Onyo Kwa Mama Mwenye Mimba: Kuto Kula Protini Kunaweza Sababisha Haya!

Onyo Kwa Mama Mwenye Mimba: Kuto Kula Protini Kunaweza Sababisha Haya!

Lishe ya mama mjamzito ni muhimu sana kwa kumlisha mtoto. Je, huku kuna maana kuwa wanawake wanao zingatia kuto kula protini katika mimba wako katika hatari ya kupata watoto ambao hawaja komaa? Kulingana na ripoti hii, kuna uwezekano mkubwa wa hili kufanyika.

Hatari Za Kuto Kula Protini Katika Mimba

kuto kula protini katika mimba

Inasema kuwa kulingana na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Norwegia, nyama kidogo sana kutoka kwa wanyama ina sababisha ukosefu wa vitamini ya B12, na kusababisha ongezeko la asilimia 21 ya nafasi zake za kujifungua kabla ya wakati. Lakini kulingana na daktari Sunil K Agrawal kutoka hospitali ya Fortis Mohali India, wakati ambapo nambari ya masomo imeonyesha ongezeko la hatari ya kujifungua kabla ya wakati, ushahidi zaidi unahitajika. Alizidi kusema, "Wanawake wajawazito wanao zingatia lishe isiyo na protini kutoka kwa wanyama wana nafasi zaidi za kuugua ukosefu wa vitamini B12 tosha. Ukosefu wa vitamini pamoja na folic acid una husishwa na changamoto za maumbili katika kujifungua.

Pia, hiyo haiegemezi 'lishe isiyo na protini za wanyama ina sababisha kujifungua mtoto asiye komaa'. Walakini, ni vyema kwa mama mjamzito kuwa na lishe iliyo na virutubisho vyote, protini, madini na vitamini ili kuhakikisha kuwa mtoto anakua na afya. Nini inayo sababisha kujifungua kabla ya wakati? Kulingana na daktari Agrawal, hapa kuna baadhi ya sababu ambazo huenda zika sababisha kujifungua mtoto asiye komaa:

kuto kula protini katika mimba

 • Kujifungua mtoto kabla ya wakati hapo awali
 • Mimba ya mapacha ama zaidi
 • Kipindi chini ya miezi sita kati kati ya ujauzito
 • Kutunga mimba kupitia kwa IVF(in vitro fertilisation)
 • Matatizo ya uterasi, kizazi ama placenta
 • Kuvuta sigara ama dawa za kulevya
 • Lishe isiyo na afya
 • Kuto ongeza uzito unaofaa katika mimba
 • Baadhi ya maambukizi, hasa ya amniotic fluid
 • Baadhi ya hali sugu kama vile shinikizo la juu la damu na kisukari
 • Kuwa na uzito wa chini wa mwili ama uzito mwingi kabla ya mimba
 • Tukio za kukwaza maishani kama vile kifo cha mtu unaye mpenda ama vita vya kinyumbani
 • Kupoteza mimba mara kadhaa
 • Majeraha ya kifizikia

Kutoka kwa orodha hii, wakati ambapo hali nyingi za kimatibabu na matukio fulani maishani huenda yakawa hayawezi kudhibitiwa na mwanamke mjamzito, anaweza kuwa na usemi wa lishe yake. Haijalishi ikiwa hali protini za wanyama, ama hali nyama kabisa, anapaswa kuhakikisha lishe yake ni ya afya, kwa kudhibiti na yenye virutubisho vyote muhimu. Na akifanya hivi bila shaka hakuna haja ya kuwa na shaka kuhusu afya ya mtoto wake.

Bila shaka watoto wanao zaliwa kabla ya wakati huwa na hatari zaidi ya kuugua wanapo zidi kukomaa na huenda wakakomaa pole pole ikilinganishwa na watoto walio zaliwa wakati unaofaa. Pia wako katika hatari ya kuugua matatizo ya kiafya ya muda mrefu kama vile autism, matatizo ya ushupavu, shida za mafua na cerebral palsy na kadhalika. Lakini watoto wanao zaliwa baada ya miezi 7 wana hitaji kukaa kwa muda mfupi hospitalini kwenye sehemu ya utunzi wa dharura (NICU) neonatal intensive care unit. Watoto wanao zaliwa mapema kuliko hivyo huwa katika hatari zaidi.

Hata kama mtoto wako alizaliwa kabla ya wakati, usiwe na shaka, mara nyingi wao hukua na kupata afya.

Soma Pia:Lishe Na Siha Ya Mama Mwenye Mimba: Vyakula Muhimu Katika Mimba

Written by

Risper Nyakio