Jinsi Ya Kumweleza Mume Wako Kuwa Hakutoshelezi Kitandani

Jinsi Ya Kumweleza Mume Wako Kuwa Hakutoshelezi Kitandani

Kumbuka kuwa kitendo cha mapenzi kina hitaji watu wawili. Ikiwa hauto shelezwi kitandani, unaweza msaidia mume wako kwa kumwuliza anacho kipendelea pia.

Ndoa ina mengi na kuna nyakati ambazo mnahitaji kuwa na mazungumzo ya undani kuhusu mada tofauti hata zisizo wafurahisha sana. Lakini mnapo ongea kuhusu mada nyeti, unapaswa kutia akilini hisia za mwenzi wako. Na ikiwa unataka kumweleza mchumba wako kuhusu kuto toshelezwa kitandani kwako, unapaswa kufikiria kuhusu hisia zake.

Wanaume hujivunia ustadi wao wa kitandani. Na mara nyingi huenda wakajiona kuwa wao ni simba katika nyanja hiyo ilhali wao ni paka.

Lakini unaweza saidia kwa kupendekeza mbinu za kuimarisha ustadi wao bila kuumiza hisia zao.

Jinsi ya kumwelezea mume wako kuhusu kuto toshelezwa kitandani kwako

kuto fika kilele katika ngono

Ikiwa mume wako hakutoshelezi kitandani, hapa kuna njia 5 nzuri za kumjuza haya

  1. Kuwa na hisia chanya na usiwe rasmi sana

Ibua mada za kitandani katika mazungumzo yenu, mnapo tazama televisheni ama mkikula nyumbani. Kwa njia hii, haita onekana kuwa jambo kubwa. Badili mtazamo wako uwe kwa mazuri na kilicho kufurahisha zaidi kuhusu kipindi chenu kilicho pita. Sisitiza unacho penda mnapo kuwa katika awamu zenu kitandani. Baada ya muda, ata anza kujitahidi.

Mwana saikolojia Kristen alieleza kuwa matatizo ya kitandani yana paswa kujadiliwa mbali na chumba hicho. Ana washauri wanawake kuzungumza kuhusu wanavyo pendelea kitandani.

2. Mara kwa mara, zidi kuhimiza mazuri

Hata kitandani, unaweza mhimiza mchumba wako kufanya vyema zaidi bila kuisema kwa makali. Vipi? Mjuze anacho fanya vyema mara kwa mara. Kwa mfano, ikiwa haupendelei kitu anacho kufanyia wakati wa kufanya mapenzi huku akidhani kuwa unakifurahia, jaribu kubadili mwendo wake katika kipindi chenu cha kufanya mapenzi.

Kumbukeni kuwa, mkizidi kufurahishana, hakuna njia mbaya wala sahihi ya kufanya mapenzi. Lakini kuna njia bora ya kufanya kinacho wafurahisha nyote.

"Ni rahisi sana kwa wanaume kuhisi kana kwamba wanafanya kitu kibaya, lakini hakuna mbaya wala sahihi," alieleza Carin Goldstein. "Nyote mnapaswa kuelewana, miili yote ya wanawake huwa tofauti."

3. Mwonyeshe unacho taka wala sio kumkemea

Jinsi Ya Kumweleza Mume Wako Kuwa Hakutoshelezi Kitandani

Epuka kumkemea mchumba wako anapo fanya kitu usicho kipendelea. Badala yake, mwonyeshe unacho kipendelea. Angazia vitendo unavyo vipendelea kitandani. Mwelekeze unavyo pendelea.

4. Usimliwaze

Unapo zungumza naye kuhusu unacho kipendelea na usicho kipenda, usimliwaze na maagizo mengi. Ikiwa mume wako hakutoshelezi kitandani, huenda akawa ana mambo yanayo mtatiza akilini. Jambo la mwisho unalo taka kufanya ni kumtia mawazo zaidi. Mwelekeze mara kwa mara.

5. Kuwa wazi kupokea maoni yake pia

Kumbuka kuwa kitendo cha mapenzi kina hitaji watu wawili. Ikiwa hauto shelezwi kitandani, unaweza msaidia mume wako kwa kumwuliza anacho kipendelea pia. Huenda mbinu yake ika imarika unapo fanya staili zilizo asili zaidi kwake.

Mazungumzo ni muhimu! Mwisho wa siku, tendo la kufanya mapenzi huwa bora mnapo elewa miili ya wachumba wenu.

Vyanzo: SELF, Bustle

Soma PiaJinsi Ya Kumpa Bwanako Hamu Ya Kufanya Mapenzi Ili Kuipa Ndoa Yako Ladha

Written by

Risper Nyakio