuna uwezekano kuhisi baridi na kutingika.

Hii ni kwa sababu nyingi kati ya IV fluids ni baridi kuliko joto ya mwili. Kwa hivyo vinapo ingia mwilini, zinaweza kufanya uhisi baridi.

5. Mguzano wa Amniotic fluid

Wakati wa mchakato wa kujifungua, baadhi ya wakati, amniotic fluid huingia kwenye bloodstream. Hii hufanyika mara nyingi wakati wa upasuaji wa C-section na sio kujifungua kwa asili. Ila, pia inaweza sababisha kiwango cha kutingizwa.

6. Maambukizi

Katika baadhi ya visa, wamama huenda pia wakawa na joto jingi katika wakati wa kujifungua. Iwapo joto yako ni zaidi ya 100 C, huenda ikathibitisha una maambukizo.

Daktari wako ata angalia masaa yako 24 baada ya kujifungua. iwapo nambari bado iko 100 na unahisi uchungu wa pelviki ama kuumwa na matiti na wanaweza pima maradhi yako kutoka kwa tishu ambazo hazija toka, na kuzibwa kwa misuli kutoa maziwa ama hata mastitis.

Walakini, iwapo unafikiria una shuhudia hii mara moja kwenye maisha yako, umefeli.

 Je, utashuhudia kutingika kila mara kabla ya kujifungua?

Jibu ni ndio. Kila mara unapo jifungua na kushuhudia homini nyingi katika hatua ya mwisho ya ujauzito, utahisi kutingizwa huku.

Pia, iwapo una shuhuda moja wapo ya hizi, una weza shuhudia kutingika wa uchungu wa uzazi.

Kama tulivyo taja hapo juu, kutingika wakati wa uchungu wa uzazi unakuja bila ya kuitwa, haijalishi idadi ya kujifungua uliko shuhudia hapo awali. Ila, kuna njia za asili nyingi kwa mama ili kufanya jambo hili liwe kawaida na kuhisi nguvu zaidi.

 Njia bora zaidi za kumtuliza mama mpya ni zipi?

Kwa sababu mama mpya ameshuhudia kutingika wakati wa kujifungua, mwili wake ni nyeti na una baridi. katika hatua hii, atahitaji msaada wote ambao anaweza pata- wa kifizikia, kiakili ama kihisia.

Hapa ni baadhi ya njia za kumsaidia kutulia.

1. Mpashe joto

Punde tu baada ya mama kushuhudia kutingika katika kujifungua, madaktari na wauguzi wanapaswa kumfunika kwa blanketi. Huku kuna mfanya ahisi joto na kutuliza mwili wake.

Kwa wakati mwingi, madaktari humfunika upande wa juu wa mwili katika meza ya kujifungua kwa sababu wanajua kinacho fuata. Punde baada ya kujifungua kumefanyika, mama anasafishwa na kufunikwa kwa kutumia blanketi zenye joto na kupatiwa muda apumzike.

african mum holding newborn

Shaking during pregnancy before and after labour: Skin-to-skin contact with the baby can help bring down a new mother’s temperature. | Image courtesy: Pinterest

2. Ngozi kwa ngozi na mtoto

Kuhisi joto na usalama hakushuhudiwi na mtoto tu, ila na mama anapo mshika mwanawe kwa mara ya kwanza.

Madaktari wanashauri mama wapya kuwashika watoto wao punde tu baada ya kujifungua. Kama kuna wezekana, wanaulizwa kuwa na uhusiano wa ngozi kwa ngozi kuhisi joto.

Baadhi ya wamama huenda wasiweze kufanya hivi ama hawa tataka. Ila, ukweli ni kuwa kuguzana ngozi kwa ngozi na mtoto kuna weza saidia kushusha joto mwilini.

3. Matibabu

Katika visa vilivyo nadra, kutingika hufuatwa na joto jingi. Jambo hili huenda likawa hatari kwa mama na pia kwa mtoto mchanga aliye zaliwa.

Mama lazima amnyonyeshe mtoto kati ya lisaa limoja baada ya kujifungua. Na iwapo ana joto jingi, mtoto hatapata maziwa ya kwanza ya mama na colostrum.

Katika visa kama hivi, mama anaweza patiwa dawa ili kupunguza joto jingi mwilini na kutingika huku. Huenda pia aafunganishwa na blanketi zilizo na joto na kupewa wakati zaidi ili apone kutokana na kujifungua.

Jambo la pekee unalopaswa kukumbuka hapa ni kuwa kutingika wakati wa kujifungua ni la kawaida. Ni mwili wako unaanza kupona. Ina maana kuwa unahitaji msaada wa kiakili, kihisia na kifizikia.

Kwa hivyo iwapo hujasoma kuhusu kutingika wakati wa kujifungua hapo awali, kuwa tayari kushuhudia jambo hili kwenye meza ya kujifungua.

Vyanzo: N CBI, WebMD

SOMA PIA: The Way We Think About Labour Might Change How We Feel It

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Deepshikha Punj kisha yaka chapishwa tena na idhini kutoka kwa  theAsianparent na baadaye kutafsiriwa na Risper Nyakio.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio