Watu wengi hutatizika na hali ya gesi kujaa tumboni, na kuifanya iwe muhimu kujua namna za kutoa gesi tumboni kwa haraka. Vitu kama mazoezi, tembe na kukanda mwili husaidia kutatua hali ya kupunguza kufura tumbo.
Kufura tumbo hufanyika gesi inapojaa tumboni ama kwenye matumbo. Kujaa tumbo kunapofanyika baada ya kula chakula, tatizo hilo hujitatua lenyewe.
Jinsi ya kutoa gesi tumboni kwa haraka
- Fanya yoga

Kuna baadhi ya nafasi za yoga zinazofanya misuli ya tumbo kwa njia inayoboresha kuwachilia gesi na kusaidia katika kupunguza kujaa gesi tumboni. Nafasi kama child's pose na kuchuchumaa.
2. Kutembea
Kufanya shughuli za kifizikia hufanya utumbo kuwa na mwendo wa mara kwa mara na kusaidia kutoa gesi zaidi tumboni. Kutembea kwa dakika chache kwa siku ni njia bora ya kutoa gesi tumboni kwa haraka.
3. Kukandwa tumbo

Masi ya tumbo inaweza saidia na mwendo wa utumbo. Unaweza kufuata mbinu hii kufanya masi ya tumbo. Fuata mkondo wa duara huku ukishinikiza kwa upole kwenye upande wa kulia wa ribcage, kisha upande wa juu wa tumbo kisha upande wa kushoto wa ribcage. Kisha kurudia mara zinazohitajika.
4. Kutumia essential oils
Essential oils kama fennel na curcumin zimedhibitishwa kusaidia na maumivu ya tumbo na kufura kwa tumbo. Hata hivyo, ni muhimu kuwasiliana na daktari kabla ya kutumia essential oils.
5. Tembe za kutoa gesi

Kuna tembe kama simethicone zinazosaidia kutoa gesi zaidi kutoka kwa mfumo wa kuchakata chakula. Hata hivyo, hakikisha kuwa unafuata maagizo yaliyoonyeshwa.
6. Punguza unywaji wa soda
Soda huwa na gesi nyingi, kadri unavyozidi kuinywa ndivyo unavyoongeza viwango vya gesi tumboni. Sukari iliyo kwenye soda husababisha kufura tumbo na tumbo kujaa gesi. Badala yake, unaweza kunywa maji.
7. Kula fiber

Fiber mwilini husaidia kuepusha kufura tumbo na kujaa gesi tumboni. Kuongeza chakula kilicho na fiber kulingana na mahitaji ya mwili wako kunasaidia. Ongeza viwango vya fiber polepole hadi mwili uzoee.
8. Fanya mazoezi
Kufanya mazoezi husaidia mwili kutoa gesi mwilini. Mazoezi yanatoa sodium zaidi kutoka mwilini kupitia kwa jasho na inasaidia kutoa maji yaliyohifadhiwa mwilini.
Kupunguza ulaji wa chumvi ama kiwango unachochukua na kula gum kunasaidia katika kutoa gesi tumboni kwa haraka.
Soma Pia:Vyakula 5 Vya Kuepuka Kwa Mama Mjamzito Ili Kudumisha Afya Katika Mimba