Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Jinsi Ya Kutumia Vidonge Kutoa Mimba Na Athari Kwa Mwanamke

3 min read
Jinsi Ya Kutumia Vidonge Kutoa Mimba Na Athari Kwa MwanamkeJinsi Ya Kutumia Vidonge Kutoa Mimba Na Athari Kwa Mwanamke

Kutoa mimba salama kunafanyika kwenye kituo cha hospitali chini ya usimamizi wa daktari mwenye cheti ili kudumisha usalama wakati wote.

Kuavya mimba ni suala tata lililozua mazungumzo tofauti duniani kote. Je, mwanamke anapaswa kutoa mimba? Kwa walio upande wa maamuzi, ambapo wanampa mwanamke uhuru wa kufanya uamuzi wake na kuunga mkono uavyaji wa mimba. Huku upande mwingine ukiwa na wanaounga mkono uhai, na kusema kuwa hakuna kiumbe kinachopaswa kuuliwa, na kupinga kuavya mimba.

Nchi nyingi zinapinga uavyaji wa mimba, ila kuna nchi chache zilizopitisha kuwa mwanamke anaweza kuamua anachotaka kufanya na mwili wake. Na kwa njia hii kuwasilisha njia salama za kuwawezesha wanawake kutoa mimba kwa njia salama. Kuna idadi kubwa ya wanawake wanaopoteza maisha kila mwaka wakijaribu kutoa mimba kwa njia zisizosalama. Kwa kuwasilisha njia salama, nchi zinanusuru maisha ya wanawake wengi. Njia salama zinawasaidia wanawake kuweza kutunga mimba tena kwani uterasi zao hazikuathiriwa katika mchakato wa kuavya mimba. Njia zisizo salama zinamweka mwanamke katika hatari ya kupoteza maisha yake ama kuharibu mji wake wa mtoto.

Kutoa Mimba Kutumia Vidonge

kutoa mimba

Kuna njia nyingi za kuavya mimba, kama vile kutumia vidonge vya kutoa mimba ama kutumia mashine kutoa kiinitete kwa kuingiza sindano kwa uke wa mwanamke.

Jambo la kwanza ni kuwasiliana na daktari kisha kuwa na kipindi cha ushauri. Kumbuka kuwa njia zote hizi zinafanyika kwenye kituo cha afya na kufanywa na daktari mwenye cheti. Ni vigumu kupata vidonge vya kuavya mimba nje ya vituo vya afya, kwa hivyo daktari peke yake ndiye anayeweza kuziwasilisha kwa mwanamke. Mara nyingi kama njia ya kipekee ya kunusuru maisha ya mama kama mwanamke ana mimba yenye hatari ama alipata mimba kwa njia kama vile kubakwa ama sababu zingine zinazokubalika kisheria.

Katika kipindi na daktari, atathibitisha mambo haya:

  • Kuwa utaratibu huu ni sawa kwa mwanamke
  • Kueleza utaratibu wa kuavya mimba unavyofanyika na athari zake
  • Kujadili mbinu za kupanga uzazi baada ya utaratibu huu
  • Kufanyiwa vipimo vya mwili na ushauri
  • Jinsi ya kutumia vidonge vya kuavya mimba

Utaratibu wa kutoa mimba kutumia vidonge huwa:

Chukua kidonge cha kwanza cha mifepristone. Baada ya masaa 24 hadi 48, chukua kidonge cha pili cha misoprostol. Kwa kawaida, utoaji wa mimba huchukua masaa manne hadi sita kuanza kuvuja damu baada ya kuchukua kidonge cha pili. Kumbuka kuwa utaratibu huu unafanyika kwenye kituo cha hospitali kwa usimamizi wa daktari. Mwanamke anapaswa kuchukua siku moja ama mbili kupumzika baada ya utaratibu huu.

kutoa mimba

Kinachofanyika baada ya kuchukua dawa

Mwanamke huhisi mambo haya baada ya kuchukua dawa za kuavya mimba:

  • Kichefuchefu
  • Maumivu vya kichwa
  • Maumivu makali ya tumbo
  • Kutapika

Baada ya kati masaa mawili hadi sita, damu huanza kutoka. Kiwango cha damu kinachotoka siku ya kwanza na ya pili huwakimekolea rangi ama cha hudhurungi. Rangi huanza kubadilika siku zinavyozidi kupita na pia kiwango kupungua. Kuvuja damu kunapozidi zaidi ya wiki mbili, mwanamke anapaswa kurudi kwenye kituo cha afya.

Chanzo: WebMD

Soma Pia: Sifa Za Hedhi Baada Ya Kuavya Mimba

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Abortion
  • /
  • Jinsi Ya Kutumia Vidonge Kutoa Mimba Na Athari Kwa Mwanamke
Share:
  • Njia 3 Salama Za Kuavya Mimba: Sindano Ya Kutoa Mimba Inatumika Vipi?

    Njia 3 Salama Za Kuavya Mimba: Sindano Ya Kutoa Mimba Inatumika Vipi?

  • Matokeo 7 Mwanamke Anayoshuhudia Baada Ya Kutoa Mimba

    Matokeo 7 Mwanamke Anayoshuhudia Baada Ya Kutoa Mimba

  • What Does It Mean To Have An Abortion?

    What Does It Mean To Have An Abortion?

  • Njia 3 Salama Za Kuavya Mimba: Sindano Ya Kutoa Mimba Inatumika Vipi?

    Njia 3 Salama Za Kuavya Mimba: Sindano Ya Kutoa Mimba Inatumika Vipi?

  • Matokeo 7 Mwanamke Anayoshuhudia Baada Ya Kutoa Mimba

    Matokeo 7 Mwanamke Anayoshuhudia Baada Ya Kutoa Mimba

  • What Does It Mean To Have An Abortion?

    What Does It Mean To Have An Abortion?

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2022 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it