Kutoa gesi tumboni kwa mtoto mchanga huwa baadhi ya shaka za mama wa mara ya kwanza. Ni kawaida kwa watoto kuwa na gesi nyingi. Sio jambo jipya kwao kupitisha gesi ama kunyamba kwa mara 13-21 kwa siku. Watoto wachanga huwa na nafasi nyingi ya kumeza hewa kama wanapokula, kunywa maziwa kutoka kwa chupa ama kulia.
Unaweza fahamu kuwa mtoto ana gesi tumboni anapolia na kusumbua ovyo, kufura tumbo, kushuta kwa sana, kuwa na tumbo ngumu. Kulingana na mtaalum wa afya ya watoto, mtoto anapokuwa na furaha dakika moja kisha kuanza kusumbua dakika nyingine anapopitisha gesi, ni ishara kuwa ni kawaida. Ila, anapogeuka na kuwa mwekundu kisha kupiga kelele, ina maana kuwa kuna kitu kinachomsumbua. Pia, hali hii ya kuwa na gesi tumboni kwa watoto hupungua japo mtoto anavyozidi kukua.
Kutoa gesi tumboni kwa mtoto mchanga

Mama anaweza kutumia baadhi ya mbinu hizi za kutoa mtoto hewa tumboni.
1.Kusukuma tumbo la mtoto kidogo na kwa upole. Kushinikiza sehemu za mtoto kunasaidia kutoa hewa tumboni na kumfanya kubeua.
2. Kumkanda mtoto mgongoni. Nusu saa baada ya mtoto kunyonyeshwa, mlaze kati ya mapaji kisha uanze kumkanda mgongoni. Ikiwa amepata hewa akinyonya, hewa itatoka.
3. Mara nyingi mtoto hupata hewa tumboni anaponyonya kwa muda mrefu. Kama vile kumnyonyesha mtoto baada ya kila dakika 30 kwa dakika tano. Kumnyonyesha mtoto kwa muda mfupi mara kwa mara kunapunguza uwezekano wa mtoto kutatizika na hali ya gesi tumboni.

4. Kutumia mpira wa kadanda, ila usio mgumu. Mlaze mtoto kwenye tumbo, kisha ufanye kana kwamba unauviringisha mpira na kumruhusu mtoto kuzunguka pande na pande. Hii ni mbinu bora ya kutoa hewa tumboni mwa mtoto.
5. Mama pia anaweza kumlaza mtoto chini kwa mgongo, kisha kunyonga miguu kana kwamba anaendesha baiskeli. Mbinu hii pia ni maarufu kwa kusaidia kutoa hewa tumboni mwa mtoto mchanga.
Wakati wa kuwa na shaka
Mara nyingi, hewa tumboni kwa watoto wachanga, ni jambo la kawaida na linaloweza kutibika. Ila katika visa vya nadra, huenda hali hii ikawa ishara ya kwanza kubwa ya tatizo la kuchakata chakula. Hakikisha kuwasiliana na daktari wa mwanao unapogundua kuwa ana:
- Tatizika kuenda msalani, kuenda choo chenye damu
- Tapika kwa sana
- Anasumbua mara kwa mara na hatulii hata baada ya kumlisha
- Ana joto jingi mwilini
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Hatua Katika Ukuaji Wa Mtoto Wa Miezi Minne