Kulingana na kiwango cha damu ambacho mwanamke ana vuja katika mimba, huenda ikawa ishara ya hatari. Kutoka damu wakati wa mimba changa sio jambo la kawaida. Kwani mwanamke anapo tunga mimba, yai haliachiliwi kutoka kwa ovari. Na kumaanisha kuwa hawezi shuhudia vipindi vyake vya kawaida vya hedhi. Kwa hivyo kuvuja damu huenda kuka ashiria kuwa kuna tatizo mahali. Je, ni visababu gani vinavyo mfanya mwanamke kutoka damu wakati wa mimba changa?
Mimba 15 kati ya 100 huharibika. Wanawake wenye mimba wana shauriwa kuwa makini na kuwa na mawasiliano ya kila mara na madaktari wao. Wanapo gundua kuwa kuna jambo lisilo enda inavyo tarajiwa.
Kuna sababu mbalimbali zinazo sababisha kutoka damu wakati wa mimba changa

Kuharibika kwa mimba ni kawaida katika miezi ya kwanza miwili ya mimba. Mara nyingi, mwanamke huenda akakosa kujua kuwa ni mimba ina haribika. Na kudhani kuwa ni kuvuja kwa damu kwa kawaida. Kuharibika kwa mimba huenda kuka sababishwa na magonjwa ya zinaa, mwanamke anapo fanya kazi nyingi na kuushinikiza mwili wake. Mawazo mengi ama hata kula chakula chenye sumu.
Kuvuja damu baada ya kuharibika kwa mimba huenda kuka hatarisha maisha ya mama. Ana stahili kuenda kwenye hospitali anapo gundua kuwa ameanza kuvuja damu.
- Kujipandikiza kwa yai/ damu ya implantation

Baada ya yai kurutubishwa na manii. Linajipandikiza kwenye kuta za uterasi na damu inatolewa. Hii ni mojawapo ya ishara za mapema za mimba. Huenda ika sawasishwa na damu ya kipindi cha hedhi. Ila kuna tofauti. Damu ya implantation huwa kiasi kidogo, ya pinki na isiyo jaza pedi. Pia ina shuhudiwa kwa kipindi cha kati ya siku moja hadi tatu. Mwanamke anapo vuja damu inayo jaza pedi, anapaswa kuwasiliana na daktari, huenda akawa ana poteza mimba.
- Kutunga mimba nje ya mji wa mtoto/ uterasi

Hata ingawa sio kawaida, kuna uwezekano wa mwanamke kutunga mimba nje ya uterasi. Mimba ya aina hii ni hatari kwa afya ya mama. Inaweza tungwa kwenye mirija ya ovari ama endometria. Mimba kukua kwenye mirija ya ovari ina shinikiza mirija hiyo na huenda ika isababisha ipasuke. Hali hii inafaa kurekebishwa kwa kasi kwani kuvuja damu nyingi kuna madhara hasi kwa afya ya mama. Hiki ni chanzo kingine cha kutoka damu wakati wa mimba changa.
Mbali na sababu hizi, mwili ulikuwa umezoea kuvuja damu katika kipindi fulani kila mwezi. Ikiwa ni kiasi kidogo cha damu, huenda likawa sio ishara ya hali nyeti.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Jinsi Ambavyo Mwanamke Anaweza Kuongeza Nafasi Zake Za Kutunga Mimba